Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Majibu kwa wasafiri kuhusu COVID-19

  Pata maelezo ya jinsi tunavyokusaidia upate machaguo ya usafiri unaoweza kubadilika, sehemu za kukaa safi zaidi na kadhalika.
  Na Airbnb tarehe 10 Mac 2020
  Inachukua dakika 6 kusoma
  Imesasishwa tarehe 25 Jun 2021

  Tunajua bado kuna hali kubwa ya kutokuwa na uhakika kuhusu COVID-19 na iwapo itaathiri mipango yako ya likizo kadiri safari zinaporejea katika miezi ijayo. Ili kuwasaidia wasafiri, tunafuatilia maswali yako na kujibu baadhi yake hapa. Tutaendelea kufanya mabadiliko kwenye ukurasa huu kadiri hali inavyobadilika na kadiri majibu zaidi yanavyopatikana.

  Ninahitaji kughairi safari yangu. Machaguo yangu ni yapi?
  Sera za kughairi zinawekwa na Wenyeji na zinaweza kutofautiana. Unaweza kupata maelezo kuhusu sera ya kughairi ya kila sehemu ya kukaa kwenye ukurasa mkuu wa kila tangazo au kwenye sehemu ya Safari ya tovuti au programu ya Airbnb kwa nafasi ulizoweka zilizopo.

  Wageni ambao waliweka nafasi mpya baada ya tarehe 14 Machi, 2020 hawatarejeshewa fedha chini ya sera ya sababu zisizozuilika ikiwa wataghairi kwa sababu ya COVID-19 isipokuwa kama wanaumwa COVID-19. Pata maelezo zaidi kuhusu sera yetu ya sababu zisizozuilika.

   Ninataka kuweka nafasi ya safari, lakini sina uhakika kuhusu jinsi hali ya COVID-19 au vikwazo vya kusafiri vya kimatiafa vitakavyobadilika. Nifanye nini?
   Inaeleweka, unaweza kuhisi kutokuwa na uhakika kuhusu kuweka nafasi ya safari siku zijazo sasa hivi. Tunawahimiza sana wageni wote wazingatie kwa makini sera ya kughairi kwa nafasi yoyote wanayoiweka na kuchagua matangazo ambayo yanaruhusu uwezekano wa kubadilika. Tumeweka kichujio ili iwe rahisi kwako kutafuta maeneo yenye sera za kughairi zinazoweza kubadilika. Pia tumeunda nyenzo hii ili kuwasaidia wasafiri wapate maelezo zaidi kuhusu machaguo ya bima ya safari ya wahusika wengine. Wageni ambao wanaweka nafasi mpya baada ya tarehe 14 Machi, 2020 hawatarejeshewa fedha chini ya sera ya sababu zisizozuilika ikiwa wataghairi kwa sababu ya COVID-19 isipokuwa kama wanaumwa COVID-19.

   Ninawezaje kupata sehemu ya kukaa yenye sera ya kughairi inayoweza kubadilika?
   Tumeweka kichujio ili iwe rahisi kwako kutafuta maeneo yenye sera za kughairi zinazoweza kubadilika. Pata maelezo zaidi kuhusu kichujio hicho. Kumbuka kuwa sera za kughairi zimewekwa na Wenyeji na zinaweza kutofautiana. Unaweza kupata maelezo kuhusu sera ya kughairi ya kila sehemu ya kukaa kwenye ukurasa mkuu wa kila tangazo.

   Nitapata wapi maelezo zaidi kuhusu vizuizi vya kusafiri na ushauri?
   Jumuiya nyingi zimetoa ushauri wa kusafiri wa eneo husika au vizuizi vya muda kwenye nyumba za kupangisha kwa muda (ikiwa ni pamoja na sehemu za kupangisha kwa muda mfupi). Tunapendekeza uangalie vizuizi vya kusafiri na ushauri wa eneo husika ili kujua ikiwa ukaaji wako unaweza kuathiriwa.

   Nimeshindwa kurejeshewa fedha kulingana na sera yangu ya kughairi ya Mwenyeji. Kwa nini?
   Airbnb ni jumuiya ya wageni na Wenyeji wanaounganishwa kupitia tovuti ya Airbnb. Wenyeji wanaamua kiasi wanachotoza, sheria mahususi kuhusu sehemu hiyo na sera zao za kughairi. Unaweza kupata maelezo kuhusu sera ya kughairi ya kila sehemu ya kukaa kwenye ukurasa mkuu wa kila tangazo au kwenye sehemu ya Safari ya tovuti au programu ya Airbnb kwa ajili ya nafasi ulizoweka zilizopo. Katika visa vingi, Wenyeji wanategemea mapato ya Airbnb kuendesha maisha yao, jambo ambalo linaweza kuwa gumu kwao kuweka vighairi kwenye sera zao.

   Mwenyeji amenighairia. Sasa itakuwaje?
   Tunajua kughairi kunaweza kufadhaisha na hata wakati ambapo kunafanyika kwa sababu inayoeleweka. Kumbuka kwamba Wenyeji wengi ambao wanaghairi sehemu iliyowekewa nafasi wanaweza kuwa wameathiriwa na COVID-19 au wanatenda kwa namna ya kusaidia kulinda ustawi wa jumuiya yote.

   Ikiwa Mwenyeji wako ataghairi, unaweza kustahiki kurejeshewa fedha zote. Angalia sehemu ya Safari ya tovuti au programu ya Airbnb kwa maelezo kuhusu fedha zako zinazorejeshwa.

   Ikiwa bado unahitaji kusafiri, tunatazamia kwamba utachagua kuweka tena nafasi kwenye Airbnb.

   Ni aina gani ya itifaki za kiafya, usalama na kufanya usafi ambazo zinatumika kwa wageni na Wenyeji wakati wa ukaaji?
   Usalama wa jumuiya yetu ni kipaumbele chetu cha kwanza, kwa hivyo tumeunda mazoea ya lazima ya usalama dhidi ya COVID-19 kwa Wenyeji na wageni wa matangazo ya Airbnb, kwa kuzingatia mwongozo kutoka kwa wataalamu kama vileShirika la Afya Duniani na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Ugonjwa vya Marekani. Wenyeji ulimwenguni kote wanajizatiti kufuata mazoea yetu yaliyofanyiwa mabadiliko ya usalama na kufanya usafi ya COVID-19 ili kukusaidia kukupa utulivu wa akili. Pata maelezo zaidi hapa.

   Hivi karibuni, tumeacha matakwa ya jumla ya kimataifa kwa ajili ya kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko. Badala yake, tunaanza kuwaomba Wenyeji na wageni wafuate sheria na miongozo ya eneo husika kwa kuwa Airbnb ina matangazo duniani kote na jumuiya mbalimbali zipo katika hatua tofauti za jitihada zao za kuidhibiti COVID-19. Tunapendekeza uangalie miongozo ya jumla ya afya na usalama kwa ajili ya usalama wa COVID-19, ufuatilie vizuizi husika vya kusafiri vya serikali na ushauri wa kusafiri na ufuate miongozo yote ya kitaifa na eneo husika unaposafiri.

   Ninataka kuweka nafasi ya Tukio la Airbnb la ana kwa ana. Ninahitaji kujua nini?
   Tumefungua tena matukio ya ana kwa ana katika maeneo ambapo inaruhusiwa kufanya hivyo na tumeanzisha miongozo ya afya na usalama ambayo inawataka Wenyeji na wageni wavae zana za ulinzi za kufunika uso na kuepuka mikusanyiko pale wanapotakiwa na sheria au miongozo ya eneo husika. Kadiri vizuizi vya serikali vinavyobadilika, tunaweza kusitisha matukio katika eneo fulani baada ya eneo hili kufunguliwa tena na tutakujulisha ikiwa hiyo itatokea. Endapo umeweka nafasi ya tukio la ana kwa ana katika eneo ambalo limesitishwa, utapokea kuponi ya USD25 ili ushiriki kwenye tukio la wakati ujao.Pata maelezo kuhusu kufunguliwa tena

   Ikiwa ungependa kufanya tukio la ana kwa ana ukiwa na kundi lako pekee, fikiria kuweka nafasi ya kundi binafsi. Ikiwa matukio ya ana kwa ana bado hayajafunguliwa kwenye jumuiya yako, angalia matukio yetu ya mtandaoni. Iwe unataka kujifunza ujuzi mpya, kuhusiana na marafiki kwenye shughuli ya kufurahisha au kujaribu zoezi la kujenga timu pamoja na wafanyakazi wenzako, sasa unaweza kufanya hivyo kwa usalama ukiwa nyumbani kwako. Kuanzia kujifunza siri za mazingaombwe hadi kupika pamoja na familia ya Kimoroko hadi kutaamali pamoja na mtawa wa Kibudha, tayari kuna matukio mengi ya mtandaoni ya kuyachunguza.

   Je, wageni wanapaswa kufuata mazoea ya usalama ya Airbnb kuhusu COVID-19?
   Wakati janga la ugonjwa linaendelea, ni muhimu kwamba sisi sote tutimize sehemu yetu katika kusaidia kuzuia COVID-19 isienee. Kwa kuzingatia hili, tulizindua mazoea ya usalama ya lazima ambayo kila mtu katika jumuiya ya Airbnb anapaswa kufuata, kulingana na mwongozo kutoka kwa wataalamu wa afya kama vile Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Ugonjwa vya Marekani. Kama sehemu ya mazoea ya usalama, wageni na Wenyeji wanapaswa kukubali, wanapotakiwa na sheria na miongozo ya eneo husika, kuvaa barakoa au kitambaa cha kufunika uso wakati wa kuingiliana na mtu na kuepuka mikusanyiko.

   Niliweka nafasi ya sehemu ya kukaa kwenye Airbnb kwa ajili ya hafla ambayo imeghairiwa. Je, ninaweza kughairi nafasi yangu niliyoiweka?
   Tunajua kwamba wasafiri wetu wengi wanaweka sehemu za kukaa kwenye Airbnb kwa ajili ya hafla. Ikiwa hafla uliyokuwa unapanga kuhudhuria imeghairiwa na nafasi uliyoweka hailindwi na sera yetu ya sababu zisizozuilika, tafadhali angalia sera ya kughairi kwenye nafasi uliyoweka. Pia, jisikie huru kuwasiliana na Mwenyeji wako moja kwa moja.

   Sera ya sababu zisizozuilika ni nini?
   Sera ya Airbnb ya sababu zisizozuilika inawapa wageni na Wenyeji chaguo la kughairi bila kutozwa fedha ikiwa wameathiriwa na mambo kama vile majeraha au ugonjwa mkubwa, majanga ya asili, vizuizi vya kusafiri na matukio mengine yasiyotarajiwa. Wageni ambao wanaweka nafasi mpya baada ya tarehe 14 Machi, 2020 hawatarejeshewa fedha chini ya sera ya sababu zisizozuilika ikiwa wataghairi kwa sababu ya COVID-19 isipokuwa kama wanaumwa COVID-19. Kuchunguza machaguo ya kughairi yaliyopo kwa ajili ya sehemu yako uliyoiwekea nafasi, tafadhali tembelea sehemu ya Safari ya tovuti au programu ya Airbnb.

   Niliweka nafasi kwenye nyumba ya Airbnb Luxe. Je, ninalindwa na sera ya sababu zisizozuilika?
   Sera yetu ya sababu zisizozuilika haihusu nafasi zilizowekwa za Airbnb Luxe, ambazo zinadhibitiwa na sera tofauti ya kurejesha fedha ya wageni wa Luxe.

   Je, kuna nyenzo za ziada za kunisaidia kupata taarifa wakati ninasafiri?
   Kwa taarifa za hivi karibuni kuhusu vizuizi na miongozo ya safari, angalianyenzo hii.

   Ili kusaidia kupunguza kasi ya kuenea COVID-19, unaweza kupakua programu za Arifa za Mazingira ya Maambukizi kwenye simu yako. Programu hizi za wahusika wengine, zilizotengenezwa na mamlaka ya afya ya umma duniani kote kulingana na teknolojia ya Google na Apple, zinakutaarifu ikiwa utakutana na mtu ambaye alipimwa na kugundulika kuwa ana COVID-19. Pata maelezo zaidi kuhusu Arifa za Mazingira ya Maambukizi, mazoea yake ya faragha na jinsi ya kupata arifa.

   Bado nina maswali. Ninapaswa kuwasiliana na nani?
   Kwa sababu ya athari zilizoenea za COVID-19 katika usafiri duniani kote, timu yetu ya usaidizi wa jumuiya bado inapokea simu na ujumbe mwingi kuliko kawaida. Ikiwa hali yako inahitaji usaidizi wa haraka kutoka kwa mwanatimu wa timu ya usaidizi wa jumuiya, siku zote unaweza kuwasiliana nasi moja kwa moja kupitia programu hiyo..

   Pia unaweza kupata majibu kwa maswali yako mengi katika baadhi ya nyenzo za kujihudumia ambazo tumezitengeneza ili kufanya iwe rahisi kwako kutatua matatizo wewe mwenyewe. Tafadhali tembelea nyenzo hii kwa ajili ya vikwazo vya kusafiri vya hivi karibuni au Kituo cha Msaada kwa ajili ya nyenzo na taarifa zaidi.

   Tunajua jinsi ambavyo COVID-19 imewasumbua wasafiri na tuko hapa kukusaidia. Asante kwa kufanya kazi pamoja nasi ili kusaidia kulinda usalama na ustawi wa jumuiya yetu.

   Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

   Airbnb
   10 Mac 2020
   Ilikuwa na manufaa?