Simamia kalenda yako

Fanya mabadiliko kwenye mipangilio yako ya kuweka nafasi ili kuepuka kughairi nafasi zilizowekwa.
Na Airbnb tarehe 22 Feb 2024
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 22 Feb 2024

Wageni wanaweza kupata tangazo lako katika matokeo ya utafutaji ndani ya saa 24 baada ya kulichapisha. Kalenda yako imefunguliwa kabisa kwa chaguo msingi. Ni muhimu kusasisha upatikanaji wako mara moja, kisha uchague sera yako ya kughairi na jinsi wageni wanavyoweza kuweka nafasi kwenye sehemu yako.

Kusasisha upatikanaji wako

Zuia kalenda yako kwa tarehe ambazo huwezi kukaribisha wageni. Hatua hii huficha tangazo lako lisionekane kwenye matokeo ya utafutaji na inakusaidia kuepuka kughairi nafasi zilizowekwa.

"Unatoa huduma kwa mgeni wako na unahitaji kufanya kila kitu kadiri unavyoweza kuheshimu huduma hiyo," anasema Felicity, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji na Mwenyeji Bingwa huko New South Wales, Australia.

Chukua hatua hizi ili usimamie upatikanaji wako.

  • Weka ni mapema kiasi gani wageni wanaweza kuweka nafasi. Unaweza kukubali nafasi zilizowekwa siku hiyo hiyo hadi wakati fulani, au kuhitaji wageni waweke nafasi hadi siku saba kabla ya kuingia.

  • Kulandanisha kalenda zako. Kulandanisha kalenda yako ya Airbnb na kalenda nyingine zozote hukusaidia kusimamia ratiba yako ya kukaribisha wageni na kuepuka kuweka nafasi mara mbili.

  • Chagua sera ya kughairi. Unaamua ni jinsi gani unaweza kusimamia utaratibu uliowekwa au kulegeza masharti ikiwa mgeni ataghairi. Chagua kinachokufaa.

  • Weka kalenda yako ikiwa na taarifa za hivi karibuni. Hii husaidia kuzuia kughairi nafasi zilizowekwa na kupata adhabu na ada zinazohusiana na kufanya hivyo.

Kuamua wakati ambao wageni wanaweza kukaa

Amua ni muda gani unataka wageni waingie na kutoka na muda gani unapendelea kati ya nafasi zilizowekwa.

  • Weka kima cha chini na cha juu cha muda wa kukaa. Unaweza kuunda urefu mahususi wa safari kwa tarehe mahususi. Fuata sheria na kanuni za mahali ulipo kila wakati.

  • Amua muda wako wa maandalizi. Je, wewe au wafanya usafi wako mnahitaji muda gani kabla mgeni mwingine hajawasili? Wenyeji wengi huwaruhusu wageni kuingia siku hiyo hiyo wageni wengine wanapotoka. Wengine huzuia usiku mmoja au mbili kabla na baada ya kila nafasi iliyowekwa kukamilika.

  • Kuweka muda wa kuingia na kutoka. Chagua ni mapema kiasi gani wageni wanaweza kuwasili na wanaweza kuchelewa kuondoka kwa kiasi gani. Pia una chaguo la kuweka muda wa mwisho wa kuingia ikiwa hutaki wageni wawasili wakiwa wamechelewa sana.

Kuchagua jinsi wageni wanavyoweza kuweka nafasi

Unaweza kukubali uwekaji nafasi kiotomatiki au kwa kufanya wewe mwenyewe. Ni rahisi kusasisha mpangilio huu wakati wowote.

  • Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo kinamruhusu mtu yeyote anayekidhi mahitaji yako ya mgeni na kukubali sheria za nyumba yako kuweka nafasi kiotomatiki kwenye tarehe zinazopatikana katika kalenda yako. Wageni bado wanaweza kuwasiliana nawe ikiwa wana maswali.

  • Maombi ya kuweka nafasi hukupa saa 24 za kukubali au kukataa ombi la mgeni kabla ya muda wake kuisha. Hali hii inakupa muda wa kuthibitisha kwamba wageni wanajua sheria au vipengele vyovyote maalumu, kama vile ngazi zenye mteremko mkali zinazoelekea kwenye mlango mmoja pekee uliopo. Ukiruhusu muda wa maombi ya kuweka nafasi uishe, tarehe zilizoombwa zinazuiwa kwenye kalenda yako hadi utakapozifungua tena.

Bila kujali ni njia gani ya kuweka nafasi unayochagua, sasisha kalenda yako ili kusaidia kuzuia migongano wa ratiba na kughairi.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
22 Feb 2024
Ilikuwa na manufaa?