Njia mpya za wageni kugundua tangazo lako

Pata maelezo kuhusu badiliko kubwa kwa Airbnb katika muongo mmoja na maana yake kwa Wenyeji.
Na Airbnb tarehe 11 Mei 2022
Inachukua dakika 5 kusoma
Imesasishwa tarehe 11 Mei 2022

Vidokezi

Safari za kukumbukwa zaidi mara nyingi huanza kwa kuwa na shauku ya kutoka na kwenda mbali. Ili kujua wapi pa kwenda na lini, wasafiri mara nyingi hutafuta mawazo mtandaoni wanapojaribu kutengeneza mpango kamili. Kwa hivyo tunawaletea njia mpya kabisa ya wageni kuchunguza Airbnb na kugundua matangazo mazuri kama yako.

Airbnb 2022 Toleo la Kiangazi linawakilisha mabadiliko makubwa zaidi kwenye Airbnb katika muongo mmoja. Ubunifu mpya kabisa unaonyesha matangazo katika Aina 56 za Airbnb na kufanya iwe rahisi kwa wageni kupata na kuweka nafasi katika maeneo ambayo hawakujua kamwe yapo, pamoja na kipengele cha ubunifu kinachoitwa Kukaa Kwenye Nyumba Mbili, ambacho kinawaruhusu wageni kugawanya ukaaji wa muda mrefu kati ya nyumba mbili.

Kama Mwenyeji, unaweza kufaidika na vipengele hivi vya kuvutia kwa kuhakikisha tangazo lako lina maelezo kamili na ya sasa, upatikanaji wa hivi karibuni na picha za ubora wa juu.

Njia nyingi zaidi za kugunduliwa

Ubunifu mpya wa Airbnb hulisaidia tangazo lako, iwe ni chumba cha pamoja, chumba cha kujitegemea au nyumba nzima, gunguliwa na wageni wengi wa aina mbalimbali mapema katika mipango yao ya safari.

Wageni wanaweza kupata tangazo lako na:

  • Aina za Airbnb. Kila mara wageni wanapofungua programu, wanaletewa sehemu nzuri za kukaa zinazopatikana hivi karibuni ambazo wanaweza kuwekea nafasi mara moja.
  • Kukaa Kwenye Nyumba Mbili. Matokeo ya utafutaji ya sehemu za kukaa za usiku saba au zaidi sasa yanajumuisha chaguo la wageni kugawanya safari yao kati ya sehemu mbili.
  • Uwezo zaidi wa kubadilika. Wageni wanaweza kutafuta sehemu za kukaa kwa kutumia tarehe na maeneo yaliyo wazi, kwa kutumia vipengele tulivyozindua mwaka jana au wanaweza kupunguza matokeo yao ili kukidhi mahitaji mahususi.

Jinsi Aina za Airbnb zinavyofanya kazi

Wageni wanapofungua Airbnb, wanaonyeshwa aina kwenye sehemu ya juu ambayo huyapanga matangazo katika makusanyo yaliyopangwa kulingana na mtindo wa kipekee, eneo au shughuli za karibu. Aina hizo zinaonyesha sehemu za kukaa zilizo na vipengele kama vile mandhari za kipekee au majiko ya mpishi, ukaribu na ziwa au hifadhi ya taifa au ufikiaji wa maeneo ya gofu au kuteleza mawimbini.

Wageni wanapotafuta sehemu za kukaa katika eneo mahususi, wanapata matokeo yanayofanana na ya hapo awali, katika kundi linaloitwa Nyumba Zote. Sasa, pia watapata makundi ya ziada kulingana na eneo hilo, ikifanya iwe rahisi kugundua nyumba nzuri zilizo ndani ya eneo lao la utafutaji au nje kidogo tu.

Matangazo pia yanaweza kuonekana katika makundi mengi. Ikiwa nyumba yako ya ziwani ina jiko la mpishi, tangazo hilo linaweza kuonekana katika Kundi la Ziwa na Kundi la Jiko la Mpishi, pamoja na matokeo ya utafutaji ya eneo lako.

Mojawapo ya makundi mapya ya kipekee zaidi ni Ubunifu, mkusanyiko wa nyumba zaidi ya 20,000 zilizochaguliwa kwa ajili ya usanifu wake maarufu na ubunifu wa ndani unaovutia. Kundi la Ubunifu linajumuisha nyumba kutoka kwa wasanifu majengo maarufu kama vile Frank Lloyd Wright na Zaha Hadid, zile ambazo zimeonyeshwa kwenye machapisho ya ubunifu na sehemu zinazotolewa na Wenyeji ambao wamefanya kazi ya kipekee ya kutekeleza kanuni zao wenyewe za ubunifu.

Ubunifu mpya kabisa unaonyesha matangazo katika Aina 56 za Airbnb, ikiwemo Ubunifu, Mashambani na Nyumba ya Kwenye Mti.

Hizi ni baadhi tu ya Aina za Airbnb: Mandhari za Kipekee, Ufukwe, Kupiga Kambi, Majiko ya Mpishi, Mashambani, Sehemu za Ubunifu, Maeneo ya Gofu, Nyumba za Kihistoria, Miji Maarufu, Hifadhi za Taifa, Kuteleza Thelujini, Kuteleza Mawimbini, Mazingira ya Joto na Mashamba ya Mizabibu.

Makundi haya ni mwanzo tu wa njia hii mpya ya kutafuta, ambayo inawaruhusu wageni wagundue maeneo zaidi kuliko hapo awali. Baada ya muda tutaanzisha makundi zaidi ambayo yanaonyesha vipengele vya kipekee na maeneo maalumu ya nyumba zako. Tunaamini kwamba makundi ndio mustakabali wa utafutaji na kuna kundi kwa ajili ya kila nyumba na kila Mwenyeji kwenye Airbnb.

Nyumba katika kila kundi hupitia mchakato wa utayarishaji. Mamilioni ya matangazo amilifu kwenye Airbnb hutathminiwa kwa kutumia uchanganuzi wa kompyuta ili kuchambua vichwa, maelezo, maelezo ya picha na tathmini za wageni. Kwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kwamba taarifa za tangazo lako zimesasishwa na ni kamili.

Jinsi huduma ya Kukaa Kwenye Nyumba Mbili inavyofanya kazi

Wageni wanaweza kuvinjari na kuwekea nafasi matangazo yote wakiwa na uwezo wa kubadilika kadiri hali zao zinavyoruhusu. Kipengele cha Kukaa Kwenye Nyumba Mbili kinawapa Wenyeji wengi zaidi fursa ya kuwa sehemu ya safari ya wageni.

Wageni wanapotafuta safari ya wiki moja au zaidi, sehemu za Kukaa Kwenye Nyumba Mbili huonekana kiotomatiki katika matokeo ya utafutaji. Wanapoteremka chini kwenye Kundi la Nyumba Nzima, wageni wanaweza kupata machaguo ya kugawanya safari yao kati ya nyumba mbili katika eneo moja.

Kipengele cha Kukaa Kwenye Nyumba Mbili kinaongeza matangazo asilimia 40 zaidi kwenye matokeo ya utafutaji wageni wanapotafuta ukaaji wa usiku 14 au zaidi.*

Hapo awali, ikiwa wageni wangetafuta safari ya mwezi mzima lakini ulikuwa na upatikanaji wa wiki mbili tu wakati huo, nyumba yako isingeonekana katika matokeo ya utafutaji. Kupitia huduma ya Kukaa Kwenye Nyumba Mbili, tangazo lako linaweza kuunganishwa na jingine ili kushughulikia safari nzima ya mgeni.

Kila sehemu ya Kukaa Kwenye Nyumba Mbili huunganisha nyumba mbili zinazolingana na eneo, aina ya nyumba na vistawishi kutoka kwenye utafutaji. Kwa mfano, ikiwa familia inatafuta nyumba nzima iliyo na vipengele vya ufikiaji, kama vile mlango wa kuingia usiokuwa na ngazi au milango yenye upana wa zaidi ya inchi 32, sehemu za Kukaa Kwenye Nyumba Mbili zitaunganisha matangazo mawili yaliyo na vipengele hivi.

Wageni wanapoweka nafasi ya Kukaa Kwenye Nyumba Mbili, Wenyeji hupata maombi tofauti ya kuweka nafasi. Bei yako na sheria za nyumba zinatumika kwa idadi ya usiku uliowekewa nafasi, kama ilivyo kwa nasafi nyingine yoyote iliyowekwa.

Unachoweza kufanya ili uonekane

Vipengele vipya vya Airbnb vinaonyesha nyumba yako kwa watu wengi katika maeneo mengi zaidi kuliko hapo awali. Hizi ni njia kadhaa unazoweza kufanya ili tangazo lako lionekane:

  1. Eleza kile kinachofanya eneo lako liwe la kipekee kwa kutumia picha za ubora wa juu. Picha zenye maelezo, iwe zimepigwa na mtaalamu au na simu mahiri yako, zinaweza kulisaidia tangazo lako liwavutie wageni.
  2. Tathmini orodha ya vistawishi na vipengele na uangalie kitu chochote kipya. Weka au usasishe kila kitu ambacho eneo lako linatoa, ukikumbuka vistawishi maarufu ambavyo wageni wanataka, ili liingie katika makundi yanayofaa.
  3. Fanya jaribio la kasi ya Wi-Fi. Ufikiaji wa intaneti unaoaminika unaweza kuwahakikishia wageni kwamba wataweza kufanya kazi na kuwasiliana mtandaoni kama inavyohitajika wakati wa ukaaji wao.
  4. Fikiria ikiwa tangazo lako linafikika kwa wasafiri wote. Weka picha na maelezo ya vipengele vya ufikiaji, kama vile milango ya kuingia isiyo na ngazi na milango mipana, ambayo hufanya iwe kivutio kwa wageni wenye mahitaji mbalimbali.

Kusasisha tangazo lako kwa kuweka maelezo yote, makubwa na madogo, kunaweza kusaidia tangazo lako liwafikie wageni wengi wa aina mbalimbali. Eneo lako linaweza kuwa tu kile wanachotafuta.

*Kulingana na takwimu za majaribio ya ndani ya Airbnb kufikia tarehe 14/4/2022.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

Airbnb
11 Mei 2022
Ilikuwa na manufaa?