Pata vidokezi muhimu kwenye dashibodi ya mapato
Kuelewa mapato yako kunaweza kukusaidia uendeshe biashara ya kukaribisha wageni yenye mafanikio zaidi. Hivi ndivyo unavyoweza kutumia vipengele vilivyo kwenye dashibodi ya mapato.
Chati tendanishi ya mapato
Chati ya mapato iliyo kwenye sehemu ya juu ya dashibodi inaonyesha:
- Kiasi ulichopata katika kila mwezi mmoja katika miezi sita iliyopita
- Kiasi ambacho umepata kufikia sasa mwezi huu
- Kiasi unachokadiriwa kupata katika kila mmoja wa miezi mitano ijayo kulingana na nafasi zilizowekwa zinazokaribia
Panua chati ili uone mapato yako kulingana na mwezi au mwaka na utumie kichujio ili uone kulingana na tangazo.
Chini ya chati tendanishi ya mapato, takwimu za utendaji zinaonyesha jumla ya usiku uliowekewa nafasi na wastani wa muda wa kukaa.
Muhtasari wa mapato unaangazia mapato yako yote, makato na jumla ya malipo halisi tangu tarehe 1 Januari ya mwaka wa sasa.
Kadi za mapato
Kadi ya mapato inaonekana kwenye dashibodi ya mapato wakati malipo yapo njiani. Inaonyesha:
- Njia ya kupokea malipo
- Kiasi cha muamala
- Kadirio la muda wa kuchakata
Fungua muamala ili uone maelezo zaidi.
Chuja kulingana na aina ya mapato
Chuja mapato yako kulingana na aina unapotathmini miamala inayokaribia au iliyolipwa. Aina hizo zinajumuisha:
- Nyumba
- Matukio
- Huduma
- Masalio
- Masuluhisho
Unaweza pia kuchuja miamala kulingana na tarehe, tangazo na njia ya kupokea malipo.
Ripoti za mapato
Airbnb inakutolea taarifa za kila mwezi na za kila mwaka kuanzia mwezi ulipoanza kukaribisha wageni. Unaweza kupakua ripoti yoyote au kutuma nakala ya PDF kupitia barua pepe kwa ajili ya kumbukumbu zako.
Unaweza pia kuunda ripoti mahususi kwa tangazo na tarehe zozote unazochagua. Kila ripoti hutoa mchanganuo wa mapato yako yote, makato na jumla ya malipo halisi.
Una chaguo la kujumuisha:
- Njia za kupokea malipo zinazoonyesha jumla ya mapato kwa kila akaunti ya kupokea malipo
- Takwimu za utendaji zinazoonyesha usiku uliowekewa nafasi na wastani wa muda wa kukaa
Mara baada ya kuchagua kitu cha kujumuisha, unaweza kupakua au kutuma PDF ya ripoti kupitia barua pepe kwa ajili ya kumbukumbu zako.
Settings and documents
Ikoni ya gia iliyo upande wa juu kulia mwa dashibodi ya mapato inakuruhusu ufikie:
- Njia za kupokea malipo na kanuni za anwani ya kutuma malipo
- Maelezo ya mlipa kodi na hati za kodi
- Ripoti za mapato kwa tangazo na tarehe zozote
- Michango ya mara kwa mara ya Airbnb.org kama asilimia ya kila malipo yanayotumwa ili kuwasaidia watu wakati wa shida
User experience may vary by location.
Information contained in this article may have changed since publication.