Kinachohitajika ili kuandaa Huduma kwenye Airbnb
Huduma kwenye Airbnb ni huduma bora za kufanya ukaaji wa mgeni uwe maalumu zaidi. Aina za huduma zinajumuisha wapishi, upigaji picha, usingaji, huduma za spa, mazoezi ya viungo kwa mtu binafsi, mitindo ya nywele, upodoaji, huduma za kucha, vyakula vilivyoandaliwa na kuandaa chakula.
Huduma zinakaguliwa kwa ajili ya ubora na wenyeji na matangazo yanatarajiwa kukidhi viwango na matakwa yetu. Haya ni baadhi ya mambo muhimu unayopaswa kujua.
Viwango vya msingi
- Uthibitishaji wa utambulisho: Thibitisha utambulisho wako na inapofaa, pita uchunguzi wa rekodi ya uhalifu na ukaguzi mwingine.
- Leseni na vyeti: Dumisha leseni, bima na vyeti halali vinavyohusiana na huduma yako. Toa uthibitisho unapohitajika.
- Uzoefu: Uwe na uzoefu usiopungua miaka 2 katika fani husika au miaka 5 kwa wapishi wasio na shahada ya upishi. Tunaweza kuthibitisha elimu, historia ya ajira au tuzo na utambuzi unaoweka kwenye tangazo lako.
- Sifa: Dumisha sifa ya hali ya juu, kama inavyoonekana katika mambo kama vile maoni bora ya wageni, kwa kuzingatia zaidi tuzo na vipengele katika machapisho au aina nyingine za utambuzi.
- Potifolio: Shiriki picha zinazoonyesha uzoefu wako wa kazi unapounda tangazo lako.* Chagua picha zinazoonyesha mchakato wako na maandalizi, zana au vifaa na eneo la biashara ikiwa unapanga kuwakaribisha wageni.
Viwango vya tangazo
- Picha: Wasilisha angalau picha 5 zenye ubora wa juu, ikiwemo picha moja kwa kila huduma inayotolewa, inayotoa mawazo dhahiri, yenye uhalisia kuhusu huduma unayotoa.* Ikiwa wewe ni mpiga picha, lazima uwasilishe angalau picha 15.
- Kichwa: Eleza huduma ni gani na ni nani anayeitoa. Anza kwa maneno machache yenye maelezo na ujumuishe jina lako la kwanza mwishoni.
- Utaalamu: Eleza kwa nini unastahiki kipekee kukaribisha wageni kwenye huduma yako. Eleza moja kwa moja, toa maelezo mafupi na mahususi.
- Huduma zinazotolewa: Weka huduma zisizopungua 3 zilizo na bei mbalimbali, ya kuingia, ya kawaida na ya juu, kwa kila tangazo. Angazia maelezo mahususi kama vile viambato, mbinu, vifaa au nyenzo katika maelezo yako, ili wageni wajue wanachonunua.
Uwasilishaji wa huduma na mabadiliko yaliyofanywa kwenye matangazo yaliyoidhinishwa yatatathminiwa.
Matakwa ya kukaribisha wageni
- Nafasi zilizowekwa: Heshimu nafasi zilizowekwa na wageni na uepuke kughairi kwa sababu zinazoweza kuzuilika.
- Tangazo: Dumisha tangazo sahihi, ikiwemo eneo, mahitaji ya mgeni na muda wa kuanza na kumaliza huduma.
- Kutuma ujumbe: Wasiliana na wageni kwa wakati unaofaa. Wajulishe wageni ikiwa unamleta mtu wa kukusaidia wakati wa huduma, ukiwapa ilani ya kutosha ya kughairi bila ada.
- Usalama: Toa mafunzo na maelekezo sahihi ili kuzuia majeraha, toa vifaa safi na uwe na mpango wa kukabiliana na dharura. Weka sharti la umri unaofaa wa mgeni kwa ajili ya huduma unazotoa kama inavyohitajika.
- Eneo: Heshimu eneo unalotoa huduma. Usiharibu mali na ufanye usafi ukimaliza.
Mchakato wa ukaguzi unaendelea. Mbali na kile kilichoainishwa hapo juu, unahitaji pia kuzingatia Masharti ya Huduma ya Airbnb na Sheria za Msingi za Mwenyeji na Sera za Usalama za Kukaribisha Wageni.
Matangazo au akaunti za wenyeji ambao hawakidhi viwango na matakwa yetu zinaweza kusimamishwa au kuondolewa. Soma viwango na matakwa kamili ya Matukio ya Airbnb.
*Ikiwa unatoa huduma ya usingaji au spa, hutahitaji kuwasilisha picha kwa ajili ya tangazo lako. Tutakuchagulia picha kutoka kwenye maktaba ya picha za kitaalamu zinazoonyesha huduma hizi.
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.