Jinsi AirCover kwa ajili ya Wenyeji inavyofanya kazi
AirCover kwa ajili ya Wenyeji hutoa ulinzi kamili kila wakati unapowakaribisha wageni. Inajumuisha uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni, ukaguzi wa nafasi iliyowekwa, bima ya dhima ya Mwenyeji ya USD milioni 1 na ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3, pamoja na ulinzi kwa ajili ya vitu vyako vya thamani, magari yaliyoegeshwa na boti kwenye nyumba yako.
Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni
Jumuiya yetu imejikita katika uaminifu. Hiyo ndiyo sababu wageni wote wanaoweka nafasi lazima wakamilishe mchakato wetu wa uthibitishaji wa utambulisho. Tunapothibitisha utambulisho wa mgeni, tunathibitisha taarifa fulani binafsi, kama vile jina lake la kisheria, anwani, nambari ya simu au maelezo mengine ya mawasiliano.
Mara baada ya mgeni kuthibitishwa, atapata beji iliyothibitishwa na utambulisho. Hii inaonyeshwa kwenye Airbnb kama beji nyekundu yenye alama karibu na picha yake ya wasifu. Aidha, tunaweza kufanya uchunguzi wa uhalifu kwa wageni wanaoishi nchini Marekani.
Pata maelezo zaidi kuhusu uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni
Teknolojia ya ukaguzi wa nafasi iliyowekwa
Sera yetu ya Usumbufu wa Jumuiya inakataza sherehe zisizoidhinishwa na zinazovuruga. Tunatumia teknolojia tunayomiliki ya ukaguzi wa nafasi iliyowekwa ili kusaidia kutekeleza sera hiyo na kupunguza uwezekano wa sherehe zenye kuvuruga.
Mfumo huu unaangalia sababu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na aina ya tangazo linalowekewa nafasi, muda wa ukaaji, umbali wa tangazo kutoka eneo la mgeni na ikiwa nafasi iliyowekwa ni ya dakika ya mwisho, miongoni mwa ishara nyingi zaidi ili kuamua ikiwa nafasi iliyowekwa inapaswa kuzuiwa.
Pata maelezo zaidi kuhusu teknolojia ya ukaguzi wa nafasi zilizowekwa
Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji wa USD milioni 3
Kwa zaidi ya muongo mmoja, Airbnb imetoa ulinzi dhidi ya uharibifu unaoongoza kwenye tasnia kwa Wenyeji. Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, ambao ni sehemu ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji, unajumuisha ulinzi huu ikiwa mgeni hatalipia uharibifu anaosababisha kwenye nyumba au mali yako akiwa anakaa kwenye eneo lako:
- Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3: Hii inajumuisha nyumba yako pamoja na vitu vilivyomo.
- Ulinzi wa sanaa na vitu vya thamani: Tunalinda sanaa, vito na vitu vya kukusanywa, ambavyo vinaweza kurejeshwa ikiwa vimeharibiwa.
- Ulinzi wa magari na boti: Tunatoa ulinzi dhidi ya uharibifu wa magari, boti na vyombo vingine vya majini ambavyo unaegesha au kuhifadhi kwenye nyumba yako.
- Ulinzi dhidi ya uharibifu wa mnyama kipenzi: Tunalipia uharibifu unaofanywa na wanyama vipenzi
- Kufanya usafi wa kina: : Tunatoa fidia kwa ajili ya huduma za kufanya usafi wa ziada zinazohitajika ili kuondoa madoa na harufu ya moshi.
- Ulinzi dhidi ya hasara ya mapato: Tunakufidia mapato yaliyopotea iwapo utaghairi nafasi zilizowekwa za Airbnb ambazo zimethibitishwa kwa sababu ya uharibifu wa mgeni.
- Mawasliiano ya usalama ya saa 24: Endapo utajihisi kwamba hauko salama, programu yetu inakupa ufikiaji wa mbofyo mmoja kwa maafisa wa usalama waliopata mafunzo mahususi, mchana au usiku.
Malipo rahisi
Ikiwa mgeni ataharibu eneo au mali zako, wewe (au Mwenyeji Mwenza aliye na ruhusa kamili za kufikia kwa niaba yako) unaweza kutembelea Kituo chetu cha Usuluhishi ili kuwasilisha ombi la kufidiwa kwa hatua chache tu, kisha ufuatilie kwa urahisi mchakato huo kuanzia kuwasilisha hadi kupokea malipo. Ombi lako litatumwa kwanza kwa mgeni. Mgeni asipojibu au kulipa ndani ya saa 24, utaweza kuihusisha Airbnb. Wenyeji Bingwa (walio na matangazo nje ya jimbo la Washington nchini Marekani) hupata uelekezaji uliopewa kipaumbele na urejeshaji wa fedha wa haraka.
Bima ya dhima ya Mwenyeji ya USD milioni 1
Bima ya dhima ya Mwenyeji, ambayo ni sehemu ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji, hukulinda katika tukio nadra ambapo mgeni atajeruhiwa au mali yake kuharibiwa au kuibwa akiwa anakaa kwenye eneo lako. Watu wanaokusaidia kukaribisha wageni, kama vile Wenyeji Wenza na wafanya usafi, pia wamejumuishwa katika bima hii.
Bima ya dhima ya Mwenyeji hukufidia ikiwa utakutwa unawajibika kisheria kwa:
- Jeraha la mwili kwa mgeni (au wengine)
- Uharibifu au wizi wa mali ya mgeni (au wengine)
- Uharibifu unaosababishwa na mgeni (au wengine) kwenye maeneo ya pamoja, kama vile kumbi za majengo na nyumba zilizo karibu
Ikiwa unahitaji kuwasilisha madai, tumia tu fomu yetu ya kujiunga na bima ya dhima. Tutatuma taarifa unayotoa kwa mtoa bima wetu kampuni nyingine inayoaminika, ambayo itampa mwakilishi ashughulikie madai yako. Atatatua madai yako kulingana na masharti ya sera ya bima.
Ikiwa wewe ni Mwenyeji wa Tukio, unalindwa na bima yetu ya dhima ya Matukio.
AirCover kwa ajili ya Wenyeji ya Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji, Bima ya dhima ya Mwenyeji na Bima ya dhima ya Matukio haziwalindi Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa au Matukio nchini Japani, ambapo Bima ya Mwenyeji ya Japani na Bima ya Ulinzi ya Tukio ya Japani zinatumika au Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa kupitia Airbnb Travel LLC. Kwa Wenyeji waliotoa sehemu za kukaa au Matukio nchini China Bara, Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China unatumika. Kumbuka kwamba vikomo vyote vya malipo vinaonyeshwa katika USD.
Bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio zinadhaminiwa na watoa bima wengine. Ikiwa unakaribisha wageni nchini Uingereza, sera za bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio zinatolewa na Zurich Insurance Company Ltd. na zinapangwa na kutekelezwa bila gharama ya ziada kwa Wenyeji wa Uingereza na Airbnb UK Services Limited, mwakilishi aliyeteuliwa wa Aon UK Limited, ambao wameidhinishwa na kudhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Kifedha. Nambari ya usajili ya Aon katika FCA ni 310451. Unaweza kuangalia maelezo haya kwa kutembelea Rejesta ya Huduma za Fedha au uwasiliane na FCA kupitia nambari 0800 111 6768. Sera za dhima ya Mwenyeji na Matukio ndani ya Aircover kwa ajili ya Wenyeji zinadhibitiwa na Mamlaka ya Maadili ya Kifedha, bidhaa na huduma zilizosalia si huduma zinazodhibitiwa zilizopangwa na Airbnb UK Services Limited. FPAFF609LC
Katika Umoja wa Ulaya, sera hizi zinapangwa na kuhitimishwa bila gharama ya ziada kwa manufaa ya Wenyeji wa Umoja wa Ulaya na Airbnb Marketing Services SLU, mshirika wa nje wa Aon Iberia Correduría de Seguros y Reaseguros, SAU, ambayo imeidhinishwa na kudhibitiwa na Autoridad de Control de la Dirección General de Seguros y Fondos de Pensiones, iliyosajiliwa na nambari tambulishi ya J0170.
Aon Iberia Correduría de Seguros y Reaseguros SAU inafanya kazi kama mpatanishi kwa ajili ya Umoja wa Ulaya, ikishiriki katika usambazaji wa bima katika nchi za Umoja wa Ulaya chini ya mfumo wa uhuru wa huduma ili kutoa huduma chini ya Sheria ya Usambazaji wa Bima ya Uhispania, Maelekezo ya Usambazaji wa Bima na vifungu vingine vya kisheria au vya udhibiti. Bila kuathiri mamlaka ya nchi mwenyeji ambapo huduma za usambazaji wa bima zinatolewa, nchi mwanachama inayohusika na usimamizi wa Aon ni Ufalme wa Uhispania na Mamlaka ya Usimamizi, Kurugenzi Kuu ya Mifuko ya Bima na Pensheni, huko Paseo de la Castellana 44, 28046 – Madrid.
Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji si bima na hauhusiani na bima ya dhima ya Mwenyeji. Kwa matangazo katika jimbo la Washington, wajibu wa kimkataba wa Airbnb chini ya ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unalindwa na sera ya bima iliyonunuliwa na Airbnb. Kwa Wenyeji ambao nchi yao ya makazi ni tofauti na Australia, Masharti haya ya Ulinzi dhidi ya Uharibifu kwa Mwenyeji yanatumika. Kwa Wenyeji ambao nchi yao ya makazi ni nchini Australia, ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji unadhibitiwa na Masharti ya Ulinzi Dhidi ya Uharibifu kwa Mwenyeji kwa Watumiaji wa Australia.
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.