Udhibiti zaidi katika kichupo cha Matangazo
Maelezo ya mhariri: Makala haya yalichapishwa kama sehemu ya Toleo la Mei 2024. Taarifa zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Soma kuhusu toleo letu la hivi karibuni la huduma
Tumeona kwamba matangazo yenye maelezo zaidi yanaweza kuwekewa nafasi zaidi kwa hadi asilimia 20. Tangu kuzindua kichupo cha Matangazo mwaka 2023, tumeendelea kukiboresha kulingana na maoni ya Mwenyeji.
Toleo la Mei 2024 linajumuisha ombi lako kuu la ziara ya picha: uwezo wa kupanga upya picha za tangazo ndani ya vyumba. Hivi karibuni, utaweza pia kusasisha ziara ya picha iliyopo kwa kusaidiwa na akili bandia (AI).
Hapa kuna njia tano za kusimamia tangazo lako kwa urahisi zaidi kwa kutumia kichupo cha Matangazo, kwa kuanza na ziara ya picha iliyoboreshwa.
1. Unda ziara ya picha
Wasaidie wageni waelewe mpangilio wa nyumba yako kwa kuunda ziara ya picha. Unaweza kutumia AI kupanga picha za tangazo lako kiotomatiki katika vyumba na sehemu za wazi, kisha uhariri ziara mwenyewe.
Sasa, unaweza kuburuta na kuweka picha ili kuzipanga upya ndani ya chumba chochote. Hivi karibuni, utaweza kusasisha ziara papo hapo unapoweka picha tatu au zaidi. AI itapanga picha mpya bila kubadilisha mabadiliko yoyote uliyofanya.
2. Badilisha vistawishi vyako
Wageni mara nyingi huchuja matokeo yao ya utafutaji kwenye Airbnb ili kupata nyumba zilizo na vipengele au vistawishi fulani. Saidia tangazo lako lionekane zaidi kwa kujumuisha kila kitu ambacho nyumba yako onatoa. Kichupo cha Matangazo hufanya iwe rahisi kuweka vistawishi na kuendelea kuvisasisha.
Unaweza kuona vistawishi karibu 150 kwa utaratibu wa alfabeti au kulingana na aina au utafute kistawishi kulingana na jina, huhitajiki kutelezesha. Jumuisha maelezo unapokuwa umeombwa, kama vile kubaini kwamba sehemu yako mahususi ya kufanyia kazi ina printa na kiti cha kufanyia kazi.
3. Weka upya maelezo ya tangazo lako
Wageni wanataka maeneo wanayoweka nafasi yalingane na maelezo ya tangazo. Kutoa taarifa iliyo wazi na sahihi kuhusu nyumba yako na mazingira yake husaidia kuweka matarajio.
Elezea mahali, mapambo na ukarimu wako. Jitahidi kuwajulisha wageni jinsi ilivyo kukaa kwenye sehemu yako, mandhari, sauti na uzoefu
4. Kamilisha mwongozo wako wa kuwasili
Wageni wanapaswa kuwa na uwezo wa kupata sehemu yako na kuingia ndani kwa urahisi. Kichupo cha Matangazo kinakuwezesha kuweka au kusasisha taarifa zote za kuwasili katika sehemu moja.
Unaweza kusimamia njia yako ya kuingia na muda, maelekezo na vidokezi vya maegesho, nenosiri la Wi-Fi, mwongozo wa nyumba, maelekezo ya kutoka na kadhalika kisha uhakiki kile ambacho wageni wataona. Wageni wanapokea taarifa baada ya kuweka nafasi, kabla ya kuingia na kabla ya kutoka.
5. Weka kufuli janja
Kufuli janja ni kufuli la kielektroniki linalowezeshwa na Wi-Fi ambalo wageni hufungua mlango kwa msimbo badala ya ufunguo. Inaweza kuwa njia rahisi na yenye ufanisi ya kuingia mwenyewe.
Unaweza kufanya mchakato wa kuingia mwenyewe uwe shwari kwa kuunganisha kufuli janja linalopatana kwenye tangazo lako. Wageni hupokea msimbo wa kipekee wa mlango kiotomatiki kwa ajili ya nafasi mpya zinazowekwa na unaweza kudhibiti kufuli lako kutoka kwenye programu ya Airbnb.
Nyenzo hii inapatikana kwa Wenyeji walio na matangazo nchini Marekani na Kanada ambao hutumia makufuli yanayopatana kutoka kampuni za August, Schlage na Yale.