Jua zaidi kuhusu wageni wako kupitia maboresho ya wasifu

Mpangilio mpya wa wasifu unajumuisha upigaji picha wa kuelekezwa ili kupata picha bora.
Na Airbnb tarehe 1 Mei 2024
Inachukua dakika 1 kusoma
Imesasishwa tarehe 21 Okt 2024

Maelezo ya mhariri: Makala haya yalichapishwa kama sehemu ya Toleo la Mei 2024. Taarifa zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Soma kuhusu toleo letu la hivi karibuni la huduma

Umetuambia kwamba ni muhimu kujua zaidi kuhusu mtu unayemkaribisha. Sasa, wageni wanaoweka nafasi au wanaojiunga na safari watakumbushwa kuunda wasifu kamili zaidi.

Wasifu wa wageni ulioboreshwa unafanyaje kazi?

Kupitia mpangilio wetu mpya wa wasifu, tunafanya iwe rahisi na kufurahisha kwa wageni kujaza wasifu wao. Hii inajumuisha upigaji picha wa kuelekezwa unaowasaidia wageni kuweka picha ya wasifu inayoonyesha dhahiri uso wao, bila watu kuwepo wengine kwenye picha hiyo.

Sawa na wasifu wa mwenyeji, wageni wanaweza kujumuisha maelezo kama vile mahali wanapoishi, lugha wanazozungumza na ukweli mwingine kujihusu, ili uweze kufahamu vizuri ni nani anayekuja kukaa. Wageni wote wanaoweka nafasi bado wanatakiwa kuthibitisha utambulisho wao. 

Wageni wanaweza pia kuweka mihuri ya safari, wakionyesha maeneo yote ambayo wamekuwa kwenye Airbnb. Hii inaonyesha historia ya kusafiri ya wageni iliyo na mihuri ya picha, kama ile unayoipata kwenye pasipoti.

Kama kawaida, utaweza kufikia wasifu wa wageni kwa kufungua nafasi iliyowekwa.

Katika mpangilio mpya wa wasifu, upigaji picha wa kuelekezwa unavuta uso wa mgeni ili kupata picha nzuri.

Wasaidie wageni kukujua kwa kukamilisha wasifu wako wa mwenyeji.

Airbnb
1 Mei 2024
Ilikuwa na manufaa?