Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Tunakuletea Huduma kwenye Airbnb

Wageni sasa wanaweza kuweka nafasi ya mpishi bora, mkufunzi, usingaji na kadhalika kwenye sehemu yako ya Airbnb.
Na Airbnb tarehe 13 Mei 2025
Imesasishwa tarehe 13 Mei 2025

Mara nyingi watu huchagua hoteli kwa sababu ya huduma wanazotoa, kama vile huduma ya chumba, ufikiaji wa chumba cha mazoezi au miadi kwenye spa. Kuanzia leo, wageni wanaweza kupata huduma moja kwa moja kwenye Airbnb yako.

Huduma kwenye Airbnb ni nini?

Huduma za Airbnb ni huduma bora za kufanya ukaaji uwe maalumu zaidi. Tunazindua aina 10 katika miji mahususi, huku huduma zinazotolewa na maeneo mapya yakiwekwa mara kwa mara kwenye programu ya Airbnb.

  • Wapishi: Milo inayoandaliwa kwenye nyumba inayoweza kufanywa kuwa mahususi kikamilifu kutoka kwa wapishi wataalamu.
  • Upigaji picha: Vipindi vya kupiga picha mahususi kutoka kwa wapiga picha wazoefu.
  • Usingaji: Usingaji wa kurejesha usawa wa mwili ikiwemo usingaji wa Kiswidi, usingaji wa kina kwenye nyama na usingaji wa kupunguza mkazo kutoka kwa wataalamu wazoefu.
  • Huduma za spa: Utunzaji wa uso, mikwaruzo midogo kwenye ngozi, skrabu za mwili na huduma nyinginezo, zinazotolewa na wataalamu wa urembo wa uso.
  • Mazoezi ya viungo kwa mtu binafsi: Yoga, mazoezi ya viungo ya kuimarisha nguvu, HIIT na kadhalika, yanayotolewa na wakufunzi wa mazoezi ya viungo, ikiwemo wataalamu maarufu wa mazoezi ya viungo na wanariadha wa mashindano ya dunia.
  • Mitindo ya nywele: Unyoaji wa nywele wa kitaalamu, mitindo ya ukaushaji nywele na kadhalika kutoka kwa wanamitindo wazoefu.
  • Upodoaji: Upodoaji kwa ajili ya kila siku au matukio maalumu kutoka kwa wapodoaji bingwa wataalamu.
  • Huduma za kucha: Utunzaji wa kucha za mikono na miguu kutoka kwa wataalamu wazoefu wa kucha.
  • Vyakula vilivyoandaliwa: Vyakula vilivyo tayari kuliwa vilivyoandaliwa na wapishi wataalamu.
  • Kuandaa chakula: Huduma kamili ya kuandaa chakula yenye menyu mahususi, mapambo na vifaa, pamoja na mpangilio na kufanya usafi.

Huduma za Airbnb zinakaguliwa kwa ajili ya ubora, kwa kuzingatia vigezo kama vile maarifa, elimu, sifa na kadhalika. Wenyeji wa huduma wana uzoefu wa miaka mingi na wamekamilisha mchakato wa uthibitishaji wa utambulisho wa Airbnb. Wengi ni maarufu katika uwanja wao, ikiwemo wapishi kutoka migahawa yenye nyota ya Michelin, wapiga picha walioshinda tuzo na wakufunzi bingwa.

Wageni wanaweza kuvinjari huduma kwa urahisi mahali zinapopatikana na kuweka nafasi papo hapo kwenye Airbnb. Huduma zinaweza kufanyika kwenye nyumba, biashara ya mwenyeji wa huduma au sehemu ya umma.

Kuruhusu huduma kwenye nyumba yako

Huduma zinaruhusiwa kiotomatiki kwenye nyumba yako. Hii ni njia moja ya kuwaonyesha wageni kwamba umewekeza katika kufanya ukaaji wao uwe wa kipekee zaidi.

Unaweza kuamua kutoruhusu huduma kwenye nyumba yako. Wasiliana na Airbnb Usaidizi ili kubainisha huduma zozote ambazo huruhusu na watasasisha sheria za nyumba yako.

Wageni hutathmini huduma kando na ukaaji wao na wewe. Wanakumbushwa kutathmini huduma mara tu inapoisha. Wageni wanaombwa kutoa ukadiriaji wa jumla, ukadiriaji wa kina, tathmini ya umma na ujumbe wa faragha kwa ajili ya huduma. Tathmini yao haiathiri ukadiriaji au uorodheshaji wa nyumba yako.

Kuelewa bima kwa ajili ya wenyeji wa huduma

Wenyeji wote wa huduma wanahitajika kudumisha bima ya dhima inayofaa kwa biashara yao wanapotoa huduma. Pia wanalindwa na bima ya dhima ya Matukio na Huduma ya Airbnb, ambayo ni sehemu ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji. Hii ni sawa na jinsi unavyolindwa na bima ya dhima ya mwenyeji kupitia AirCover kwa ajili ya Wenyeji.

Huduma inapofanyika kwenye nyumba yako, bima ya dhima ya Matukio na Huduma inatumika ikiwa mwenyeji wa huduma anawajibika kwa uharibifu wa nyumba au mali yako.

Kupendekeza huduma

Kushiriki mapendekezo kunaweza kufanya iwe rahisi kwa wageni wako kupata huduma bora. Hivi ndivyo unavyoweza kupendekeza huduma.

  • Angalia kile kinachotolewa karibu: Vinjari Airbnb kwa ajili ya huduma zinazopatikana katika eneo hilo. Ungana na wenyeji wa huduma ili upate maelezo zaidi au uweke nafasi ya huduma zinazotolewa ili ujaribu mwenyewe.
  • Unda jibu la haraka: Tuma ujumbe ulioandikwa mapema kiotomatiki wakati wageni wanaweka nafasi kwenye nyumba yako au kama jibu ikiwa wataomba mapendekezo.

Kumwalika mwenyeji wa huduma

Unamjua mtu anayeweza kuandaa huduma bora? Shiriki kiungo chako cha mwaliko na unaweza kujipatia USD 100 (au sarafu sawa ya nchi husika) anapoanza kukaribisha wageni.*

Wenyeji unaowaalika wana siku 180 za kukamilisha nafasi ya kwanza wanayowekewa. Unaweza kufuatilia iwapo wamechapisha tangazo au wamewekewa nafasi inayokaribia kwenye ukurasa wako wa waalikwa.

Tutatuma zawadi yako moja kwa moja kwenye akaunti yako takribani siku 14 baada ya mwenyeji anayestahiki uliyemwalika kukamilisha nafasi iliyowekwa inayostahiki.

Maswali na Majibu ya Huduma kwenye Airbnb

*Zawadi za mwaliko zinapatikana tu katika maeneo yanayostahiki na zinadhibitiwa na Ofa ya Mwaliko wa Mwenyeji na Masharti ya Mpango. Kipindi cha siku 180 huanza wakati mwenyeji anaunda tangazo jipya kwa kutumia kiungo chako cha mwaliko. Matangazo yaliyoanza kutumia kiungo chako cha mwaliko kabla ya tarehe 17 Machi, 2025, yanadhibitiwa na masharti yaliyotumika wakati mialiko hiyo ilifanywa.

Huduma hazipatikani katika maeneo yote, ikiwemo Brazili na Puerto Rico.

Bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio na Huduma hutolewa na watoa bima wengine. Ikiwa unakaribisha wageni kwenye nyumba, matukio au huduma nchini Uingereza, bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio na Huduma zinadhaminiwa na Zurich Insurance Company Ltd. na kupangwa na kukamilishwa bila gharama ya ziada kwa Wenyeji wa Uingereza na Airbnb UK Services Limited, kampuni iliyoteuliwa kuwakilisha Aon UK Limited, ambayo imeidhinishwa na kudhibitiwa na Financial Conduct Authority. Nambari ya rajisi ya Aon katika FCA ni 310451. Unaweza kuangalia maelezo haya kwa kutembelea Rajisi ya Huduma za Fedha au kuwasiliana na FCA kupitia 0800 111 6768. Bima ya dhima ya Mwenyeji na bima ya dhima ya Matukio na Huduma ndani ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji zinadhibitiwa na Financial Conduct Authority, bidhaa na huduma zilizosalia si bidhaa zinazodhibitiwa zilizopangwa na Airbnb UK Services Limited. Angalia maelezo na vighairi. FPAIR202525SD

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
13 Mei 2025
Ilikuwa na manufaa?