Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Vidokezi vya kufanya usafi kutoka kwa Wenyeji wenye uzoefu mkubwa

Sehemu isiyo na doa husaidia kuwafanya wageni wawe na furaha na kupata tathmini nzuri.
Na Airbnb tarehe 9 Mac 2023
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 9 Mac 2023

Eneo safi linaweza kusababisha upate tathmini nzuri. Lakini ukosefu wa usafi ni mojawapo ya sababu kuu za tathmini mbaya, kwa mujibu wa data ya Airbnb. Jaribu vidokezi hivi kutoka kwa Wenyeji wenye uzoefu ili kudumisha usafi wa hali ya juu kwenye eneo lako.

Kuunda mkakati wa kufanya usafi

Iwe unasafisha mwenyewe au unaajiri wasafishaji, ni muhimu kwamba sehemu yako isafishwe vizuri baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia, kila wakati.

"Ni muhimu kuwa na uthabiti na orodha kaguzi kwa ajili ya wasafishaji," anasema Juliette, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huko Nairobi, Kenya. “Inawasaidia, kwa sababu inakuwa ratiba ya kila siku. Kutunza nyumba vizuri kwa kweli hufanya kazi.”

Ikiwa unaajiri msafishaji, pitia kwa kina mchakato wa kufanya usafi wewe mwenyewe, ili ujue hasa kile kinachohitajika kufanywa na kile cha kujumuisha katika orodha kaguzi. Hakikisha unapanga muda wa kutosha kati ya nafasi zilizowekwa ili upate muda wa kufanya kazi kikamilifu na utafuta msafishaji wa pili au uunde mpango mbadala ikiwa msafishaji wako hataweza kufika siku moja.

Kufanya usafi kwa ajili ya wageni kunahitaji umakini zaidi kuliko unavyoweza kutumia unapofanya usafi kwa ajili yako mwenyewe. Fikiria kuwekeza katika usafishaji wa kina wa mara kwa mara ili kufanya kazi za kawaida kati ya nafasi zilizowekwa zisiwe kubwa na ziwe zenye ufanisi zaidi.

Kuanza na mambo ya misingi

Juliette anasisitiza umuhimu wa kulenga maeneo fulani wakati wa kusafisha.

  • Anza na maeneo yanayotumika sana. "Jikoni na bafuni ni muhimu sana, kwa sababu ndio sehemu zinazotumiwa zaidi," anasema Juliette. Mara baada ya mabafu kutokuwa na doa, anakwenda jikoni, ambapo wasafishaji wake huosha vyombo vyote. "Tunafanya usafi wa kina sana," anasema.
  • Sehemu inayofuata: chumba cha kulala. Wasafishaji wa Juliette wanafungua droo, wanaangalia uvungu wa kitanda na kuhakikisha hakuna kitu kilichoachwa. "Kisha tunaondoa mashuka kwenye vitanda, kuruhusu hewa iingie kwenye nyumba, kufungua madirisha kabisa, kulowesha matandiko," anasema.
  • Mwishowe, shughulikia vitanda. Ratiba ya Juliette ikoje? "Magodoro yana vitambaa vya kukinga, mito ina vitambaa vya kukinga, na unabadilisha seti nzima," anasema.

Kuzingatia maelezo

Fikiri kama mgeni. Kwa mfano, Tammi, Mwenyeji huko Seattle, anasema: "Pazia la sehemu ya kuogea mara nyingi husahaulika. Nina kipande cha plastiki na ninakinyunyizia dawa na kukifuta kila mgeni anapoondoka. Pia ninakibadilisha kila baada ya mwezi mmoja au miwili."

Pia, usiache maeneo yanayoguswa sana kama vile swichi za taa. "Vitu hivyo vinaweza kuwa katika hali mbaya, lakini hutambui kwa sababu umezoea," anasema Mwenyeji Adam wa Atlanta. "Ukitumia pombe kidogo ya kusugulia inaweza kusaidia."

Kuepuka hali ya nywele kutapakaa ndani

Wageni hawataki kamwe kukuta nywele za mtu mwingine katika sehemu wanayokaa. Sue na John, Wenyeji katika Jiji la Salt Lake, wana kidokezo cha kukabiliana na nywele zinazodondoka chini: "Baada ya kufua matandiko yote, ninaweka kitambaa chenye pamba kwenye mashuka, foronya na blanketi," wanasema.

Laura, Mwenyeji huko Cottonwood, Arizona, anapendekeza kubadilisha mopa. "Safisha sakafu ya bafuni kwa mikono ukiwa umepiga magoti," anasema, kwa kutumia brashi ya kusugua au nguo zenye nyuzi ndogo. "Ni haraka na rahisi, na huwezi kukosa nywele yoyote." Na kumbuka kusafisha mifereji ya bafuni kila baada ya mgeni kutoka.

Kujaribu vidokezi vya Wenyeji wengine

Hii hapa ni hamasa ya kufanya usafi kutoka kwa Wenyeji wenye uzoefu:

  • Weka nguo kwenye mashine ya kufulia kwanza. "Jambo la kwanza ninalofanya ni kuchukua mashuka na mataulo na kuyaweka kwenye mashine ya kufulia na kazi hiyo inaendelea wakati ninafanya usafi katika maeneo mengine," anasema Emma-Kate huko San Francisco. "Inatosha."
  • Ng'arisha sakafu za mbao. “Nina sakafu za mbao ngumu. Ninazing'arisha mara kwa mara ili wageni wanapoingia waweze kuona sakafu nzuri,” anasema Tammi huko Seattle. "Inatoa mtazamo wa jumla wa usafi ambao ni wa kuridhisha."
  • Kunja tishu za chooni. "Huwa ninakunja ncha ya karatasi ya chooni," anasema Emma-Kate. "Ni jambo dogo, lakini ni jambo zuri na huonesha kuwa unajali."
  • Jaza tena sabuni ya mikono na chupa za shampuu. "Ni vizuri kuwa na vistawishi vya bafuni vinavyoonekana kuwa ni vipya," anasema Alex huko San Francisco. "Chupa iliyojaa na ambayo haijafunguliwa inamfanya mgeni ajisikie kuwa wa kwanza kuitumia."
Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Airbnb
9 Mac 2023
Ilikuwa na manufaa?