Jinsi ya kukaribisha wageni wako wa kwanza kwenye Airbnb
Unaweza kuwa na maswali kuhusu jinsi ya kujitayarisha kupokea wageni wako wa kwanza. Hivi hapa ni vidokezi vichache kukuwezesha kuanza kwa urahisi.
Toa mchakato rahisi wa kuingia
Weka mchakato ambao ni rahisi na wa kuaminika. Weka maelekezo ya nyumba yako, njia ya kuingia na maelekezo ya kuingia ya hatua kwa hatua katika mwongozo wa kuwasili kwenye tangazo lako. Wageni wengi wanapendelea urahisi wa kuingia wenyewe, ambao unawaruhusu kuingia ndani bila wewe kuwepo.
Wageni wanaweza kufikia maelekezo yako ya kuingia kwenye maelezo ya safari yao saa 48 kabla hawajaratibiwa kuingia au saa 24 kabla ikiwa una sera ya kughairi inayoweza kubadilika.
Tazamia mahitaji ya mgeni
Kila mgeni ni tofauti, lakini wengi wanatarajia kuweza kufikia vitu na taarifa fulani. Chukua hatua hizi ili utoe ukaaji wa starehe.
Weka akiba ya vitu vya msingi. Hivi ni pamoja na taulo, mashuka, mito, sabuni na karatasi ya chooni.
Patikana. Kuwa na mpango wa jinsi utakavyosuluhisha matatizo haraka na kuwakumbusha wageni kwamba wanaweza kuwasiliana nawe ikiwa kuna jambo lolote litakalotokea.
Weka mwongozo wa nyumba. Toa taarifa muhimu, kama vile jinsi ya kufikia intaneti na kutumia vifaa. Weka toleo lililochapishwa ambapo wageni wanaweza kulipata kwa urahisi.
- Weka kitabu cha mwongozo. Shiriki vidokezi vyako vya eneo husika, ikiwemo maeneo ya kula, kununua, kutazama na kujionea maeneo ya nje.
Wasiliana mapema na mara kwa mara
Kila mwingiliano ulio nao na wageni ni fursa ya kuweka matarajio na kuonyesha kwamba unajali mahitaji yao.
Unda mazingira ya ukarimu. Weka kipaumbele kwenye vitendo vya ujumuishi ili kumsaidia kila mgeni ajihisi huru katika sehemu yako. Anza tu kwa kuwauliza wageni kile ambacho kitawasaidia wajisikie wapo nyumbani.
Kuwa mwelewa. Jaribu kuangalia kila hali kwa mtazamo mpya.
Toa majibu haraka. Kuwa na kiwango kizuri cha kutoa majibu hulisaidia tangazo lako lionekane kwenye orodha ya juu katika utafutaji wa wageni kwenye Airbnb. Tumia programu ili uwasiliane haraka na upange ujumbe ulioratibiwa ili utoe taarifa muhimu katika nyakati muhimu, kama vile kuingia.
Hii ni mifano michache ya ujumbe unayoweza kuzingatia kuratibu katika nyakati fulani. Mifano hii hutumia misimbo mifupi, vishika nafasi ambavyo hujaza kiotomatiki maelezo ya nafasi iliyowekwa, ya tangazo na mgeni. Iweke kutoka kwenye menyu kunjuzi, kwa sababu haitafanya kazi ikiwa utaiandika mwenyewe.
Hakikisha sehemu yako ni safi na maridadi
Wageni wanatarajia kukuta sehemu ikiwa safi wanapowasili. Unda utaratibu unaohusisha kusafisha sehemu zote, sakafu na mavazi.
Angalia madoa, uchafu na nywele. Sehemu zinazopuuzwa kwa kawaida ni pamoja na chini ya kitanda, droo za ndani na kwenye mapazia ya dirishani.
Chagua harufu zisizo na marashi makali. Marashi makali ya aina yoyote yanaweza kuwakera wageni. Fungua madirisha wakati wa kusafisha na kutumia dawa za kuua viini zenye madhumuni mengi.
- Ondoa au uhifadhi vitu binafsi. Hii inaweza kusaidia sehemu yako ivutie zaidi na kutokuwa na mparaganyiko.
Omba na utoe tathmini
Wewe na wageni wako mna siku 14 za kila mmoja kumtolea mwingine tathmini baada ya kuondoka. Tathmini zimefichwa hadi wewe na mgeni aliyeweka nafasi mtakapoandika tathmini au kipindi cha siku 14 cha kutoa tathmini kuisha. Wageni pia wanaweza kutoa ukadiriaji wa nyota kwa ajili ya tukio lao kwa ujumla na katika aina sita ndogo: usafi, usahihi, kuingia, mawasiliano, mahali na thamani.
Tathmini zako kadhaa za kwanza ni muhimu sana. Ukadiriaji wako wa jumla utaonekana kwenye tangazo lako baada ya kupokea tathmini tatu na unaweza kuathiri jinsi unavyoonyeshwa kwenye matokeo ya utafutaji. Fikiria kuratibu ujumbe siku ya kutoka ukiwaomba wageni watathmini ukaaji wao.
Kuwa mkweli na mwenye heshima unapoandika tathmini na utumie viwango sawa kumtathmini kila mgeni. Mchakao wa kutathmini husaidia kujenga uaminifu miongoni mwa wageni na Wenyeji.
Mfululizo wa Mafunzo: Kukaribisha Wageni kwa Mara ya Kwanza
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.