Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Jiunge na Mtandao wa Wenyeji Wenza

Jipatie pesa ukitumia ujuzi ambao umeukuza kwa kukaribisha wageni.
Na Airbnb tarehe 16 Okt 2024
Imesasishwa tarehe 5 Jun 2025

Sasa unaweza kutoa usaidizi mahususi kwa wenyeji walio na matangazo katika eneo lako kupitia Mtandao wa Wenyeji Wenza. Kujiunga na mtandao ni njia nzuri ya:

  • Kujitangaza mwenyewe na huduma zako.
  • Kushiriki kile unachotoza.
  • Kuungana na washirika watarajiwa.
  • Kufanya kazi kwa kujitegemea kwa ratiba zako mwenyewe.

Mtu yeyote anayetafuta mwenyeji mwenza anaweza kutafuta mtandao ili kupata na kuajiri mshirika bora, mkazi. 

Mtandao wa Wenyeji Wenza unapatikana nchini Australia, Brazili, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Meksiko, Puerto Rico, Korea Kusini, Uhispania, Uingereza na Marekani.

Huduma unazoweza kutoa

Wasifu wako wa mwenyeji mwenza ni mahali ambapo unatangaza ujuzi wako na kuweka maelezo kuhusu huduma unazotoa. Chagua kutoka kwenye orodha ya huduma za kushirikiana kukaribisha wageni:

  • Kuandaa tangazo
  • Kuweka bei na upatikanaji
  • Usimamizi wa maombi ya kuweka nafasi
  • Ujumbe wa mgeni
  • Usaidizi wa mgeni kwenye eneo
  • Kufanya usafi na matengenezo
  • Upigaji picha wa nyumba
  • Usanifu wa ndani na mitindo
  • Vibali vya leseni na kukaribisha wageni

Unaweza pia kuelezea huduma zozote za ziada unazotoa, kama vile huduma ya kuboresha mandhari, uchambuzi wa biashara na mafunzo ya ukarimu.

Wenyeji wanaotafuta usaidizi katika eneo lako wanaweza kuuliza maswali na kuomba huduma zako. Algorithimu ya utafutaji wa mtandao huzingatia mambo mengi, ikijumuisha ubora, ushiriki na mahali, ili kuwasaidia wenyeji kupata wenyeji wenza wanaofaa matangazo yao.

Kinachohitajika ili kujiunga

Matakwa ya kujiunga na Mtandao wa Wenyeji Wenza ni:

  • Una tangazo amilifu kama mwenyeji au kama mwenyeji mwenza mwenye ufikiaji kamili au ufikiaji wa kalenda na ujumbe.
  • Umekaribisha wageni au umeshirikiana kukaribisha wageni kwenye sehemu 10 au zaidi za kukaa au sehemu tatu au zaidi za kukaa kwa jumla ya angalau usiku 100 kwenye Airbnb katika miezi 12 iliyopita.
  • Umedumisha ukadiriaji wa wastani wa nyota 4.8 au zaidi kutoka kwa wageni katika miezi 12 iliyopita kwa matangazo yote unayokaribisha wageni au unayoshirikiana kukaribisha wageni ukiwa na ufikiaji kamili au ufikiaji wa kalenda na ujumbe.
  • Una kiwango cha kughairi cha chini ya asilimia 3, isipokuwa kwa sababu fulani halali usizoweza kudhibiti.
  • Akaunti yako ya Airbnb iko katika hali nzuri. Utambulisho wako lazima uthibitishwe na lazima ukidhi matakwa ya jina na picha ili kuonyeshwa kwenye mtandao.

Ni wajibu wako kujua kanuni za eneo husika zinazokuhusu na kuwa na leseni, vibali na usajili wote unaohitajika. Kwa mfano, baadhi ya maeneo yanaweza kuhitaji leseni za madalali wa mali isiyohamishika kulingana na huduma zako.

Soma masharti ya huduma ya Mtandao wa Wenyeji Wenza na upate maelezo kuhusu algorithimu ya utafutaji, uthibitishaji wa utambulisho na sababu halali za kughairi kwenye Kituo cha Msaada.

Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa sasa unapatikana nchini Australia, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Meksiko, Puerto Rico, Korea Kusini, Uhispania na Uingereza (unaendeshwa na Airbnb Global Services); Kanada, Marekani (unaendeshwa na Airbnb Living LLC); na Brazili (unaendeshwa na Airbnb Plataforma Digital Ltda).

Wenyeji kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa kawaida wana ukadiriaji wa juu, viwango vya chini vya kughairi na uzoefu thabiti wa kukaribisha wageni kwenye Airbnb. Ukadiriaji unategemea tathmini za wageni kwa matangazo wanayokaribisha wageni au kushirikiana kukaribisha wageni na huenda usiwakilishe huduma za kipekee za mwenyeji mwenza.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
16 Okt 2024
Ilikuwa na manufaa?