Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.

Jinsi ya kuchagua na kuweka picha zenye ubora wa juu

Toa uanuwai, ifanye iwe rahisi na uonyeshe jambo la ajabu.
Na Airbnb tarehe 13 Mei 2025
Imesasishwa tarehe 13 Mei 2025

Picha husaidia kuvutia wageni wanapotafuta kwenye Airbnb. Picha zako zinapaswa kutoa wazo dhahiri na sahihi la huduma yako na kuwahamasisha wageni waweke nafasi.

Kuzingatia ubora

Kila picha unayoshiriki inapaswa kuwa yenye ubora wa juu. Kila picha inapaswa kuwa na udhahiri wa angalau pikseli 800 x 1,200 na ukubwa wa faili wa hadi megabaiti 10.

Wasilisha picha ambazo:

  • Umezipiga au umetumia kwa ruhusa
  • Zina mwanga wa kutosha, ikiwezekana kwa mwanga wa asili
  • Ni rahisi katika utungaji na mandharinyuma
  • Zimelengwa, huku kitu kinacholengwa kikiwa katikati
  • Ni mchanganyiko wa maelezo ya karibu na utungaji mpana

Usiwasilishe picha ambazo:

  • Ni picha dhahania au zilizovutwa karibu kupita kiasi
  • Zina mparaganyo au zina shughuli nyingi
  • Ni nyeusi au zinazotumia mmweko mkali
  • Kolaji
  • Ni matoleo mengi ya picha sawa
  • Ni nembo au chapa

Ikiwa picha zako zozote zinaonyesha uso wa mtu, hakikisha una ruhusa yake ya kuitumia.

Kuweka picha nzuri

Picha zinaonyeshwa katika maeneo 3 kwenye matangazo ya huduma: kama picha ya jalada, katika orodha ya huduma unazotoa na katika matunzio ya picha.

Wasilisha angalau jumla ya picha 5, ikiwemo moja kwa kila huduma inayotolewa. Ikiwa unatoa huduma ya kupiga picha, chagua angalau picha 15 za kuwakilisha potifolio yako.

Tutatathmini picha unazoweka na kuidhinisha picha zinazofikia viwango vyetu. Haya ndiyo mambo unayopaswa kuwasilisha kwa kila sehemu.

Chagua picha ya jalada ambayo inaonyeshwa vizuri zaidi katika mkao wa mlalo, yenye nafasi ya kupunguza pande zote.

Picha ya jalada. Picha hii inaonekana kwenye sehemu ya juu ya tangazo lako na inapaswa kuwasaidia wageni kuelewa huduma unayotoa. Picha yenye mafanikio ni:

  • Ya mlalo
  • Rahisi na haina mparaganyo
  • Iko katikati, yenye nafasi ya kupunguza pande zote

Epuka picha zilizo na mandharinyuma nyeupe au picha za karibu za nyuso za watu.

Weka picha tofauti na rahisi ambayo inawakilisha kwa usahihi kila moja ya huduma unazotoa.

Huduma unazotoa. Huduma zinazotolewa ndizo ambazo wageni watawekea nafasi, zifikirie kama karatasi yako ya bei au menyu. Weka picha moja tofauti ambayo inawakilisha kwa usahihi kila moja ya huduma unazotoa. Picha hizi ni ndogo, kwa hivyo chagua mandhari rahisi ambazo ni rahisi kuelewa. Picha zenye nguvu:

  • Zinazingatia kipengele kimoja, zikiwa na mandharinyuma safi
  • Zina utungaji sawa

Matunzio ya picha. Hii ni fursa ya kuonyesha wageni watarajiwa si tu kile unachotoa, bali pia wewe ni nani. Wageni wanaweza kuona picha zote unazoshiriki katika matunzio ya picha. Chagua picha zinazoonyesha:

  • Mchakato na maandalizi yako
  • Zana, vifaa au viambato unavyotumia
  • Eneo la biashara yako, ikiwa unapanga kuwakaribisha wageni
  • Matokeo ya huduma yako, kama vile wageni kufurahia mlo wao

Hakikisha una ruhusa ya kutumia picha zozote unazowasilisha na kwamba picha hizo zinaonyesha huduma yako kwa usahihi.

Wenyeji wote, picha na maelezo ya tangazo lazima yakidhi viwango na matakwa ya Huduma kwenye Airbnb.

Ikiwa unatoa huduma ya usingaji au spa, hutahitaji kuwasilisha picha kwa ajili ya tangazo lako. Tutakuchagulia picha kutoka kwenye maktaba ya picha za kitaalamu zinazoonyesha huduma hizi.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
13 Mei 2025
Ilikuwa na manufaa?