Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Vidokezi vya kuokoa nishati ambavyo vinaweza kupunguza bili zako za huduma za umma

Mabadiliko madogo yanaweza kukuwezesha uokoe pesa nyingi na kupunguza upotevu.
Na Airbnb tarehe 14 Des 2022
Inachukua dakika 4 kusoma
Imesasishwa tarehe 14 Des 2022

Vidokezi

  • Zuia uingiaji wa hewa baridi na uweke mabomba yanayomimina maji machache

  • Badilisha vifaa vikubwa na uondoe plagi za vifaa vidogo kwenye soketi

  • Waeleze wageni jitihada zako za uendelevu

Huku bei za nishati zikipanda, kufanya sehemu yako iwe yenye starehe kwa wageni kunaweza kugharimu pesa nyingi. Kama Mwenyeji, unaweza kuwaomba wageni wazingatie jinsi wanavyotumia vifaa vya kupasha joto, kupoza na kutumia maji, lakini hupaswi kuwategemea wapunguze bili zako za huduma za umma. Kuchukua hatua za kutotumia umeme mwingi kwenye sehemu yako ni suluhisho bora. Hii inaweza kusababisha uokoaji wa pesa nyingi na kusaidia kulinda sayari.

Airbnb inashirikiana na wataalamu wa uendelevu ili kuwapa Wenyeji ushauri na nyenzo za kufanya mabadiliko kwenye nyumba zao. Ili kuanza, jaribu vidokezi hivi kutoka Energy Saving Trust, shirika la Uingereza ambalo linajishughulisha na kuwasaidia watu kupunguza matumizi yao ya nishati na uzalishaji wa gesi chafu.

Zuia uingiaji wa hewa baridi na uweke mabomba yanayomimina maji machache

Wageni kwa kawaida hutarajia sehemu ambayo wanaweza kupata joto au baridi, pamoja na upatikanaji wa maji moto. Unaweza kukidhi mahitaji yao na kupunguza gharama zako za uendeshaji, kwa kuboresha uhifadhi wa joto na kutotumia maji mengi kwenye nyumba yako.

  • Kuziba mianya inayopenyeza hewa baridi kwenye madirisha, milango, dohani, mapengo karibu mabomba na soketi ili kuzuia uvujaji wa hewa ni njia ya bei nafuu na nzuri ya kuokoa nishati katika aina yoyote ya nyumba. Utando wa kuhifadhi joto, kalafati, gasketi za povu, luva zinazotelezeshwa na mapazia mazito au mapazia mepesi yote yanaweza kusaidia kuzuia uvujaji.
  • Kufunika vifaa vya kupasha maji joto vya zamani ili kuhifadhi joto na kuweka kipima muda ili kuepuka kupasha maji joto wakati sehemu yako haikaliwi kunaweza kusaidia kuhifadhi nishati.
  • Kubadilisha mabomba ya kawaida na vali za vyoo, mifereji na mabomba ya mvua yanayomimina maji machache kunaweza kusaidia kupunguza matumizi ya maji. Mabomba ya mvua yenye hewa ya kutosha huchanganya hewa ndani ya maji ili kudumisha shinikizo kubwa huku yakipunguza matumizi ya maji kwa hadi galoni 4.25 (lita 16) kila unapooga. Ukiwa hapo, angalia mara kwa mara na urekebishe uvujaji wowote wa maji ili uzuie upotevu.
  • Kusafisha vifaa vilivyojaa pekee katika mashine ya kuosha vyombo na mashine ya kuosha/kukausha, ikiwa imewekwa katika hali-joto ya chini au hali-tumizi ya "kutunza mazingira" kunaweza kuokoa maji na umeme. Wakati wa kuandaa sehemu yako kwa ajili ya mgeni anayefuata, weka vyombo nje na uanike mashuka ili yakauke kwa hewa inapowezekana.

Anna, Mwenyeji Bingwa na mshiriki wa Bodi ya Ushauri ya Wenyeji huko Newgale, Wales, hutumia mapambo ya kuhifadhi joto ili kusaidia kuweka nyumba zake za shambani zikiwa za starehe kwa ajili ya wageni. "Tumeweka mazulia madogo kwenye sakafu za zamani za mawe bapa na mapazia mazuri mazito ambayo yanazuia kuingia kwa hewa baridi," anasema Anna, ambaye anahudumu kwenye kamati ya uendelevu ya bodi. “Yote yanapamba vyumba vyetu na yanatusaidia kuokoa nishati.

Badilisha vifaa vikubwa na uondoe plagi za vifaa vidogo kwenye soketi

Wageni wengi wanataka vistawishi kama vile jiko lenye vifaa vya kutosha na Wi-Fi ya kuaminika. Unaweza kupunguza matumizi yako ya umeme bila kuathiri ukarimu wako.

  • Kubadilisha balbu za taa kutoka zinazotoa nuru zikiwa na joto na za halojeni kwenda balbu za LED kunaweza kukuokoa kutoka USD4 hadi USD16 kwa kila balbu kila mwaka.
  • Kuweka vihisio na vidhibiti vya taa, ambavyo ni vya bei ya chini na rahisi kuweka, kunaweza kusaidia kuhakikisha kwamba taa haziachwi zikiwa zimewaka bila kukusudia. Vihisio vya mwendo vinaweza kuokoa umeme kwa kuwasha na kuzima taa kiotomatiki vinapohisi uwepo wa mgeni.
  • Kubadilisha vifaa vikubwa kadiri muda wake wa matumizi unavyokwisha na vile visivyotumia umeme mwingi, kunaweza kuhifadhi umeme. Kuchagua friji yenye ukadiriaji wa juu kunaweza kuwa na athari kubwa kwenye bili zako za nishati katika maisha ya kawaida ya bidhaa hiyo.
  • Kuondoa plagi za vifaa vidogo kwenye soketi, ikiwemo chaja za simu, wakati hazitumiki kunaweza kuzuia umeme usitumike. Njia nyingine ni kuziunganisha kwenye kifaa chenye soketi nyingi au swichi mahiri ambayo unaweza kuzima ukiwa mbali wakati sehemu yako haikaliwi. Kuondoa vifaa mbalimbali kutoka kuwa daima katika hali ya sinzia ange kunaweza kukusaidia kuokoa karibu asilimia 5 kwenye bili yako ya umeme ya kila mwezi.
"Kuna vitu vingi ambavyo vinahusika katika kufanya usafi na kuosha," Anna anasema. "Kutumia mashine ya kuosha na kukausha yenye ukadiriaji wa juu ni muhimu sana kwangu katika kutotumia umeme mwingi."

Simulia kisa chako kwa wageni

Kisa unachosimulia katika maelezo ya tangazo lako kinaweza kuunga mkono jitihada zako za uhifadhi na kuathiri huduma ambayo wageni wako watapata.

"Nadhani kinacholeta tofauti kwetu ni kueleza ‘maadili yetu ya kutunza mazingira‘ waziwazi katika nyumba yetu," Anna anasema. “Unaweza kuelezea jinsi unavyothamini uendelevu na mambo unayofanya, kisha ulinganishe kwa usahihi na wageni wanaojali mazingira kama wewe.”

Mawasiliano ya wazi pia yanawahimiza wageni wafuatilie mwongozo wako. "Kwa kweli, tunataka wageni wawe na ukaaji mzuri, wenye starehe," Anna anasema. “Lakini kuweka matarajio katika tangazo letu kuhusu jinsi tunavyojaribu kuhifadhi nishati husaidia kuzuia tabia isiyofaa, kama vile kuongeza joto kisha kuondoka siku nzima.”

Hizi ni hatua chache ndogo ambazo unaweza kuchukua ili usitumie umeme mwingi kwenye sehemu yako. Hatua kubwa, kama vile kuweka paneli zinazonasa nishati ya jua, kubadilisha madirisha na kuboresha uhifadhi wa joto, zinaweza kukusaidia kuhifadhi hata zaidi. Mabadiliko unayoyafanya yanaweza kustahiki mapunguzo, makato ya kodi na vifuta jasho vingine.

Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha wageni kwa njia endelevu

Vidokezi

  • Zuia uingiaji wa hewa baridi na uweke mabomba yanayomimina maji machache

  • Badilisha vifaa vikubwa na uondoe plagi za vifaa vidogo kwenye soketi

  • Waeleze wageni jitihada zako za uendelevu

Airbnb
14 Des 2022
Ilikuwa na manufaa?