Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Hekima inayofanya kazi: Mahojiano na Chip Conley

Mtaalamu huyo wa ukarimu anajadili kitabu chake kipya na kwa nini hekima katika ukaribishaji wageni ni muhimu.
Na Airbnb tarehe 21 Ago 2018
Inachukua dakika 4 kusoma
Imesasishwa tarehe 21 Apr 2021

Tunafurahi kumkaribisha Chip Conley kushiriki maoni yake kuhusu uhusiano kati ya hekima na kazi na jinsi jumuiya ya wenyeji wa Airbnb imesaidia kuathiri kazi yake. Mjasiriamali wa sekta ya ukarimu wa muda mrefu, mshauri wa kimkakati wa Airbnb, mwandishi na bingwa wa wenyeji, uwekezaji wa Chip katika jumuiya hii ya wenyeji umekita mizizi na una urithi wa kudumu. Kitabu chake kipya, Wisdom@Work: The Making of a Modern Elder, kinaahidi kubuni upya wazo la kuzeeka kama fursa ya kushiriki maarifa na kuwa mwanafunzi tena.

S: Umewekeza kwa biashara ya utalii na katika jumuiya ya wenyeji wa Airbnb kwa miaka mingi. Kazi hiyo ilihamasisha vipi hekima unayoshiriki katika kitabu chako kipya?
Chip Conley:
“Kwanza kabisa, ninaikumbuka jumuiya yetu ya wenyeji. Katika miaka yangu minne ya uongozi kwenye kampuni, nilipenda kusafiri kote ulimwenguni huku nikijifunza kutoka kwa wenyeji wetu. Kuna msemo wa zamani, 'Maarifa huongea, lakini hekima husikiliza,' na nikaona jumuiya yetu ya wenyeji kuwa wasikilizaji mahiri lakini pia wachangiaji wazuri sana kwenye jumuiya kwa ujumla. 'Hekima ya umati' (jumuiya yetu ya wenyeji ya kimataifa) ilinielimisha kiasi na ninatumaini wataona maoni yao yakiwakilishwa katika kitabu changu kipya, ambacho kinaelezea kwa nini ulimwengu unahitaji kuthamini hekima katika ulimwengu ambao unazidi kutawaliwa na teknolojia.”

S: Je, wenyeji wanaweza kujifunza nini kutoka kwa mtazamo wako wa hekima katika uzoefu wao wa kukaribisha wageni?
Conley:
“Imekuwa jambo la kusisimua kuwa mara mbili ya umri wa mfanyakazi wa kawaida katika Airbnb kwa muda wa miaka mitano na nusu ambapo nimekuwa kwenye kampuni (mwaka mmoja na nusu uliopita kama mshauri). Nimejitahidi sana kuwa bingwa kwa jumuiya yetu ya wenyeji hasa wale ambao ni wazee kidogo. Brian na waanzilishi wenzake wanathamini sana kuwa wenyeji wenye umri wa miaka 50 na zaidi wanapokea alama za juu zaidi za kuridhika kwa wageni wa Airbnb katika kundi lolote la watu. Kunaweza kuwa na sababu chache za hali hii: muda zaidi wa kuzingatia stadi zao za kukaribisha wageni, uwezo unaoongezeka wa kudhibiti hisia (kipengele muhimu cha wenyeji bora) tunapozeeka na labda kujizatiti kwa muda mrefu kwa kukaribisha wageni kama njia ya kujipatia mapato ya kustaafu. Sidhani kuwa kundi lolote la umri linamiliki hekima, lakini ni sifa ambayo mtu anaweza kukuza na kuvuna baada ya muda.”

S: Je, dhana ya ukarimu imebadilika vipi, au la, kwako kuanzia miaka ya 20, 30, 40 na zaidi?
Conley:
"Wakati nilianza Joie de Vivre Hospitality katikati ya umri wa miaka ya 20 (1987), kampuni hiyo ilikuwa mojawapo ya kampuni za kwanza za hoteli mahususi huko Marekani. Tulikuwa tukithibitisha kuwa idadi kubwa ya wasafiri walikuwa wakitafuta uzoefu wa hoteli uliobinafsishwa zaidi na wa maeneo husika. Jambo la kupendeza ni kwamba tulibadilisha jina la mawakala wetu wa dawati la mbele kutoka 'makarani' na kuwa 'wenyeji,' kwa hivyo wazo la kukaribisha wageni limekuwa katika damu yangu kwa miaka 32. Kwa miaka 24 nilipokuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, tuliunda hoteli 52 mahususi na ikawa dhahiri kuwa kampuni kubwa za kimataifa zilitaka kuanza kufanana zaidi na hoteli mahususi (umakini zaidi kwa ubunifu, mikahawa na baa bora, umakini zaidi kwa uzoefu wa eneo husika, n.k.). Wakati nilijiunga na Airbnb kama Mkuu wa Ukarimu wa Kimataifa na Mkakati, niliona wimbi hili jipya la kushiriki nyumba kama uvumbuzi bayana wa hoteli mahususi, kwani teknolojia iliruhusu Airbnb kuchukua umakini huu wa ukarimu wa eneo husika na kuufanya uwe wa kimataifa. Brian Chesky alipokuja kunirai nijiunge na kampuni hii miaka mitano na nusu iliyopita, aliuliza, 'Je, ungependa kufanya biashara ya utalii iwe ya kidemokrasia?' Na nadhani hivyo ndivyo Airbnb na jumuiya yetu nzuri ya wenyeji ilivyofanya.”

S: Ni ushauri gani unaweza kumpa mwenyeji mpya anapoanza?
Conley:
"Ubora wa kawaida wa wenyeji wetu bora kote ulimwenguni ni mchanganyiko wa kujipanga vyema na kuwa wakarimu sana na wenye huruma. Hizo ni sifa tofauti na baadhi ya wenyeji wanaweza kuwa bora kwa mojawapo kuliko nyingine, lakini wale ambao wanaweza kuwa wajuzi wa zote mbili—wakati mwingine ni wenzi ambao wana mchanganyiko wa sifa hizo—watafanikiwa sana.”

S: Ni nini kinachofuata kwako, Chip? Unataka msimu huu ujao uwe wa aina gani kwako?
Conley:
“Ninaendelea kuwa mshauri wa kimkakati kwa Brian na timu yake ya waandamizi. Mchakato wangu wa kuandika Wisdom@Work ulinisaidia kuona ni watu wangapi katika umri wa kati na zaidi walio na hamu ya kutafakari tena maisha yao na kazi lakini kwamba tuna rasilimali chache za kuwasaidia watu wanaozinduka katika umri wa makamo. Kwa hivyo, nimeunda shule ya kwanza ya hekima ya watu wenye umri wa makamo, Modern Elder Academy, inayojizatiti kutoa eneo na zana za kuanza kubuni upya maisha yenye uzoefu mwingi ya mwanafunzi. Ni kampasi ya ufukweni, safari ya saa moja kaskazini mwa Cabo San Lucas huko Baja kusini, Meksiko, kwa hivyo nimerudi tena kwenye biashara ya utalii. Tuna watu wanaokuja kuungana nasi kutoka kote ulimwenguni.”

Ili kusoma zaidi kuhusu kitabu cha Chip na Modern Elder Academy, tembelea tovuti yake.

Taarifa iliyo katika makala hii inaweza kuwa imebadilika tangu kuchapishwa.

Airbnb
21 Ago 2018
Ilikuwa na manufaa?