Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Jinsi Airbnb inavyowalinda wenyeji

  Pata maelezo kuhusu ulinzi wa ndani wa Airbnb kwa ajili ya wenyeji.
  Na Airbnb tarehe 4 Feb 2020
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 7 Jun 2021

  Vidokezi

  • Madai ya uharibifu na visa vya usalama ni nadra, lakini Airbnb inachukua tahadhari ili kuwalinda wenyeji na wageni

  • Garantii ya Mwenyeji ya Airbnb na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji zinajumuishwa kwenye kila nafasi inayowekwa, zikiweza kushughulikia hadi USD 1,000,000 chini ya kila mpango

  • Usaidizi wa kimataifa unapatikana saa 24 kwa lugha 11 tofauti

  • Gundua mambo zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kugundua ulimwengu wa kukaribisha wageni

  Iwe umeanza kukaribisha wageni hivi karibuni au umeanza tu kufikiria wazo hilo, unaweza kuwa na maswali kuhusu kulinda sehemu yako na mali wakati watu usiowajua wanakaa nyumbani kwako. Madai ya uharibifu na visa vya usalama ni nadra sana, lakini inaweza kukusaidia kujua kwamba Airbnb imeweka hatua kadhaa za ulinzi ili kuwalinda wenyeji na wageni.

  "Tulikuwa na mashaka kuhusu kuwakaribisha wageni kwenye nyumba," mwenyeji Guy kutoka San Francisco anasema kuhusu wasiwasi wake kabla ya kuanza kukaribisha wageni. "Lakini ulinzi ambao Airbnb inatoa ulitupa ujasiri wa kuitangaza nyumba na kuijaribu." Na uhakika wake ulimlipa. "Tumekuwa na wageni zaidi ya 120 na hatujawahi kufanya madai."

  Utambulisho wa wageni na matakwa mengine

  Wageni wanatoa jina kamili, tarehe ya kuzaliwa, nambari ya simu, anwani ya barua pepe na taarifa ya malipo kwa Airbnb kabla ya kuweka nafasi. Wenyeji pia wana chaguo la kuwahitaji wageni waipe Airbnb kitambulisho cha serikali kabla ya kuweka nafasi.

  Unahimizwa kuweka sheria zako mwenyewe za nyumbani—kwa mfano, weka maelezo ya vizuizi vyovyote kwa wanyama vipenzi na idadi ya wageni. Wageni wote wanahitajiwa wakubaliane na sheria za nyumba yako kabla ya kuweka nafasi. Ikiwa tangazo lako lilishikiwa nafasi papo hapo, kumbuka kwamba unaweza kutumia fursa ya kughairi bila adhabu uhitaji ukitokea.

  Wasifu na tathmini

  Mbali na amani ya akili ambayo uthibitisho wa utambulisho hutoa, Airbnb inakusaidia kuwajua wageni kabla hawajaweka nafasi. Unaweza kutazama wasifu wao na usome tathmini kutoka kwa wenyeji wa zamani. Na kwa kuwa wenyeji na wageni wanaweza tu kuandikiana tathmini baada ya ukaaji kukamilika, unaweza kuwa na uhakika kwamba maoni unayosoma yanategemea uzoefu halisi. Unaweza pia kutumia zana salama ya kutuma ujumbe ya Airbnb kuuliza maswali na kuweka matarajio wakati wowote kabla ya ukaaji wa mgeni.

  Ulinzi ambao Airbnb inatoa ulitupa uhakika wa kuitangaza nyumba na kuijaribu.
  Guy,
  San Francisco

  Ulinzi wa uharibifu wa mali

  Garantii ya Mwenyeji* ya Airbnb hutoa ulinzi bila gharama ya ziada, wa hadi USD 1,000,000 katika uharibifu wa mali, kwa kila nafasi iliyowekwa. Madai yanaweza kuandikishwa moja kwa moja kupitiaKituo cha Usuluhishi cha Airbnb.

  Usalama wa akaunti

  Airbnb huchukua hatua kadhaa za kulinda akaunti yako, kama vile kuhitaji uthibitisho wa ziada wakati mtu anajaribu kuingia kwa kutumia simu mpya au kompyuta nayo inakutumia arifa za akaunti mabadiliko yanapofanywa. Maadamu unakaa kwenye tovuti katika mchakato mzima—kuanzia mawasiliano, hadi kuweka nafasi, hadi malipo—unalindwa na sera za Airbnb na Garantii ya Mwenyeji.

  Bima dhidi ya ajali

  Airbnb pia hutoa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji* bila malipo inayoshughulikia madai ya dhima hadi USD 1,000,000. Bima hii ni kwa ajili ya tukio nadra ambapo mtu anaandikisha madai dhidi yako ya uharibifu wa mali ya mgeni au majeraha yanayotokea kwenye nyumba yako wakati wa ukaaji.

  • Inatumika kiotomatiki kwa kila nafasi iliyowekwa
  • Madai yanaweza kuandikishwa moja kwa moja kupitia Airbnb

  Usaidizi wa saa 24

  Timu ya kimataifa ya Airbnb iko tayari saa 24 kwa lugha 11 tofauti kukupa msaada wa:

  • Usaidizi wa kuweka tena nafasi
  • Kurejesha fedha
  • Kurudishiwa gharama
  • Garantii ya Mwenyeji na madai ya bima
  • Upatanishi

  Kukiwa na ulinzi huu uliowekwa pamoja na baadhi yahatua za kimsingi za usalama kwa upande wako, unaweza kuanza kukaribisha wageni ukiwa na uhakika. Kwa maelezo zaidi kuhusu njia muhimu ambazo Airbnb hutumia kuwaweka wenyeji na wageni salama, tembelea Ukurasa wa Uaminifu na Usalama wa Airbnb.

  *Garantii ya Mwenyeji ya Airbnb na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji hazitumiki kwa wenyeji ambao hutoa malazi kupitia Airbnb Travel, LLC, wenyeji walio China Bara, wenyeji nchini Japani, wenyeji wa matukio, au wenyeji wa jasura. Garantii ya Mwenyeji ya Airbnb haihusiani na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji au Airbnb UK Services Limited.

  Taarifa iliyo katika makala hii inaweza kuwa imebadilika tangu kuchapishwa.

  Vidokezi

  • Madai ya uharibifu na visa vya usalama ni nadra, lakini Airbnb inachukua tahadhari ili kuwalinda wenyeji na wageni

  • Garantii ya Mwenyeji ya Airbnb na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji zinajumuishwa kwenye kila nafasi inayowekwa, zikiweza kushughulikia hadi USD 1,000,000 chini ya kila mpango

  • Usaidizi wa kimataifa unapatikana saa 24 kwa lugha 11 tofauti

  • Gundua mambo zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kugundua ulimwengu wa kukaribisha wageni

  Airbnb
  4 Feb 2020
  Ilikuwa na manufaa?