Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Mambo ya msingi ya kuwasiliana na wageni

  Pata vidokezi na kiolezo cha kuungana na wasafiri.
  Na Airbnb tarehe 8 Jan 2020
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 6 Okt 2022

  Vidokezi

  Kuwasiliana kwa ufanisi na wageni ni hatua ya kwanza kuelekea kumpa mgeni huduma nzuri. Kama Mwenyeji, unaweza kuwasaidia wageni wajisikie vizuri na kuhimiza waandike tathmini nzuri kwa kuwasiliana waziwazi na mara moja kuanzia wageni wanapoonyesha kupendezwa na sehemu yako hadi baada ya kutoka.

  Vidokezi vya mawasiliano mazuri

  Kuwa wazi. Daniel, Mwenyeji huko San Francisco, anasema kila wakati yuko wazi kuhusu eneo lake. "Kile unachowaambia wageni wako kwamba watakipata na kile wanachokipata wanapowasili kwenye nyumba yako vinapaswa kulingana," anasema. "Ni bora kuweka matarajio ya chini kwenye tangazo lako kisha wageni wafike na kukuta eneo zuri zaidi kuliko walivyotarajia badala ya kuwaahidi mambo mazuri mno ambayo hayapo kwenye eneo lako."

  Kuwa mdadisi. Unaweza kuwezeshaujumuishi kwa kuwauliza tu wageni wako: Unahitaji nini ili ujisikie kustarehe na kuhisi kuwa umekaribishwa katika sehemu yangu? Kuonyesha kwamba unajali, bila kukisia, husaidia sana.

  Patikana. Annette, Mwenyeji Bingwa huko San Francisco, anapenda kuwaambia wageni: “Tafadhali usijaribu kufanya marekebisho yoyote mwenyewe, hata kama ni madogo mno. Wasiliana nasi mara moja na tutayashughulikia.” Kuhusu matatizo ya kawaida, Wenyeji wenye uzoefu hutumia majibu ya haraka ili kuwasiliana na wageni.

  Kuwa mwenye kujali. Matendo madogo ya fadhili yanaweza kufanya ukaaji huo uwe mzuri kwako na kwa wageni wako. Tatizo likitokea, wageni mara nyingi husema kwamba cha muhimu kwao ni jinsi Wenyeji wao wanavyojibu.

  Kuwa mjuzi. Kuwasiliana na wageni kwenye programu ya Airbnb husaidia kukulinda, kwa sababu mazungumzo yote yamerekodiwa endapo utahitaji kuyarejelea unapowasiliana na huduma kwa wateja iwapo tatizo litatokea. Pia hufanya iwe rahisi kupata taarifa zote za wageni wako katika sehemu moja.

  Nyakati muhimu za kuwasiliana na wageni

  Maulizo ya kuweka nafasi: Mgeni anapowasiliana nawe mara ya kwanza ili kuweka nafasi kwenye eneo lako, jibu la haraka linathaminiwa kila wakati. Kujibu maswali si muhimu tu kwa ajili ya kuwafurahisha wageni, hiyo pia ni mojawapo ya vigezo vya kuwa Mwenyeji Bingwa.

  Unaweza kutoa huduma yenye ukadiriaji wa nyota tano tangu mwanzo kwa kujibu maulizo yote ya wageni ndani ya saa 24. Kutumia ujumbe ulioratibiwa pia kunaweza kukusaidia kupanga mapema kuhusu jinsi ya kushiriki taarifa na wageni wako.

  Wakati wa kuweka nafasi:Wageni hufurahia Wenyeji wanapowatumia ujumbe wa "asante kwa kuweka nafasi". Unaweza kufanya ujumbe wako wa kukaribisha uwe mahususi kwa kuweka taarifa kutoka kwenye wasifu wa mgeni wako.

  Hii inaweza kujumuisha maswali kuhusu mapendeleo yake, mji wake na burudani. Hii pia ni fursa yako kuuliza maswali ya ziada, kama vile lengo la ziara yake na ni nani ataandamana naye.

  Kabla ya kuwasili: Sehemu ngumu zaidi ya usafiri mara nyingi ni kufika mahali uendako, kwa hivyo maelekezo yanayoeleweka vizuri na maelezo ya kuingia ni muhimu katika kuwasaidia wageni wako wawasili kwa namna shwari.

  Unaweza kujibu maswali ya kawaida kwa kujaza sehemu zote zilizo chini ya sehemu ya Taarifa kwa wageni ya kichupo cha Matangazo, ikiwemo maelekezo ya kwenda kwenye sehemu yako, maelekezo ya kuingia na Wi-Fi. Maelezo haya yatawekwa kwenye vichupo vya Safari za wageni wako saa 48 kabla ya wakati ulioratibiwa wa kuingia.

  Kuingia: Wageni, hasa wale kutoka jumuiya zilizotengwa kihistoria, wamesema kwamba huduma yakuingia mwenyewe inaweza kuwafanya wahisi starehe. Lakini ikiwa uko karibu, unaweza pia kuwauliza wageni wako ikiwa wangependelea kukutana nawe ana kwa ana wanapoingia. Pia unaweza kuunda mwongozo wa nyumba unaojumuisha taarifa kuhusu jinsi ya kutumia mifumo na vifaa mbalimbali katika sehemu yako.

  Baada ya usiku wa kwanza: Wenyeji wengi wanasema kwamba wanapenda kuwasiliana na wageni wakati wa safari yao. Ni muhimu kujituma na kuuliza jinsi kila kitu kinavyokwenda.

  Kabla ya kutoka: Ni wazo zuri kuwakumbusha wageni ni wakati gani wanahitaji kutoka, mahali pa kuacha ufunguo na chochote wanachohitaji kufanya katika sehemu hiyo kabla ya kuondoka, kama vile kuondoa takataka.

  Baada ya kuondoka: Baadhi ya Wenyeji wanapenda kutuma ujume mfupi wa kuwashukuru wageni kwa ajili ya ukaaji wao. Hatua hii husaidia kuwakumbusha wakuandikie tathmini wakati maelezo kuhusu kile kilichofanya eneo lako kuwa zuri bado yako akilini mwao. Ni jambo la busara pia kuwatathmini wageni wako mara moja. Kuwa mkweli na mwenye heshima katika utendaji wako na utumie viwango sawa kumtathmini kila mgeni.

  Gundua mengi katika mwongozo wetu wa kuwafurahisha wageni wako wa kwanza

  Vidokezi

  Airbnb
  8 Jan 2020
  Ilikuwa na manufaa?