Miongozo ya kuandika kichwa cha tangazo lako

Sasisha kichwa chako ili uonyeshe sehemu yako katika matokeo ya utafutaji.
Na Airbnb tarehe 17 Jun 2022
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 23 Okt 2023

Kichwa cha tangazo lako ni mojawapo ya mambo ya kwanza ambayo wageni husoma katika matokeo ya utafutaji na ni fursa ya kuonyesha kile kinachofanya sehemu yako iwe ya kipekee. Fuata miongozo hii ya kuandika kichwa kinachofaa ili kusaidia tangazo lako lionekane zaidi katika utafutaji, kuchochea hamu ya kuweka nafasi kwenye sehemu yako na kuweka matarajio kwa ajili ya wageni.

Vichwa vifupi vinafaa zaidi

Wageni hutafuta Airbnb kwa kutumia aina zote za vifaa vyenye skrini zenye ukubwa tofauti. Kichwa kinachofanya kazi vizuri kwenye kivinjari cha wavuti kinaweza kuwa kirefu sana kwa wageni wanaovinjari matangazo kwenye programu ya simu ya mkononi.

Kutozidi kikomo cha herufi 32 husaidia kuhakikisha kwamba kichwa chako kinaonyeshwa kikamilifu kwenye kompyuta ya mezani na vifaa vya mkononi.

Hii hapa ni mifano mitatu mizuri ya vichwa vifupi vya matangazo:

  • Roshani ya kisasa inayotazama eneo la kibiashara la mji

  • Maficho ya mlimani yenye starehe kwa ajili ya wapishi

  • Vila ya ufukweni karibu na Año Nuevo

Iwapo kichwa chako kinazidi herufi 32, weka taarifa muhimu zaidi kwanza. Vichwa virefu vinafupishwa kiotomatiki katika matokeo ya utafutaji na nukta endelezi zinachukua nafasi ya sehemu iliyosalia ya kichwa chako. Kwa mfano, kichwa kama vile "Nyumba ya mbao ya mashambani iliyo na mwonekano wa ziwa, meko, kijia chenye mteremko cha boti" kinakuwa "Nyumba ya mbao ya mashambani iliyo na mwonekano wa ziwa..." katika matokeo ya utafutaji.

Chagua mtindo wa sentensi

Mtindo wa sentensi unahitaji herufi ya kwanza ya neno la kwanza pekee iwe kubwa katika kichwa chako. Inaweza kuwa rahisi kusoma na kuzungumza zaidi kuliko mtindo wa kichwa cha habari, ambapo maneno mengi yanaanza kwa herufi kubwa au HERUFI KUBWA ZOTE.

Ili kuwapa wageni huduma nzuri ya utafutaji, epuka kutumia herufi kubwa kwenye maneno mengine ya kichwa chako isipokuwa liwe ni jina rasmi kama vile jiji. Unaweza pia kutoa vighairi kwa ajili ya vifupisho, kama vile Uingereza (UK) au msimbo wa uwanja wa ndege kama vile LHR.

Hii hapa ni mifano mitatu mizuri ya vichwa vya matangazo katika mtindo wa sentensi:

  • Kibanda cha ufukweni huko Bondi Beach

  • Chumba cha wageni cha kimahaba cha Victorian

  • Studio inayotunza mazingira karibu na LAX

Maneno ni dhahiri zaidi kuliko emoji

Emoji na alama zinaweza kukanganya au kupotosha kwa sababu zinamaanisha vitu tofauti kwa watu tofauti ulimwenguni. Kwa mfano, kidole gumba juu kinaweza kufasiriwa kama ishara ya idhini, nambari moja au ishara ya kuchukiza.

Ili ufanye kichwa cha tangazo lako kiwe cha kuvutia na rahisi kusoma, tumia maneno rahisi na yenye maelezo kuhusu eneo lako. Kutumia vibambo maalumu (kama vile !, # au *) ni sawa, lakini kuvirudia kwa ajili ya msisitizo (kama vile !!! au ***) si sawa. Ili utenganishe mawazo, jaribu kutumia alama za mkato pamoja na nafasi au mkwaju mmoja bila nafasi.

Huu hapa ni mfano wa jambo la kutofanya:

  • ****Ski na Chalet ya gofu ****!!!

Hapa kuna njia bora ya kuandika hii:

  • Fleti ya kuteleza thelujini/gofu yenye uga wa kujitegemea

Maelezo zaidi ni bora kuliko kurudiarudia

Katika visa vingi, si lazima urudie taarifa yoyote ambayo tayari imetolewa kwa wageni katika matokeo ya utafutaji, kama vile jiji au mji wako au idadi ya jumla ya vitanda. Badala yake, tumia kichwa cha tangazo lako kuongeza maelezo ya kipekee ambayo yanaweza kusaidia kuwavutia watu.

Kwa mfano, ikiwa tangazo lako liko Buenos Aires, unaweza kujumuisha kitongoji chako, kama vile “Recoleta,” katika kichwa cha tangazo lako. Ikiwa liko Florence, Italia, unaweza kutaja "karibu na Uffizi" au alama-ardhi nyingine ambayo iko karibu na eneo lako. Au, ikiwa una sehemu mahususi ya ofisi, huenda ukataka kuonyesha "inayofaa kwa kazi" kwenye kichwa. Hii husaidia kufafanua maelezo muhimu kwa wageni.

Unaweza pia kuondoa neno "mpya" kwenye kichwa cha tangazo jipya, kwa sababu taarifa hii tayari imewasilishwa kwa wageni kwenye beji katika matokeo ya utafutaji.

Soma Sera ya Maudhui ya Airbnb

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
17 Jun 2022
Ilikuwa na manufaa?