Wasiliana kwa ufanisi zaidi ukitumia maboresho ya ujumbe
Kutuma ujumbe ni sehemu kubwa ya kuwasiliana kwa ufanisi kama mwenyeji. Maboresho kwenye kichupo cha Ujumbe yatakusaidia kuokoa muda na kuwajibu wageni kwa uwazi.
Violezo vipya vya majibu ya haraka vina majibu ya maswali yaulizwayo mara kwa mara, kwa hivyo si lazima uanze kuandika kutoka mwanzo. Unaweza kuhariri na kutuma violezo hivi wakati wa kuzungumza na wageni au kuviratibu kwa ajili ya kutuma baadaye.
Vipengele vingine vipya katika kichupo cha Ujumbe ni pamoja na:
- Majibu kwenye mfumo wa uzi ambayo hukusaidia kupanga mazungumzo
- Nyenzo za kuhariri zinazokuruhusu kuhariri au kubatilisha ujumbe uliotuma
Maboresho haya yanawasilishwa kwa wenyeji wote katika miezi ijayo.
Majibu mapya ya haraka
Zaidi ya dazeni ya violezo vipya vya majibu ya haraka hukupa majibu ya sampuli ya maswali maarufu ya wageni kuhusu mada kama vile maelekezo, Wi-Fi na kutoka. Tumia ujumbe ulioandikwa mapema kama ulivyo au uhariri ili kuonyesha mtindo wako wa kukaribisha wageni, vistawishi au mahitaji ya wageni.
Violezo vipya pia huweka vipengele ili kufanya mawasiliano yawe ya haraka na rahisi.
- Mapendekezo: Wakati mojawapo ya violezo vipya vinaweza kukusaidia kujibu swali la mgeni, jibu la haraka lililopendekezwa na AI linaonekana kiotomatiki katika mazungumzo yako, ambapo ni wewe tu unayeweza kuliona. Unaweza kutathmini na kuhariri jibu kabla ya kulituma au uandike ujumbe tofauti.
- Maelezo: Majibu mapya ya haraka yana vishika nafasi ambavyo hujaza kiotomatiki jina la mgeni na maelezo fulani ya nafasi iliyowekwa na tangazo wakati ujumbe unatumwa.
- Vikumbusho: Ujumbe ulioratibu unapokaribia, utaona kumbusho katika mazungumzo yako na mgeni. Rekebisha au ruka kutuma ujumbe ikiwa unarudia taarifa ambayo tayari umeshiriki.
Vipengele vipya vitapatikana mapema mwaka 2025. Hadi wakati huo, unaweza kutumia nyenzo zetu za sasa ili kuunda majibu yako ya haraka na ujumbe ulioratibiwa kwa ajili ya wageni. Hutapoteza violezo vyovyote ambavyo umehifadhi tunapoongeza vipya.
Majibu kwenye mfumo wa uzi na nyenzo za kuhariri
Tunakuletea majibu kwenye mfumo wa uzi na nyenzo za kuhariri ili kukusaidia kusimamia ujumbe wako.
- Majibu kwenye mfumo wa uzi: Unapojibu ujumbe mahususi kama uzi, jibu lako linakuwa chini ya ujumbe wa awali. Wageni wanaweza kujibu kwa njia ileile, wakiunda mfululizo wa ujumbe unaohusiana.
- Nyenzo za kuhariri: Utaweza kuhariri ujumbe ndani ya dakika 15 baada ya kuutuma na kubatilisha ujumbe uliotuma ndani ya saa 24.
Majibu kwenye mfumo wa uzi na nyenzo za kuhariri zitaanza kuzinduliwa mwezi Novemba. Maboresho ya kichupo cha Ujumbe ni sehemu ya Toleo la Oktoba 2024.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.