Kunufaika zaidi na kichupo cha Ujumbe
Kichupo cha Ujumbe ni kikasha chako cha Airbnb. Inaweka ujumbe wako wote wa kukaribisha wageni, kusafiri na usaidizi katika sehemu moja. Vipengele katika kichupo cha Ujumbe vinakuruhusu:
- Kuchuja ujumbe na kutafuta kwenye kikasha chako.
- Kutuma na kuratibu ujumbe, ikiwemo violezo vilivyoandikwa mapema vinavyoitwa majibu ya haraka.
- Kuwasiliana na kila mgeni kwenye nafasi iliyowekwa katika mazungumzo mamoja.
- Kuanza majibu kwenye mfumo wa uzi ili kupanga mazungumzo.
- Kuhariri na kubatilisha kutuma ujumbe uliotumwa.
- Tumia uthibitisho wa kusoma ujumbe ili uone wageni wanapoangalia ujumbe wako.
- Kuitikia ujumbe kwa kutumia emoji.
Kuchuja na kutafuta ujumbe
Mwonekano chaguomsingi unaonyesha ujumbe wako wote kwenye Airbnb. Chagua Kukaribisha wageni, Kusafiri au Usaidizi ili kuchuja ujumbe kulingana na aina.
Ndani ya Kukaribisha wageni, unaweza kutumia vichujio hivi vya ziada:
- Ujumbe ambao haujasomwa huonyesha tu ujumbe ambao haujafunguliwa.
- Hatua ya safari hupanga ujumbe kulingana na maombi ya kuweka nafasi, nafasi zilizowekwa zinazokaribia, kukaribisha wageni kwa sasa au nafasi zilizowekwa hapo awali.
- Matangazo hupanga ujumbe kulingana na tangazo ikiwa una zaidi ya moja.
- Wenye nyota huonyesha tu ujumbe ambao umeweka alama ya nyota.
Ikiwa una mwenyeji mwenza, wewe ni Balozi Mwenyeji Bingwa au unakaribisha wageni kwenye Tukio la Airbnb, utapata vichujio hivi kwenye kichupo cha Ujumbe:
- Mwenyeji Mwenza huonyesha mazungumzo kati yako na wenyeji wenza wowote kwenye tangazo.
- Balozi Mwenyeji Bingwa huonyesha ujumbe kati yako na wenyeji uliounganishwa nao.
- Matukio hukuruhusu kusoma ujumbe unaohusiana na nafasi hizo zilizowekwa.
Tumia kichujio cha Kusafiri ili kuona ujumbe unaotuma na kupokea kama mgeni. Tumia kichujio cha Usaidizi ili kuona mazungumzo yako na Airbnb Usaidizi.
Unatafuta mazungumzo mahususi? Unaweza kutafuta ujumbe kulingana na majina, maneno au mafungu ya maneno. Matokeo yanazingatia vichujio vyovyote ambavyo umetumia na kukusaidia kupata mazungumzo haraka.
Kutuma na kuratibu majibu ya haraka
Mawasiliano ya wazi, ya wakati unaofaa ni sehemu muhimu ya kukaribisha wageni kwa mafanikio. Anza mazungumzo, toa taarifa na ujibu maswali kutoka kwa wageni katika kichupo cha Ujumbe.
Ili kuokoa muda, jaribu kutumia kipengele cha majibu ya haraka. Majibu ya haraka ni violezo vya ujumbe wa kushiriki taarifa za kawaida, kwa hivyo si lazima uanze kutoka mwanzo. Utapata ujumbe mchache ulioandikwa mapema katika kichupo cha Ujumbe ili kuwasaidia wageni wakati muhimu, kama vile mara baada ya kuweka nafasi. Unaweza kutumia majibu haya ya haraka kama yalivyo, kuyahariri au kuunda violezo vyako mahususi.
Kichupo cha Ujumbe kinatumia akili bandia kuelewa maswali ya wageni na kupendekeza jibu la haraka kiotomatiki kuwa jibu. Jibu lililopendekezwa linaonekana katika mazungumzo yako na mgeni, ambapo ni wewe tu unayeweza kuliona.
Utaweza kutathmini, kuhariri na kutuma jibu la haraka lililopendekezwa mara moja au kuratibu ili kutuma baadaye. Vishika nafasi katika violezo hujaza kiotomatiki maelezo fulani kuhusu nafasi iliyowekwa na tangazo, kama vile eneo, jina la mgeni na wakati wa kuingia, wakati ujumbe unatumwa. Hakikisha kwamba tangazo lako limekamilika na ni la hivi karibuni, kwa sababu ujumbe ulio na vishika nafasi tupu hautatumwa kwa usahihi.
Ujumbe ulioratibu unapokaribia, utaona kumbusho katika mazungumzo yako na mgeni. Rekebisha au ruka kutuma ujumbe ikiwa unarudia taarifa ambayo tayari umeshiriki.
Pata maelezo zaidi kuhusu kutumia majibu ya haraka ili kuokoa muda
Kuwasiliana na kikundi
Kila nafasi inayowekwa huanzisha mazungumzo mapya katika kichupo cha Ujumbe.
Mgeni aliyeweka nafasi anaweza kuwaalika watu wengine wazima wanaosafiri pamoja naye wajiunge kwenye nafasi iliyowekwa. Wageni wanaokubali mwaliko huwekwa kwenye mazungumzo na wewe hutuma ujumbe kwa kikundi kizima. Wageni wanaweza kusoma ujumbe wote, hata kama watajiunga kwa kuchelewa, kwa hivyo si lazima ujirudie.
Gusa kitufe cha Maelezo kwa taarifa zaidi kuhusu kuweka nafasi na mazungumzo, ikiwa ni pamoja na orodha ya kila mtu ambaye amejiunga. Chagua picha ya mgeni ili kufikia wasifu wake na upate maelezo zaidi kuhusu mtu unayemkaribisha.
Kutumia vipengele vingine vya kutuma ujumbe
Utapata vipengele zaidi vya kudhibiti mazungumzo katika kichupo cha Ujumbe, ikiwemo majibu kwenye mfumo wa uzi, nyenzo za kuhariri, uthibitishaji wa kusoma ujumbe na emoji.
- Majibu kwenye mfumo wa uzi hukuruhusu kuanzisha uzi wakati wa kujibu ujumbe, ambao huweka jibu lako chini ya ujumbe wa awali.
- Nyenzo za kuhariri hukuruhusu kuhariri ujumbe ndani ya dakika 15 baada ya kuutuma na kubatilisha kutuma ujumbe ndani ya saa 24.
- Uthibitishaji wa kusoma ujumbe unaonyesha iwapo wageni au wapokeaji wengine wameangalia ujumbe wako, isipokuwa kama wamezima kipengele hiki katika mipangilio ya akaunti yao.
- Emoji hukuruhusu uthibitishe ujumbe kwa uso wenye tabasamu, moyo, kidole gumba kilichoinuliwa juu, mikono ya kupiga makofi au uso unaocheka.
Maswali na Majibu kuhusu kichupo cha ujumbe
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.