Labda una sehemu maalumu ya kukaa, wazo zuri kwa ajili ya tukio lisilosahaulika au unataka kutoa huduma kama vile chakula cha jioni kilichoandaliwa ambacho kinaweza kufanya ukaaji wa wageni uwe maalumu zaidi. Iwe unataka kukaribisha wageni kwenye nyumba yako, tukio au kutoa huduma, unaweza kuungana na wageni kote ulimwenguni-na tuko hapa ili kukusaidia.
Hebu tuanze! Ni bure kuunda akaunti na kutangaza nyumba, tukio au huduma. Kabla ya kuanza, fahamu kanuni na viwango vyetu vya kukaribisha wageni.
Jinsi unavyokaribisha wageni ni juu yako. Unaweza kutangaza nyumba nzima au chumba cha kujitegemea-au labda sehemu nyingine ya kipekee. Unaweza kuwasalimu wageni wako kwenye eneo lako, au utoe huduma ya mgeni kuingia mwenyewe. Ili kujiandaa kwa ajili ya mafanikio, angalia mahitaji ya msingi ya Airbnb ya kukaribisha wageni.
Kuna njia tofauti za kukaribisha wageni:
Unaweza pia kutoa nyumba yako ya Airbnb bila malipo kwa kujiunga na jumuiya ya wenyeji zaidi ya 60,000 wanaotoa makazi ya dharura wakati wa shida.
Unahitaji msaada zaidi? Pata maelezo zaidi kuhusu ulimwengu wa kukaribisha wageni, kuungana na Mwenyeji Bingwa, au kujiunga na darasa la kukaribisha wageni bila malipo. Ikiwa uko tayari kukaribisha wageni, ni rahisi kuunda tangazo lako.
Matukio ya Airbnb huwaleta watu pamoja-iwe ni madarasa, ziara, matamasha au shughuli nyinginezo, kote ulimwenguni.
Ikiwa uko tayari kushiriki utaalamu fulani wa eneo husika, hakikisha tu:
Hivi ndivyo unavyoweza kujisajili ili kukaribisha wageni kwenye tukio.
Huduma za Airbnb hufanya safari ziwe za kipekee zaidi kwa wageni walio na huduma nzuri kama vile wapishi binafsi, upigaji picha, ukandaji mwili na matibabu ya spa. Huduma hukaguliwa na kufanyika katika nyumba ya Airbnb, mahali pa biashara au katika sehemu za umma.
Ikiwa unataka kutoa huduma zako, unahitaji:
Je, ungependa kutoa huduma? Unda tangazo lako.
Nyumba, matukio na huduma hutolewa kote ulimwenguni, ingawa tunatakiwa kuzingatia kanuni za kimataifa ambazo zinazuia matumizi ya tovuti yetu na wakazi wa nchi fulani au maeneo fulani. Kwa sababu hii, huduma zetu hazipatikani katika baadhi ya maeneo, kama vile Crimea, Iran, Syria na Korea Kaskazini. Pata maelezo zaidi kuhusu masuala ya kisheria na ya udhibiti kwa ajili ya kukaribisha wageni kwenye sehemu za kukaa na kukaribisha wageni kwa kuwajibika kwa ajili ya matukio kwenye Airbnb.