Jinsi ya kushughulikia tathmini ya kulipiza kisasi
Wenyeji wanapaswa kujisikia huru kukaribisha wageni bila kuwa na wasiwasi kuhusu uwezekano wa tathmini ya kulipiza kisasi. Unaweza kuomba kuondolewa kwa tathmini ambazo unaamini zinakwenda kinyume na Sera yetu ya Tathmini, kama vile tathmini ya kulipiza kisasi.
Kuomba kuondolewa kwa tathmini ya kulipiza kisasi
Tathmini za kulipiza kisasi ni tathmini za kibaguzi ambazo wageni wanaweza kuacha baada ya kuripoti ukiukaji mkubwa wa sera, kama vile:
- Kuharibu mali yako
- Kupitisha muda wa kukaa kwenye nafasi aliyoweka
- Kukiuka sheria zako za kawaida za nyumba
- Kufanya sherehe au tukio lisiloidhinishwa mahali pako
Hebu tuseme mgeni anavuta sigara nyumbani kwako, kinyume cha sheria za nyumba yako. Unamwambia mgeni wako kwamba umekuta mabaki ya sigara sebuleni na uwasilishe ombi la kufidiwa ili uweze kufanya usafi wa kina. Kwa kujibu, mgeni wako anakataa kulipa kisha anaandika tathmini ya hasira. Unaweza kupinga tathmini hii na tutachunguza ili kubaini ikiwa inastahiki kuondolewa.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuomba kuondolewa kwa tathmini
Kuomba kuondolewa kwa tathmini hakuhakikishii kwamba itaondolewa. Utaombwa uonyeshe jinsi ambavyo tathmini haifuati Sera yetu ya Tathmini. Utaweza kutupatia maelezo na hati zozote kuhusu ukiukaji wa sera, kama vile picha au nyuzi za ujumbe kwa wageni.
Hati zako zitahitaji kuthibitisha kuwa kuna ukiukaji dhahiri wa sera uliotokea. Lazima pia iwe wazi kwamba kuripoti ukiukaji wa sera kwa Airbnb na/au mgeni kuna uwezekano kulisababisha tathmini ya kulipiza kisasi.
Ni wazo zuri kuweka mawasiliano yote na wageni kwenye kichupo chako cha Ujumbe, ili Airbnb Usaidizi iweze kutathmini hati hizi kwa urahisi.
Wenyeji wametuambia sera yetu kuhusu tathmini za kulipiza kisasi imewasaidia kukaribisha wageni kwa kujiamini. Mwenyeji Leanne anasema tathmini ya kulipiza kisasi kwenye tangazo lake "ilitathminiwa mara moja na kuondolewa nilipofanya ombi hilo. Nilihisi Airbnb imeniunga mkono.”
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.