Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kwa nini ujitahidi kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa

  Jifunze kuhusu faida za mpango na ujue jinsi ya kustahiki.
  Na Airbnb tarehe 21 Nov 2019
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 13 Mei 2021

  Vidokezi

  • Wenyeji Bingwa ni wenyeji walio na ukadiriaji wa juu na wenye uzoefu mkubwa kwenye Airbnb

  • Wenyeji Bingwa wanaweza kuwekewa nafasi zaidi, mapato zaidi na marupurupu mengine ya mpango

  • Unavyopaswa kuwa navyo: ukadiriaji wa jumla wa 4.8+, sehemu za kukaa zaidi ya 10 au usiku 100,

  • Angalia jinsi ulivyokaribia kwenye kichupo chaFursa cha wasifu wako

  • Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kuwezesha ukaribishaji wako wa wageni kwenda ngazi ya juu

  Je, wewe hutoa ukarimu wa hali ya juu? Je, wewe huwajibu wageni haraka kabisa? Je, unapata tathmini nzuri? Unaweza kustahiki kuwa Mwenyeji Bingwa! “Nilipoanza kukaribisha wageni miezi 10 iliyopita, nilijifikiria kama mgeni na jinsi ambavyo ningependa kutendewa,” anasema Mwenyeji Bingwa Terry kutoka Toronto. "Nilipata mafanikio." Endelea kusoma ili ujue maana ya kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa inayotamaniwa sana.

  Karibuni nyote bila kukosa (wenyeji)

  Mpango wa Mwenyeji Bingwa wa Airbnb huenzi na kuwazawadi wenyeji wa Airbnb walio maarufu na wenye uzoefu zaidi. Haijalishi aina ya sehemu uliyo nayo—kuanzia chumba sahili cha ziada hadi majengo makubwa—mwenyeji yeyote anaweza kuwa Mwenyeji Bingwa kwa kutoa kwa kawaida ukarimu wa hali ya juu kabisa.

  Wenyeji Bingwa, manufaa makubwa

  Unapokuwa Mwenyeji Bingwa, unazawadiwa beji maalumu kwenye wasifu wako na tangazo. Wenyeji Mabingwa wana fursa ya:

   • Pata fedha ya ziada
    Wenyeji Bingwa kwa kawaida hunufaika kutokana na ongezeko kubwa la mapato. Kuonekana zaidi na kuaminiwa na wageni kunaweza kukupatia pesa zaidi.
   • Wavutie wageni zaidi
    Beji inaweza kufanya tangazo lako liwavutie zaidi wageni—watajua kuwa wewe ni mwenyeji mzoefu unayejulikana kwa ukarimu mkubwa. Wageni wanaweza hata kuchuja matokeo yao ya utafutaji ili kuonyesha tu matangazo yenye hadhi ya Mwenyeji Bingwa.
   • Pata ufikiaji wa zawadi za kipekee
    Utapata asilimia 20 ya ziada pamoja na bonasi ya kawaida utakapowaalika wenyeji wapya. Na baada ya robo 4 mfululizo kama Mwenyeji Bingwa, utapokea kuponi ya kusafiri.

   Manufaa ya mpango huweza kutofautiana kulingana na soko na nchi.

   Nilipoanza kukaribisha wageni, nilijifikiria kama mgeni na jinsi ambavyo ningependa nitendewe. Nilipata mafanikio.
   Terry,
   Toronto

   Mambo 4 unayopaswa kuwa nayo ili uwe Mwenyeji Bingwa

   Je, unajiuliza ikiwa unakidhi matakwa? Wenyeji Bingwa ni lazima wakidhi vigezo vifuatavyo ili kustahiki—na kudumisha—hadhi yao maalumu:

   1. Dumisha ukadiriaji wa juu wa jumla
   Lazima uwe na wastani wa jumla wa ukadiriaji wa 4.8 au zaidi kulingana na tathmini kutoka kwa wageni wako wa Airbnb katika mwaka uliopita. Wageni wanajua wanaweza kutarajia ukarimu bora kutoka kwa wenyeji hawa.

   2. Uwe na uzoefu
   Lazima uwe umekaribisha wageni kwenye angalau ukaaji 10 katika mwaka uliopita, au ikiwa unakaribisha wageni kwenye sehemu za kukaa za muda mrefu, usiku 100 kwa angalau sehemu 3 za kukaa. Wageni wako watajisikia kuwa na uhakika wanapokaa kwa mwenyeji mwenye uzoefu.

   3. Epuka kughairi
   Lazima uwe umeghairi chini ya asilimia 1 ya nafasi zilizowekwa, bila kujumuisha sababu zisizozuilika. Hii inamaanisha kughairi 0 ikiwa una nafasi zilizowekwa zilizo chini ya idadi ya 100 kwa mwaka. Kughairi nadra kunamaanisha utulivu wa akili kwa wageni.

   4. Toa majibu
   Lazima uwe umejibu asilimia 90 ya ujumbe mpya unaohusiana na nafasi zilizowekwa ndani ya saa 24. Wageni wanapokuuliza maswali, wanajua watapata jibu la haraka.

   Fuzu kila baada ya miezi 3

   Mara nne kwa mwaka, utakuwa na fursa ya kustahiki kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa. Airbnb huwakagua wenyeji wote kila baada ya miezi mitatu kulingana na siku 365 zilizopita za kukaribisha wageni. Ikiwa wenyeji wana maeneo ya kuboresha, wanahitaji kukidhi mahitaji yote kwa tathmini inayofuata ili kupata au kuweka hadhi yao ya Mwenyeji Bingwa.

   Vidokezi

   • Wenyeji Bingwa ni wenyeji walio na ukadiriaji wa juu na wenye uzoefu mkubwa kwenye Airbnb

   • Wenyeji Bingwa wanaweza kuwekewa nafasi zaidi, mapato zaidi na marupurupu mengine ya mpango

   • Unavyopaswa kuwa navyo: ukadiriaji wa jumla wa 4.8+, sehemu za kukaa zaidi ya 10 au usiku 100,

   • Angalia jinsi ulivyokaribia kwenye kichupo chaFursa cha wasifu wako

   • Gundua zaidi katika mwongozo wetu kamili wa kuwezesha ukaribishaji wako wa wageni kwenda ngazi ya juu
   Airbnb
   21 Nov 2019
   Ilikuwa na manufaa?