Jinsi ukaaji wa muda mrefu unavyoweza kuinufaisha biashara yako ya kukaribisha wageni
Kukubali ukaaji wa muda mrefu kunaweza kuwa mkakati mzuri wa kukaribisha wageni. Unaweza kutengeneza chanzo cha mapato kinachotabirika zaidi, kupunguza mzigo wako wa kazi wa kusimamia wageni wanaoondoka na kukaribisha wageni kwa urahisi zaidi.
Kujaza kalenda yako
Ukaaji wa muda mrefu husaidia kujaza kalenda yako haraka. Uwe ni wa kuanzia wiki moja (angalau usiku saba) au kuanzia mwezi mmoja (angalau usiku 28), hupunguza idadi ya mapengo kati ya nafasi zilizowekwa.
Sehemu za kukaa za muda mrefu pia zinaweza kuunda mtiririko wa mapato unaotabirika na ulio thabiti. Unapokaribisha mgeni kwa zaidi ya mwezi, unalipwa katika awamu za kawaida.
Unaweza kuhamasisha ukaaji wa muda mrefu kwa kuweka mapunguzo ya kila wiki na kila mwezi:
Bofya au gusa aikoni ya mipangilio katika kalenda yako.
Nenda kwenye Mapunguzo kwenye kichupo chako cha Bei.
Chagua kila wiki au kila mwezi. Utapata punguzo lililopendekezwa kulingana na tangazo lako na uhitaji wa matangazo kama hayo katika eneo lako.
Sogeza kitelezeshi kati ya asilimi 0 na 99 ili kurekebisha punguzo na ufuatilie jinsi linavyobadilisha bei yako ya wastani ya kila wiki au kila mwezi.
Chagua bei ya mgeni hapa chini ili kupata mchanganuo wa bei, ikiwemo ada yoyote na mapato yako.
Gusa au bofya Hifadhi ili kuweka punguzo unalotaka.
Baadhi ya Wenyeji wanatafuta wageni ambao wanavutiwa na ukaaji wa muda mrefu. Wanashiriki viungo vya matangazo yao na kampuni au vyuo vikuu vya mahali walipo ambavyo wafanyakazi au wanafunzi wao wanaweza kuwa wanatafuta malazi ya muda.
"Ninapendelea tu kukaribisha wageni kwenye sehemu za kukaa za muda mrefu," anasema Patricia, Mwenyeji Bingwa huko Austin, Texas. "Ninatumaini kuwapa makazi wataalamu wanaosafiri ambao kazi zao zinadumu kati ya mwezi mmoja na miezi mitatu."
Kupunguza kazi yako
Uwekaji nafasi za kukaa muda mrefu, kwa ujumla humaanisha kiwango kidogo cha wageni wanaotoka, hasa linapokuja suala la kutuma ujumbe kwa wageni na kufanya usafi katika sehemu yako.
Kwa mfano, Wenyeji kwa kawaida hutumia muda mchache kuwasiliana na seti moja ya wageni wanaokaa kwa mwezi kuliko wageni kadhaa wanaokaa siku chache tu kwa wakati mmoja.
Ili kudumisha usafi, baadhi ya Wenyeji hutoa huduma za usafi na vifaa. "Ninatoa huduma ya kufanya usafi ya kila wiki bila malipo, pamoja na mashuka safi na vifaa kadhaa vya msingi, ili niweze kuhakikisha kwamba kila kitu kipo shwari," anasema Omar, Mwenyeji Bingwa katika Jiji la Mexico, ambaye ni mwenyeji wa familia na wafanyakazi wanaofanya kazi mbali na ofisi kwa hadi wiki sita kwa wakati mmoja.
Kukaribisha wageni ukiwa na uwezo wa kubadilika
Ukaaji wa muda mrefu unaweza kukufaa kikawaida ikiwa uko mbali kwa muda mrefu. Maggie, ambaye ni mwenyeji mwenza huko Northampton, Massachusetts, anasema kuwa nyumba ya wazazi wake ilikuwa tupu wakati walipokuwa huko Puerto Rico katika majira ya baridi. "Kabla ya kuanza, hatukuwa na mapato yoyote na baadaye tukatumia Airbnb na kujipatia USD3,500 kwa mwezi," anasema.
Ukaaji wa muda mrefu pia unaweza kufaa katika jumuiya zinazowekea vizuizi upangishaji wa muda mfupi. Hakikisha kwamba muda wa chini na wa juu wa kukaa ulioweka unafuata sheria na kanuni za eneo lako.
Ikiwa uko katika eneo linaloruhusu nafasi zilizowekwa za muda mfupi na mrefu, fikiria kurekebisha mipangilio yako mara kwa mara. Hii inaweza kukusaidia unufaike zaidi na uhitaji wa kimsimu katika eneo lako huku ukiwashawishi wageni kuweka nafasi ya usiku au wiki zozote zinazopatikana kati ya ukaaji wako wa kuanzia mwezi mmoja.
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.