Wavutie wageni ukitumia Wi-Fi ya kasi na ya kuaminika
Wageni wengi wanategemea intaneti ya kasi wakati wa safari yao, hasa ikiwa wanatiririsha video au wanafanya kazi wakiwa mbali. Kwa kweli, wageni hutafuta Wi-Fi mara nyingi zaidi kuliko vistawishi vingine vyovyote kwenye Airbnb.*
Kuweka Wi-Fi ya kasi kwenye tangazo lako kunalisaidia lionekane kwenye matokeo ya utafutaji. Unaweza kuthibitisha kasi ya muunganisho wako ukitumia jaribio la kasi ya Wi-Fi.
Kufanyia majaribio kasi ya Wi-Fi yako
Utahitaji kuwa kwenye nyumba yako ili kufanyia majaribio kasi ya Wi-Fi yako. Hakikisha umeunganishwa kwenye mtandao wa Wi-Fi na umeingia kwenye programu ya Airbnb kwenye kifaa cha iOS au Android.
Nenda kwenye kichupo cha Matangazo kisha uchague tangazo unalotaka. Gusa Vistawishi kisha ufuate hatua hizi:
- Gusa jumlisha (+) ili uweke Wi-Fi kama kistawishi au uguse Hariri ikiwa tayari umeiweka.
- Gusa Anza jaribio (unaweza kuhitaji kutoa ufikiaji wa mtandao wako).
- Matokeo yanapoingia, gusa Weka kwenye tangazo ili kuonyesha maelezo ya Wi-Fi yako kwenye tangazo lako.
Baada ya kuweka kasi ya Wi-Fi yako kwenye tangazo lako, wageni wataona kwamba sehemu yako inaitoa kama kistawishi. Ikiwa usomaji wako ni Mbps 50 au zaidi, "Wi-Fi ya kasi" pia itaonekana kama kidokezi kwenye sehemu ya juu ya tangazo lako.
Kuelewa kasi ya Wi-Fi yako
Jaribio la kasi ya Wi-Fi hupima kasi ya muunganisho katika megabiti kwa sekunde. Huu ni usomaji tofauti unaoweza kupata.
- Mbps 50 na zaidi: Wi-Fi ya kasi. Wageni wanaweza kutazama video za 4K mtandaoni na kujiunga kwenye simu za video kwenye vifaa vingi.
- Mbps 25-49: Wi-Fi ya haraka. Wageni wanaweza kutazama video za 4K zenye ubora wa juu mtandaoni na kujiunga kwenye simu za video.
- Mbps 7-24: Wi-Fi thabiti. Wageni wanaweza kutazama video za HD mtandaoni.
- Mbps 1-6: Wi-Fi ya msingi. Wageni wanaweza kuangalia ujumbe na kuvinjari wavuti.
- Haionyeshi usomaji: Huna Wi-Fi au huwezi kuunganisha kwenye mtandao. Jaribu kuwasha upya ruta yako au uende kwenye sehemu nyingine kwenye nyumba yako.
Pata maelezo zaidi kuhusu kuthibitisha kasi ya intaneti yako
*Kulingana na takwimu za ndani za Airbnb zinazopima vistawishi vilivyotafutwa mara nyingi zaidi na wageni ulimwenguni kote kuanzia tarehe 1 Januari hadi tarehe 31 Desemba, 2024.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.