Mchakato wa kutoka ambao ni wazi na rahisi

Airbnb hutuma maelekezo yako ya kutoka kiotomatiki kwa wageni.
Na Airbnb tarehe 8 Nov 2023
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 8 Nov 2023

Mchakato wa kutoka unapaswa kuchukua jitihada kidogo kutoka kwa wageni na Wenyeji. Weka maelekezo yako katika tangazo lako na Airbnb itayatuma kiotomatiki kwa wageni usiku mmoja kabla ya kutoka.

Futa maelekezo ya kutoka

Unaweka maelekezo ya kutoka sawa na jinsi unavyoweka sheria za kawaida za nyumba. Andaa kwa haraka orodha ya kutoka kwa kuchagua kutoka kwenye kazi hizi za kawaida:

  • Kusanya mataulo yaliyotumika
  • Tupa taka
  • Zima vifaa vya umeme
  • Funga
  • Rejesha funguo

Una chaguo la kuweka maelezo kuhusu kila jukumu. Kwa mfano, unaweza kubainisha kwamba wageni huweka takataka kwenye pipa moja na vitu vinavyoweza kutumika tena kwenye pipa jingine. Unaweza pia kuandika maombi ambayo ni maalum kwa nyumba yako, kama vile kufunika jiko la kuchomea nyama baada ya matumizi.

Chagua kutoka kwenye orodha ya majukumu ya kawaida ya kutoka ili kuunda maelekezo yako ya kutoka.

Wageni wanaweza kufikia maelekezo ya kutoka na sheria za nyumba kabla ya kuweka nafasi ya eneo. Baada ya kuweka nafasi, wanaweza kupata maelekezo ya kutoka kwenye kichupo chao cha Safari, pamoja na sheria za nyumba, taarifa za Wi-Fi na maelezo mengine muhimu.

Wageni wanatarajia kutoka kwa urahisi bila majukumu yoyote ya kufanya usafi, lakini hawapaswi kuacha eneo lako katika hali ambayo inahitaji usafi wa ziada au wa kina, kwa mujibu wa sheria za msingi kwa ajili ya wageni.

"Tunataka kufanya mchakato wetu wa kutoka uwe rahisi kadiri iwezekanavyo," anasema Keshav, mwanabodi wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huko New Delhi. "Mfanya usafi anakuja na kufanya kila kitu kinachohitajika kufanywa."

Vikumbusho vya kutoka vya kiotomatiki

Tutawatumia wageni kikumbusho cha kiotomatiki kikiwa na muda wa kutoka na maelekezo yako. Hii inatumwa kama arifa ya kwenye simu katika kifaa cha mkononi cha mgeni wako siku moja kabla ya kutoka saa 11:00 jioni katika saa za eneo alipo.

Wageni wanapaswa kupakua programu ya Airbnb na kipengele cha arifa za kwenye simu kiwashwe ili kupokea kikumbusho hiki. Mara baada ya kutoka, wageni wanaweza kukujulisha kuwa wameondoka kwa mbofyo au mguso mmoja tu.

Utapaswa kusisitiza kwa nini ni lazima mtu atoke kwa wakati. "Ninawaambia wageni kwamba msafishaji atafika saa 5:00 asubuhi ili kuandaa fleti kwa ajili ya wageni watakaofuata, kwa hivyo wanaelewa kwa nini ni muhimu kutoka kwa wakati," anasema Joh, Mwenyeji Bingwa huko San Francisco.

Wageni hupata kikumbusho cha kiotomatiki cha kutoka kikiwa na wakati wa kutoka na maelekezo yako.

Kadi za kutoka

Kadi ya kutoka ni njia rahisi ya kutuma taarifa za kutoka kwa wageni wako. Mara baada ya kuweka maelekezo ya kutoka, unaweza kuweka kadi ya kutoka kwenye jibu la haraka au ujumbe ulioratibiwa. Kadi inaunganishwa kwenye maelekezo yako.

Ingawa Airbnb itatuma kiotomatiki kikumbusho kwa wageni usiku mmoja kabla ya kutoka, daima wewe ndiye mwenye udhibiti wa uzoefu wa wageni. Unaweza kuweka ujumbe ulioratibiwa ili utume kikumbusho cha kutoka moja kwa moja kwenye kikasha cha Airbnb cha wageni wako, ikiwa hawajapakua programu au hawajawasha kipengele cha arifa kwa simu.

Maoni ya kutoka

Baada ya wageni kuondoka, wanaweza kumpatia Mwenyeji wao ukadiriaji wa nyota na kubainisha kilichokwenda vizuri au kinachoweza kuwa bora zaidi. Chaguo moja ni kuripoti "kazi nyingi wakati wa kutoka." Matangazo yenye ukadiriaji wa chini kwa kujirudia kutokana na kazi zisizofaa wakati wa kutoka yanaweza kuondolewa kwenye Airbnb.

Wageni pia huchagua ukadiriaji wa jumla wa nyota kwa ajili ya ukaaji wao. Maoni na ukadiriaji wa nyota kwa ajili ya vipengele mahususi, kama vile mawasiliano, hauathiri hadhi ya Mwenyeji Bingwa.

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
8 Nov 2023
Ilikuwa na manufaa?