Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuweka sheria za nyumba zinazofaa

  Saidia kulinda nyumba yako na kuunda mazingira bora kwa wageni.
  Na Airbnb tarehe 1 Des 2020
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 9 Mac 2023

  Sheria za nyumba yako zinaweka matarajio kwa wageni na kuwadokezea mtindo wako wa kukaribisha wageni. Sheria hizi pia huwasaidia wageni watathmini iwapo sehemu yako inawafaa kabla ya kuiwekea nafasi.

  Kuchagua sheria za kawaida za nyumba yako

  Wenyeji wanaweza kuchagua kutoka kwa seti ya sheria za kawaida za nyumba katika maeneo haya:

  • Wanyama vipenzi
  • Matukio
  • Uvutaji sigara, uvutaji wa mvuke wa sigara na sigara za kielektroniki
  • Saa za utulivu
  • Saa za kuingia na kutoka
  • Idadi ya juu ya wageni
  • Kupiga picha na kurekodi video za kibiashara

  Sheria za nyumba yako zinaangaziwa katika maeneo manne: kwenye ukurasa wa tangazo lako, kwenye skrini wakati wageni wanaweka nafasi kwenye sehemu yako, kwenye barua pepe ya wageni ya Fungasha Mizigo Yako na kwenye Mwongozo wa Kuwasili ambao wageni hupokea kabla ya safari yao.;

  Jinsi sheria za nyumba zinavyosaidia kukulinda

  Ukiwa na sheria za msingi kwa ajili ya wageni, sheria yoyote unayochagua kutoka kwenye orodha ya sheria za kawaida za nyumba inaweza kutekelezwa. Ikiwa mgeni atakiuka sheria ya nyumba, hatua yako ya kwanza inapaswa kuwa kuwasiliana na mgeni huyo kisha ujaribu kutatua tatizo hilo moja kwa moja. Ikiwa utashindwa kutatua tatizo hilo, wasiliana na kituo cha Usaidizi wa Jumuiya ili upate usaidizi.

  Kuandika sheria za ziada

  Ikiwa una matakwa maalumu ambayo hayajawekwa katika seti ya sheria za kawaida za nyumba, unaweza kuyaandika chini ya sheria za ziada. Ni jambo bora kuepuka kuwachosha wageni kwa kuwapa sheria nyingi kupita kiasi, lakini unaweza kuongeza chochote muhimu kuhusu desturi za mahali ulipo au afya na usalama. Mifano michache kutoka kwa Wenyeji:

  • "Hatuna lami, tuna matope, kwa hivyo tunaomba viatu vivuliwe kwa sababu nyumba ina zulia," anasema Juliette, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huko Nairobi, Kenya.
  • "Tafadhali funga na uweke kufuli kwenye madirisha na milango yote unapokuwa unaondoka chumbani," anasema Dave na Deb, Wenyeji huko Edmonton, Kanada.
  • "Tafadhali usiweke chakula chochote kwenye chumba cha kulala," anasema Momi, Mwenyeji huko Honolulu.

  Sheria zote za ziada lazima zipatane na sera na masharti ya Airbnb, ikiwemo masharti yetu ya huduma na sera ya kutobagua.

  Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Airbnb
  1 Des 2020
  Ilikuwa na manufaa?