Maboresho ya kukusaidia kusimamia na kukuza biashara yako
Ni rahisi zaidi kuliko hapo awali kuendelea kuwa na ushindani, kuweka bei kwa busara na kuwasiliana kwa ufanisi kupitia maboresho ya hivi karibuni ya Airbnb kwenye zana za kukaribisha wageni. Pia tunakuletea vipengele vya kuwasaidia wageni kugundua matangazo ambayo huenda wangekosa na kuwaruhusu kuweka nafasi kwa USD 0 wakati wa kuweka nafasi, bila gharama ya ziada kwako.* Utaona maboresho haya katika programu yako kuanzia sasa na mengine yatapatikana mapema mwaka ujao.
Weka bei kwa busara na upange mapema
Nyenzo hizi zinakusaidia kuongeza mapato na kuepuka ughairi wa dakika za mwisho.
Sera za kughairi zinazobadilika: Weka sera tofauti za kughairi kwa tarehe mahususi, kama vile sikukuu au misimu isiyo na shughuli nyingi. Unaweza kufikiria kutoa sera ya kughairi inayoweza kubadilika zaidi katika miezi yako yenye shughuli chache ili kuwavutia wageni, lakini uendelee na sera yako ya kawaida wakati wa msimu wenye shughuli nyingi.**
Vidokezi vya bei vilivyoboreshwa: Pata vidokezi vya bei kwa tarehe hadi mwaka mmoja mapema na utumie vidokezi vyote kwa mguso mmoja tu. Vidokezi vya bei hutumia sifa za nyumba yako, ikiwemo eneo, vistawishi na nafasi zilizowekwa hapo awali, pamoja na bei za hivi karibuni za nyumba nyingine katika eneo lako.**
Hakiki za bei ya safari: Angalia kile ambacho wageni watalipa na makadirio ya mapato yako unapohariri bei yako ya kila usiku kwa usiku mmoja au nyingi.
Shiriki video na vidokezi vya mtu mwenyeji
Wasiliana na wageni kwa kutuma ujumbe mpya wa video na mapendekezo ya mwenyeji.
Ujumbe wa video: Wasaidie wageni waielewe sehemu yako kwa kushiriki video katika ujumbe. Unaweza kutuma ziara ya nyumba kwa wageni kabla ya kuingia au kuweka mafunzo ya kuchoma nyama kwenye ujumbe wako wa makaribisho.
Mapendekezo ya mwenyeji: Tuma kadi ya kidijitali kwa urahisi ukionyesha kitabu chako cha mwongozo au Tukio au Huduma kwenye Airbnb moja kwa moja kwenye ujumbe wako, kwa miguso michache tu. Unaweza pia kuweka kiungo kwenye tukio au huduma na wageni wako wataona kadi iliyo na pendekezo hilo.
Fuatilia utendaji
Kuanzia mwaka ujao, pata grafu zilizo rahisi kusoma kwenye dashibodi yako ya mapato ili uelewe vizuri utendaji wa tangazo.
Dashibodi ya mapato iliyosasishwa: Angalia mienendo ya mapato mwaka baada ya mwaka na ulinganishe utendaji wa msimu katika kichupo kipya kabisa. Kwa mfano, angalia jinsi mapato yako ya mwezi Novemba mwaka uliopita yanavyolinganishwa na mapato yanayotarajiwa mwezi Novemba mwaka huu.***
Dumisha mpangilio
Maboresho mawili ya kalenda yanakusaidia kufuatilia ratiba yako.
Maelezo ya usiku uliozuiwa: Sasa unaweza kuweka vikumbusho kwenye usiku uliozuiwa na uone kwa ufupi kwa nini umezuiwa wakati huo katika siku zijazo.
Onyesho la sarafu lililofupishwa: Bei zozote ndefu za usiku zitafupishwa kwenye kalenda yako. Kwa mfano, peso za Kolombia $35,103.42 zitaonekana kama $35.1K.
Gundua maboresho ili kuwasaidia wageni kuweka nafasi
Wageni sasa wanaweza kufikia njia zaidi za kulipa na utafutaji mahiri.
Weka Nafasi Sasa, Lipa Baadaye: Wageni wana chaguo la kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa inayostahiki na kulipa USD 0 wakati wa kuweka nafasi. Hii haina athari kwenye ratiba yako ya kupokea malipo. Machaguo yanayoweza kubadilika zaidi kwa ajili ya wageni pia yanaweza kusababisha kuwekewa nafasi zaidi kwa ajili ya wenyeji. Zaidi ya asilimia 60 ya wageni walichagua kutumia chaguo hili la malipo wakati wa kulipa kwa nafasi zilizowekwa zinazostahiki.****
Utafutaji mahiri: Wakati wa kutafuta sehemu ya kukaa, wageni huona machaguo zaidi ya nyumba nje ya vigezo vyao vya utafutaji. Kwa mfano, tutaonyesha nyumba zilizo na bei zinazofanana au vistawishi tofauti au sehemu za kukaa katika miji ya karibu kwa bei ya chini, hivyo kuwasaidia wageni kupata machaguo mazuri ambayo huenda wangekosa.
Ramani zilizoboreshwa: Sasa ramani huwaruhusu wageni kuona alamaardhi, vivutio, migahawa ya karibu na kadhalika. Wageni wanaweza kugusa alamaardhi muhimu ili kuona muhtasari na umbali wa kusafiri hadi kwenye nyumba wanayoangalia au ambayo tayari wamewekea nafasi. Baadaye mwaka huu, wageni wanaweza kubadilisha kati ya mitazamo tofauti ya ramani, ikiwemo setilaiti, barabara na usafiri wa umma, kulingana na mapendeleo yao.
*Weka Nafasi Sasa, Lipa Baadaye inapatikana kwa wageni nchini Marekani na itapatikana kwa wageni mahususi ulimwenguni kote kuanzia leo, huku upatikanaji mpana ukitarajiwa mapema mwaka ujao. Nafasi zilizowekwa zinazolipwa kwa Real ya Brazili (BRL), Rupia ya India (INR) au Lira ya Uturuki (TRY) hazistahiki.
**Ughairi unaoweza kubadilika na vidokezi vya bei vilivyoboreshwa vitaanza kutumika kwa idadi ndogo ya wenyeji mwezi Novemba, huku upatikanaji mpana ukitarajiwa mapema mwaka 2026.
***Kichupo kipya cha Utendaji kitapatikana kwa wenyeji mapema mwaka 2026.
****Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb kati ya mwezi Aprili na Juni 2025 kutoka kwenye majaribio ya Weka Nafasi Sasa, Lipa Baadaye nchini Marekani katika nusu ya kwanza ya mwaka.
Bei zinaonyeshwa katika USD. Hali ya utumiaji inaweza kutofautiana kulingana na mahali.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.