MUHTASARI WA BIMA YA JAPANI
Bima ya Ulinzi ya Tukio
Bima ya Ulinzi ya Tukio ni nini?
Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Tukio huwapa Wenyeji wa tukio ulinzi wa dhima ya jeraha la mwili au uharibifu wa mali kwa wageni au wahusika wengine kutokana na ajali wakati wa tukio lililoandaliwa na Mwenyeji. Mpango wetu wa Bima ya Ulinzi ya Tukio hauwalindi Wenyeji kutokana na uharibifu au upotezaji wa mali yao wenyewe unaotokea wakati wa tukio.
Mpango wetu wa Bima ya Ulinzi ya Tukio nchini Japani hutoa ulinzi chini ya sera inayotolewa na Sompo Japan Insurance Inc. bila gharama za ziada kwa Wenyeji. Ili kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuwasilisha ombi la malipo chini ya mpango wa Bima ya Ulinzi ya Tukio, tafadhali angalia taarifa iliyo hapa chini.Nchi zilizojumuishwa
Ulinzi wa mpango wetu wa Bima ya Ulinzi ya Tukio huwajumuisha Wenyeji ulimwenguni kote, isipokuwa kwa maeneo yanayolengwa na sheria za vikwazo za Marekani. Bima ya Ulinzi ya Tukio nchini Japani inatolewa na Sompo Japan Nipponkoa Insurance Inc. chini ya sera tofauti. Vikomo na masharti tofauti ya ulinzi yanaweza kutumika.
Ulinzi huanza na kumalizika lini?
Muda wa sasa wa sera kwenye mpango wa Bima ya Ulinzi ya Tukio ulianza tarehe 31 Julai, 2023 na unaisha tarehe 31 Julai, 2024.
Je, ni nani anayestahiki bima?
Wenyeji wa Tukio wanalindwa chini ya mpango wa Bima ya Ulinzi ya Tukio ikiwa kisa kinachosababisha dhima ya kisheria ya madai ya jeraha la mwili au uharibifu wa mali unatokea wakati wa tukio linalotolewa na mwenyeji ndani ya kipindi cha sera. Tukio linafasiliwa kuwa ni shughuli inayotolewa na Mwenyeji wa tukio na kufikiwa kupitia tovuti au programu ya Airbnb. Mwenyeji wa tukio hufasiliwa kuwa ni mtu au shirika lililoidhinishwa kutangaza tukio kwenye tovuti au programu ya Airbnb. Kwa madhumuni ya fasili hii, Mwenyeji wa tukio pia ataweza: (i) kujumuisha mhusika mwingine ambaye anapanga utaratibu wa safari au kupanga tukio moja au zaidi kwa wageni wa Airbnb, hata kama haandai tukio moja kwa moja na (ii) Mwenyeji Mwenza ambaye anatoa huduma zinazohusiana na tukio na wahusika fulani wengine ambao wana mkataba na Mwenyeji wa tukio ili kutoa eneo linalohusiana na tukio.
Vikomo vya dhima
Mpango wetu wa Bima ya Ulinzi ya Tukio hutoa bima yenye kikomo cha hadi JPY ¥ 100,000,000 kwa kila tukio.
Ni nini ambacho Bima ya Ulinzi ya Tukio hailindi?
Bima ya Ulinzi ya Tukio haijumuishi:
Madai ya bima
Tafadhali ijulishe Airbnb mara moja ikiwa utafahamu kuhusu jeraha lolote la mwili au uharibifu wa mali ambao unaweza kulindwa chini ya sera hii.
Muhtasari huu wa Bima ya Ulinzi ya Tukio haujumuishi masharti yote ya sera ya bima. Ili kuomba nakala ya sera ya bima, tafadhali wasiliana na Aon Japan Ltd. na ujumuishe taarifa za akaunti yako ya Airbnb.