Jinsi ya kusaidia kuzuia changamoto za kukaribisha wageni
Vidokezi
Kuwa na taarifa za mawasiliano za fundi bomba, fundi umeme na Mwenyeji Mwenza karibu ili iwe rahisi kutatua matatizo
Matengenezo ya kawaida husaidia kuweka sehemu yako katika hali nzuri
Mawasiliano yaliyo wazi na kuelewa watu kunaweza kukusaidia kuzuia na kudhibiti changamoto
Licha ya juhudi zako bora, nyakati nyingine shida hutokea tu. Labda mgeni hapati ufunguo uliomwachia au mabomba yameziba. Ingawa ni nadra kukabili tatizo kubwa, Wenyeji wenye mafanikio wanaweka mipango kwa ajili ya mambo yasiyotarajiwa.
Hivi ndivyo Diana, Mwenyeji Bingwa kutoka Oakland, California, anavyopendekeza ushughulikie changamoto wakati wa kukaribisha wageni.
1. Kusanya timu ya usaidizi
Kukaribisha wageni kunahusu jumuiya na jumuiya hiyo inajumuisha watu wanaosaidia biashara yako ya kukaribisha wageni iendelee vizuri.
"Tuna majina na nambari za simu za fundi bomba, fundi umeme na msafishaji wa nyumba tayari," anasema Diana. Na anapokuwa ameondoka mjini, Diana ana dada yake, ambaye ni Mwenyeji wake mbadala, tayari kupigiwa simu. "Hatujaachwa njia panda kamwe ikiwa tatizo linatokea."
2. Kufanya matengenezo ya kawaida
Ni nini bora kuliko kuwa tayari kushughulikia haraka bomba linalovuja au kipasha joto kilichoharibika? Kuzuia tatizo hilo lisitokee hata kidogo.
"Nina orodha kaguzi ya matengenezo ninayotathmini kila mwaka," anasema Diana. "Mimi huzifanya mwenywe baadhi ya kazi hizi, nyingine naajiri wataalamu wazifanye. Kila sehemu ni tofauti, lakini ni muhimu kubainisha kile kinachohusika katika kuiweka sehemu yako katika hali nzuri kwa ajili ya wageni."
Orodha kaguzi ya matengenezo ya kila mwaka ya Diana inajumuisha:
- Kuondoa majani na takataka nyingine kwenye michirizi
- Kuhakikisha kwamba mifumo yote ya kupasha joto, hewa safi na viyoyozi inafanya kazi
- Kusafisha taa za juu ambazo ni ngumu kufikia ili sehemu yake iendelee kuwa na mwangaza wa kutosha
3. Fanya mawasiliano yawe kipaumbele
Mawasiliano mazuri na wageni yanamaanisha kuwa mwaminifu na mkweli.
"Nadhani ni muhimu sana usiahidi mambo mengi kupita kiasi, lakini badala yake utoe mawasiliano ya kutosha," anasema Diana. "Hata kama sina suluhisho, ninamjulisha mgeni kile ninachofanyia kazi."
Kwa hivyo bomba lilipopasuka kabla ya mgeni kuwasili, Diana alichukua simu mara moja.
"Nilimpigia mgeni na kumjulisha kwamba tunashughulikia hali hiyo na nikamuuliza ikiwa tungeweza kuchelewesha saa yake ya kuingia," anasema Diana. "Pia niliahirisha saa yake ya kutoka, jambo ambalo alipenda na nikamwachia chupa ya mvinyo na barua ya shukrani. Kwa wageni wengi, mawasiliano ya wazi na ishara ndogo ndogo za shukrani—iwe ni mvinyo au kadi ya zawadi ya kununua vitu kwenye duka la kahawa la eneo husika—husaidia sana.”
4. Sikiliza na uonyeshe huruma
"Tuna milango migumu ambayo mara nyingi wageni hushindwa kufungua, hata ingawa nimeweka maelekezo katika mwongozo wa nyumba na maelekezo ya kuingia," anasema Diana. "Jambo hili linapotokea, mimi husikiliza kero zao kila wakati kisha nazungumza nao kwa subira kwa simu au ana kwa ana."
Mambo machache ambayo Diana amejifunza kwa kuwasikiliza wageni wake kwa miaka mingi:
- Toa huduma ya kuingia bila kutumia ufunguo ili kufanya uingiaji uwe rahisi
- Weka taa zenye mwangaza wa kutosha nje ili kuwasaidia wageni wawasili salama wakati wa giza
- Omba taarifa ya usafiri mapema na urudie kutaja saa za kuingia na kutoka
5. Tarajia sehemu za kawaida zinazoleta kero
Wageni kuwasili mapema, kuchelewa kutoka na matatizo ya usafi yote hayo yanaweza kusababisha changamoto. Hapa kuna mawazo kadhaa kwa ajili ya kupunguza matatizo yanayoweza kutokea:
- Weka saa zilizo dhahiri za kuingia na kutoka na sababu yako ya kuziweka ("Tafadhali usiingie kabla ya saa 9:00 alasiri ili kuwapa wasafishaji muda wa kuandaa chumba chako")
- Weka mapendeleo yako ya nafasi iliyowekwa ili uache muda zaidi wa kufanya usafi
- Zingatia kujitolea kuhifadhi mizigo ya wageni ikiwa unajua watafika mapema
- Jumuisha maelezo muhimu—jinsi ya kuingia kwenye sehemu yako, jinsi sehemu yako inavyoonekana, n.k.—katika maelezo ya tangazo lako na maelekezo ya kuingia ili kusaidia kuweka matarajio
Toa mwongozo wa nyumba ambao una maelekezo ya kufikia Wi-Fi na jinsi ya kutumia vifaa vinavyoleta changamoto
Kwa kutarajia changamoto kabla hazijaibuka, umekaribia sana kuunda ukaaji bora wa wageni.
Na ikiwa bado una maswali au ukipata matatizo yoyote, unaweza kuwasiliana nasi ili upate msaada.
Diana si mfanyakazi wa Airbnb wala hafanyi kazi chini ya mwelekezo wa Airbnb. Kama Mtengenezaji wa Mwenyeji, alishirikiana na Airbnb kuandika chini mawazo yake na kuunda video hii. Maoni yoyote, taarifa ya vidokezi au ushuhuda uliotolewa ni za kweli, ni zake mwenyewe, na si taarifa rasmi za Airbnb.
Vidokezi
Kuwa na taarifa za mawasiliano za fundi bomba, fundi umeme na Mwenyeji Mwenza karibu ili iwe rahisi kutatua matatizo
Matengenezo ya kawaida husaidia kuweka sehemu yako katika hali nzuri
Mawasiliano yaliyo wazi na kuelewa watu kunaweza kukusaidia kuzuia na kudhibiti changamoto