Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Maelezo ya kina ambayo wageni wanapenda

  Jumuisha kipengele chenye kuvutia kwa kuongeza vistawishi vyako.
  Na Airbnb tarehe 11 Des 2019
  Inachukua dakika 4 kusoma
  Imesasishwa tarehe 13 Mei 2021

  Vidokezi

  • Tafuta njia za kuboresha vistawishi vyako

  • Maamkizi zingativu, kama kikapu cha kukaribisha au barua fupi liyoandikwa kwa mkono, ni ya muhimu sana

  • Shiriki vyakula vitamu vya eneo husika ili kuwapa wageni uzoefu wa kipekee

  • Vistawishi vinavyofaa, kama vile mafuta ya kuzuia miale ya jua, dawa ya kufukuza wadudu na miavuli, vinaweza kusuluhisha matatizo mbalimbali

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuunda sehemu inayofaa wageni

  Unataka kuunda uzoefu wa kukumbukwa kwa ajili ya wageni wako? Sio lazima kuwa na sehemu ya kifahari sana au vistawishi vya hali ya juu. Badala yake, fikiria ishara ndogo ambazo zinaweza kuwa na matokeo makubwa, kama vile kutoa kahawa yako uipendayo ya ndani ya nchi au maelezo ya ukaribisho yaliyoandikwa kwa mkono. Hapa, wenyeji wanashiriki maoni rahisi, yanayofaa kwa bajeti ili kuwapa wageni ukaaji wa kukumbukwa.

  Njia tamu zaidi ya kusalimiana

  Wageni mara nyingi hufika wakiwa wamechoka na kuchanganyikiwa kidogo. Wafanye wahisi kukaribishwa wakati wanaingia.

  • Andaa kikapu cha kukaribisha. "Nina kikapu cha kukaribisha kilicho na unga wa shayiri wa papo hapo, PowerBars, karanga, biskuti na bisi ya kujiandalia papo hapo ya kuwatosheleza iwapo wamesafiri safari ndefu kwa ndege na hawataweza kufanya ununuzi mara moja." —Carrie, Jiji la New York
  • Andika maelezo mahususi. “Mojawapo ya vitu ambavyo wageni wanapenda ni kadi iliyo na ujumbe mahususi. Ninatumia kadi iliyotengenezwa na wabunifu chipukizi ambao mada yake ni jiji langu, São Paulo.” —Priscilla na Gabriel, São Paulo
  • Toa sehemu ya wao kuweka masanduku yao. “Nina uchaga wa kuweka mizigo kwenye sehemu ya mwisho ya mguuni mwa kila kitanda. Ninaupenda kwa kuwa ni rahisi kuondoa iwapo mtu anataka nafasi ya ziada au ninapofanya usafi.” —Allison, Traverse City, Michigan

  Hakikisha kitanda na bafu lako vinalingana

  Mara baada ya kuweka vistawishi muhimu vya kutosha, vitumie kama kichocheo cha ukarimu bora zaidi.

  • Weka vifaa vya ziada mahali panapofikika. "Ninahakikisha kuna taulo nyingi, matandiko ya ziada, sabuni na shampuu." —Susan, Covington, Georgia
  • Toa vifaa vya usafi wa mwili ambavyo ni vyema kuwa navyo. "Ninawapa wageni vifutio vya kitaalamu vya kuondoa vipodozi usoni." -Beverlee na Suzie, Oakland, California (Bonasi: Pia vitakusaidia kuepusha madoa ambayo ni magumu kuondoa kwenye mashuka na taulo zako!)
  • Boresha bafu lako. “Ninakunja upande wa chini ya karatasi ya choo. Ni jambo dogo, lakini linahisi kuwa zuri na linaonyesha kuwa unajali.” —Emma-Kate, San Francisco
  • Fanya iwe ya kifahari. “Ninatoa majoho meupe yenye starehe yaliyotengenezwa kwa pamba. Wageni huyatumia wanapokuwa kwenye spa au wanapopumzika.” —Linda, La Quinta, California
  Nina kikapu cha ukaribisho kikiwa na oatmeal ya papo hapo, PowerBars, karanga, biskuti, na bisi ya kujiandalia papo hapo.
  Carrie,
  Jiji la New York

  Yote kuhusu ladha hiyo ya eneo husika

  Sehemu ya furaha ya kusafiri ni kugundua ladha tofauti, harufu, vituko, na manhdari ya mahali uendako. Shiriki na wageni baadhi ya mambo yako uyapendayo.

  • Fanya kiamsha kinywa kiwe cha kukumbukwa. "Ninatoa zawadi ndogo inayotoka eneo husika kwa ajili ya kiamsha kinywa, kulingana na msimu—asali maalumu na nadra ya msonobari kutoka kwa wakulima wa milimani, jibini iliyotengenezwa kienyeji au sharubati na matunda kutoka kwa wakulima wa vijiji vya karibu." —Claudia, Black Forest, Ujerumani
  • Fikiria kwa ujumla. "Niko Portland, kwa hivyo nataka wageni wapate hisia ya Portland katika vipengele vyote vya uzoefu wa wageni. Hiyo ndiyo maana ya Airbnb! Ninatoa pombe zilizotengenezwa kienyeji, maua kutoka kwenye bustani yangu, vitabu vingi kuhusu jiji, maduka ya vitafunio vya kienyeji na gazeti la Oregon linafika kila siku. Vilevile ninanunua majarida ya eneo husika. Kahawa nzuri ya Portland ni muhimu na mchanganyiko wa maziwa na malai vilevile.” -Lisa, Portland, Oregon
  • Fanya uzoefu ufae hali fulani. "Ikiwa wageni wangu wanasherehekea siku ya kuzaliwa wikendi, nitaacha keki ndogo zilizotengenezwa kienyeji." —Tiffany, Hollywood Beach, California
  • Wape kitu kidogo cha ukumbusho. "Mimi naweka kadi ya posta kutoka kwenye eneo la kuandaa hafla linalopendeza au alama-ardhi katika eneo husika ambayo mgeni anaweza kuweka au kutuma nyumbani." -Debi, Thousand Oaks, California

  Wakati mwingine, vitendo ni bora

  Vistawishi vinavyofaa vinaweza kufanya utofauti kati ya safari nzuri na ile ya kufadhaisha ambayo haijatarajiwa. Unaweza kuokoa siku kwa mafuta ya kuzuia miale ya jua, visanduku vilivyo na vifaa vya huduma ya kwanza, adapta za kompyuta na kadhalika.

  • Wasaidie kutoka nje. “Vifaa vya ufukweni: viti, mwavuli, kanga, mpira wa raketi za mbao, friji ndogo inayobebeka, kadi, vitu vya kuchezea vya watoto na mpira wa kandanda. Vifaa vya kujikinga dhidi ya mbu: dawa na mishumaa inayotoa harufu ya limau ya kufukuza mbu." -Danielle, Rio de Janeiro
  • Zingatia hali ya hewa ya eneo husika. "Tumenunua makoti 10 ya mvua ya dharura yanayoweza kutupwa, ambayo yametengenezwa kwa plastiki nyembamba na nyepesi. Inatokea kwamba wageni huwasili wakati hali ya hewa ni nzuri na baadaye kunakuwa na mvua kubwa kabla ya wao kuondoka." —Till na Jutta, Stuttgart, Ujerumani
  • Hakikisha una kikausha nywele na pasi. "Kikausha nywele na pasi ni vifaa vya bei nafuu na kuwa navyo katika nyumba yako kunaonyesha kuwa umewazia vitu vidogo ambavyo vinaweza kusuluhisha matatizo ya mgeni." -Richard, Lenox, Massachusetts
  • Weka vistawishi vinavyofaa familia. "Jambo la msingi sana ambalo linapendwa na wengi ni: gari la zamani la kukokotwa lililo na mito kwa ajili ya kuwavuta watoto wadogo wakiwa ndani yake." —Chantal, Dinan, Ufaransa

  Je, bado hujui uanzie wapi? Kaa kwenye sehemu yako kwa usiku mmoja ili kupata uzoefu wa mgeni. Kazia umakini wako kwa maoni ya wageni wako—yatatoka kwa mitazamo anuwai na kutoa mawazo ambayo huenda usingeyafikiria peke yako. Baada ya muda, utagundua njia bora ya kuboresha tangazo lako. Uko tayari kupokea tathmini nzuri!

  Vidokezi

  • Tafuta njia za kuboresha vistawishi vyako

  • Maamkizi zingativu, kama kikapu cha kukaribisha au barua fupi liyoandikwa kwa mkono, ni ya muhimu sana

  • Shiriki vyakula vitamu vya eneo husika ili kuwapa wageni uzoefu wa kipekee

  • Vistawishi vinavyofaa, kama vile mafuta ya kuzuia miale ya jua, dawa ya kufukuza wadudu na miavuli, vinaweza kusuluhisha matatizo mbalimbali

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuunda sehemu inayofaa wageni
  Airbnb
  11 Des 2019
  Ilikuwa na manufaa?