Chunguza dashibodi ya mwenyeji mwenza
Dashibodi yako ni muhimu kwa mafanikio yako kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza. Hapo ndipo unapoungana na wenyeji na kufuatilia maendeleo kuelekea malengo yako.
Kuelewa takwimu zako
Utapata takwimu hizi kwenye kichupo cha maombi cha dashibodi yako.
- Ukadiriaji wa wastani: Lazima udumishe ukadiriaji wa 4.7 au zaidi ili uendelee kuonekana katika matokeo ya utafutaji. Ukadiriaji wako ni ukadiriaji wa wastani wa nyota kutoka kwa wageni katika miezi 12 iliyopita kwa matangazo yote unayosaidia, isipokuwa yale unayoshirikiana kukaribisha wageni ukiwa na ufikiaji wa kalenda pekee.
- Kiwango cha kutoa majibu: Huenda wasifu wako wa mwenyeji mwenza usibaki ukionekana katika matokeo ya utafutaji ikiwa kiwango chako cha kutoa majibu kitashuka chini ya asilimia 90. Kiwango chako cha kutoa majibu ni asilimia ya maombi mapya kutoka kwa wenyeji ambayo umejibu ndani ya saa 24. Kinahesabiwa kwa kipindi cha siku 90 zilizopita.
- Wageni waliotazama: Hii ni idadi ya wageni wa kipekee waliotembelea wasifu wako wa mwenyeji mwenza katika siku 90 zilizopita.
- Wageni walioshawishika: Hii ni asilimia ya wenyeji ambao waliwasiliana nawe kati ya wale ambao waliona wasifu wako katika matokeo ya utafutaji katika siku 90 zilizopita.
Kuwajibu wenyeji
Maombi kutoka kwa wenyeji yanaonekana kwenye kichupo chako cha maombi na kwenye kichupo chako cha Ujumbe. Washa arifa ili usikose ombi na uweze kujibu haraka.
Katika maombi yako, unaweza kufikia:
- Jina la mwenyeji
- Anwani ya tangazo la mwenyeji
- Taarifa za mawasiliano za mwenyeji
- Tarehe ya ombi
- Hali ya ombi
Ikiwa tayari unashirikiana kukaribisha wageni, fikiria kuwaalika washirika watarajiwa. Unaweza kushiriki mialiko kwenye ujumbe au utumie njia ambayo mwenyeji anapendelea.
Jimmy, mwenyeji mwenza huko Combs-la-Ville, Ufaransa, anasema mialiko huongeza sana uwezekano wake wa kuwa na ushirikiano wenye mafanikio. "Kwa mwenyeji, hakuna jambo zuri kama kuhakikishiwa na mmoja wa wateja wetu waliopo," anasema.
Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa sasa unapatikana nchini Australia, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Meksiko, Puerto Rico, Korea Kusini, Uhispania na Uingereza (unaendeshwa na Airbnb Global Services); Kanada, Marekani (unaendeshwa na Airbnb Living LLC); na Brazili (unaendeshwa na Airbnb Plataforma Digital Ltda).
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.