Kutumia ujumbe ulioratibiwa kuokoa muda

Fanya mawasiliano ya wageni wako yawe ya kiotomatiki kuanzia wakati wa kuingia hadi kutoka.
Na Airbnb tarehe 19 Nov 2020
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 1 Mei 2024

Nyenzo ya ujumbe ulioratibiwa inakusaidia kushiriki kiotomatiki taarifa muhimu na wageni katika nyakati mahususi, kama vile siku ya kuingia. Inakuruhusu kuunda ujumbe wa kawaida na kuuratibu kutuma wakati ambapo wageni wana uwezekano mkubwa wa kutaka taarifa hiyo.

Unaweza pia kuunda majibu ya haraka, violezo vifupi vinavyotumiwa kushughulikia maswali ya kawaida, ili kuokoa muda unapotuma ujumbe kwa wageni.

Jinsi ya kuweka mahususi na kuratibu ujumbe

Nenda kwenye mipangilio ya ujumbe kwenye kichupo chako cha Ujumbe ili kuandika na kuratibu ujumbe.

Unaweza kufanya ujumbe huu uwe mahususi kwa kuweka misimbo mifupi. Vishika nafasi hivi vinachukua taarifa kutoka kwenye tangazo lako na nafasi iliyowekwa na mgeni wako, kama vile sheria za nyumba yako na jina lake na tarehe ya kuingia. Hakikisha kwamba maelezo ya tangazo lako yamekamilika na ni ya hivi karibuni kwa sababu ujumbe ulio na misimbo mifupi mitupu hautatumwa kwa usahihi.

Tumia menyu kunjuzi kuweka misimbo mifupi. Unapomaliza kuandika, ratibu ujumbe kwa kuchagua ni hatua gani ya mgeni itakayofanya uutume. Unaweza kuhariri, kuruka au kutuma ujumbe mapema kuliko ulivyoratibiwa kadiri inavyohitajika.

Hapa kuna jinsi unavyoweza kutumia misimbo mifupi katika ujumbe ulioratibiwa:

Mpendwa [jina la kwanza la mgeni],

Asante kwa kuweka nafasi! Tunafurahi kukukaribisha tarehe [tarehe ya kuingia]. Tafadhali shiriki taarifa ya safari yako ili tuweze kuratibu mchakato mzuri wa kuingia, ambao kwa kawaida ni saa [muda wa kuingia] au baadaye.

Hapa kuna maelezo mafupi kuhusu eneo: [kitongoji]

Hivi ni vidokezi vichache vya kutembelea: [kutembelea]

Unaweza kupata mapendekezo muhimu ya kutembelea [jiji] katika kitabu chetu cha mwongozo, ambacho kipo hapa: [kitabu cha mwongozo]. Siku chache kabla ya safari yako, tutashiriki maelezo ya kuingia. Tafadhali tujulishe ikiwa una maswali yoyote.

Wakati gani wa kuratibu ujumbe

Unaweza kuratibu ujumbe wakati wowote. Zingatia nyakati hizi kutuma taarifa muhimu wakati wageni wanazihitaji.

  • Muda mfupi baada ya kuweka nafasi: Ujumbe wa shukrani wa papo hapo baada ya kuweka nafasi huwajulisha wageni kwamba umepokea ombi lao na unatoa maelezo na vidokezi kwa ajili ya ukaaji wao unaokaribia.
  • Kabla ya kuingia: Wakumbushe wageni kuhusu ukaaji wao unaokaribia ili waweze kujiandaa kwa ajili ya kuwasili. Unaweza kuratibu ujumbe huu hadi siku 14 kabla ya kuingia.
  • Siku ya kuingia: Ingawa huenda tayari umeshiriki maelekezo ya kuingia, wageni wengi wanaona ni muhimu kupokea taarifa muhimu tena siku ya kuingia, ikiwemo maelekezo.
  • Siku ya kwanza ya ukaaji: Wasiliana na mgeni ili kuthibitisha kwamba kila kitu kiko sawa na uweze kujibu maswali yoyote ambayo anaweza kuwa nayo.
  • Siku baada ya kutoka: Washukuru wageni wako kwa kukaa nawe na kuwakumbusha kuandika tathmini.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
19 Nov 2020
Ilikuwa na manufaa?