Jinsi utafutaji unavyofanya kazi kwenye Airbnb

Pata vidokezi vya kuboresha nafasi yako katika matokeo ya utafutaji.
Na Airbnb tarehe 11 Mei 2022
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 21 Nov 2022

Vidokezi

  • Bei, ubora na umaarufu wa tangazo lako unaathiri jinsi linavyoonekana katika matokeo ya utafutaji ya wageni wako

  • Jaribu kufungua tarehe zaidi kwenye kalenda yako ili zilingane na vigezo vya utafutaji vya wageni wengi zaidi

Umeunda na kuchapisha tangazo lako na sasa unataka watu waliangalie. Watalipata vipi? Haya ni mambo machache ambayo unaweza kufanya ili kuboresha nafasi yako katika utafutaji.

Elewa mambo ya msingi

Algorithimu ya utafutaji ya Airbnb hutumia vipengele vingi ili kubaini mpangilio wa matangazo yanayoonekana katika matokeo ya utafutaji. Si kila jambo linapimwa kwa usawa. Bei, ubora na umaarufu wa tangazo huathiri sana jinsi tangazo linavyoonekana.

Algorithimu huweka kipaumbele kwa jumla ya bei ya tangazo kabla ya kodi (ikiwemo ada na mapunguzo) na ubora wa tangazo, ikilinganishwa na matangazo yanayofanana nalo katika mahali husika. Picha, tathmini za wageni na sifa nyinginezo za tangazo zinaweza kusaidia kubainisha ubora wake.

Kuweka bei yenye ushindani na kudumisha ubora wa hali ya juu kunaweza kusaidia kuboresha nafasi yako, kwa sababu matangazo yanayotoa thamani bora kwa pesa katika eneo lolote huwekwa kwenye nafasi ya juu katika matokeo ya utafutaji.

Jitahidi kupata umaarufu

Algorithimu ya Airbnb inatathmini umaarufu wa tangazo lako kwa kutumia taarifa mbalimbali. Hii ni pamoja na mara ngapi wageni wanaweka nafasi kwenye tangazo lako, wanatembelea ukurasa wa tangazo lako na kuweka tangazo lako kwenye matamanio yao.

Matangazo maarufu zaidi huwa kwenye nafasi ya juu katika matokeo ya utafutaji. Ili kusaidia kuchochea hamu ya wageni, tunapendekeza kwamba:

  • Utoe vistawishi ambavyo wageni wanataka, kama vile Wi-Fi ya kasi, huduma ya kuingia mwenyewe na maegesho ya bila malipo.
  • Uelezee sifa za kipekee za sehemu yako kwa kuweka maelezo mahususi yanayowajulisha wageni ni nini hasa cha kutarajia.
  • Uangazie picha zenye ubora wa juu zinazoweka mandhari ya kuvutia. Picha zenye ubora wa juu zinaweza kuboresha umaarufu wako ndani ya aina.

Fungua upatikanaji zaidi

Algorithimu ya Airbnb huzingatia upatikanaji wa tangazo lako, nyakati zako za kutoa majibu kwa maulizo na mara ngapi unakubali nafasi zilizowekwa. Kadiri unavyoweka tarehe zilizo wazi kwenye kalenda yako, ndivyo unavyokuwa na uwezekano mkubwa wa tangazo lako kutimiza vigezo vya utafutaji vya mgeni na kuonekana katika matokeo yake ya utafutaji.

Hatua unazoweza kuchukua ili kuboresha nafasi ya tangazo lako kwenye utafutaji:

  • Jibu maombi ya kuweka nafasi ndani ya saa 24. Epuka kukataa maombi ya kuweka nafasi mara kwa mara.
  • Tumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, ili wageni waweze kupata tangazo lako wakati wanachuja matokeo yao ya utafutaji kwa chaguo hilo. Kipengele hiki kinawaruhusu wageni waweke nafasi kwenye eneo lako papo hapo (bila kukuhitaji ukubali maombi yao), hivyo kuharakisha nyakati zako za kutoa majibu.
  • Punguza idadi ya vizuizi, kama vile muda wa chini na wa juu wa kukaa, unaoweka kwenye nafasi zilizowekwa.

Toa ukarimu wa hali ya juu

Uwezo wako wa kuweka matarajio ya wageni katika maelezo ya tangazo lako, kisha uyatimize au uyazidi kama Mwenyeji, kwa kawaida huboresha nafasi yako katika utafutaji baada ya muda.

Kutoa maelezo sahihi kuhusu eneo lako na kuwasiliana kwa uwazi na wageni kunaweza kusababisha upewe ukadiriaji wa juu na tathmini nzuri za ukaaji wao kwako. Inaweza pia kukusaidia uepuke malalamiko ya huduma kwa wateja, ambayo yanaweza kuathiri vibaya nafasi ya tangazo lako.

Algorithimu pia inazingatia iwapo wewe ni Mwenyeji Bingwa, ambalo ni neno tunalotumia kumaanisha Mwenyeji mzoefu aliyepewa ukadiriaji wa juu au ikiwa unatimiza baadhi ya matakwa au matakwa yote ili kuwa Mwenyeji Bingwa. Matakwa hayo yanajumuisha mambo kama vile kujibu haraka maulizo ya wageni ya kuweka nafasi na kupunguza ughairi (wako).

Wageni wana chaguo la kuchuja matokeo yao ya utafutaji ili kufikia matangazo yanayotolewa na Wenyeji Bingwa pekee.

Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu wa kuweka tangazo lenye mafanikio

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Bei, ubora na umaarufu wa tangazo lako unaathiri jinsi linavyoonekana katika matokeo ya utafutaji ya wageni wako

  • Jaribu kufungua tarehe zaidi kwenye kalenda yako ili zilingane na vigezo vya utafutaji vya wageni wengi zaidi

Airbnb
11 Mei 2022
Ilikuwa na manufaa?