Kidokezi kipya husaidia nyumba bora zionekane
Wageni wanawaamini Wenyeji kila wakati wanapoweka nafasi. Wanapaswa kuwa na uhakika kwamba wanajua nini cha kutarajia kabla ya kuweka nafasi.
Njia moja ambayo wageni wanaweza kupata sehemu nzuri ya kukaa ni kupitia Vipendwa vya Wageni, nyumba zinazopendwa zaidi kwenye Airbnb, kwa mujibu wa wageni.
Kuanzia mwezi Mei, kidokezi kipya kitasaidia matangazo maarufu kuonekana na kufanya iwe rahisi kwa wageni kuchagua eneo linalokidhi mahitaji yao.
Kidokezi ni nini?
Kidokezi kipya kinaonyesha jinsi matangazo yanayostahiki yanavyolingana na mengine kulingana na ukadiriaji, tathmini na kutegemeka. Matangazo yenye angalau tathmini tano katika miaka miwili iliyopita yanastahiki kidokezi.
Asilimia 10 bora ya matangazo yanayostahiki yanaangaziwa na:
- Kombe la dhahabu
- Beji ya dhahabu ya Vipendwa vya Wageni
- Lebo iliyo na nafasi bora ya asilimia 1, 5 au 10 ya tangazo
Kidokezi cha asilimia 10 bora kinaonekana kwenye ukurasa wa tangazo na juu ya tathmini.
Pia tutawaonyesha wageni wakati tangazo liko katika asilimia 10 ya chini ya matangazo yanayostahiki. Kidokezi cha asilimia 10 ya chini kinaonekana juu ya tathmini.
Kidokezi husasishwa mara kwa mara kwa kutumia mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
- Ukadiriaji wa jumla wa nyota na maoni katika tathmini za wageni
- Ukadiriaji wa aina ndogo kwa ajili ya kuingia, usafi, usahihi, mawasiliano ya Mwenyeji, mahali na thamani
- Viwango vya kughairi kwa Mwenyeji
- Matatizo yanayohusiana na ubora yameripotiwa kwa Usaidizi wa Jumuiya ya Airbnb
Utaendelea kupata arifa wakati wowote mgeni anapoweka ukadiriaji na kutathmini tangazo lako au kuripoti tatizo linalohusiana na ubora. Na bado unaweza kuripoti tathmini ambayo unaamini inakiuka Sera yetu ya Tathmini.
Pata vidokezi vya kukaribisha wageni kwa ukadiriaji wa nyota 5
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.