Ruka kwenda kwenye maudhui
Shiriki sehemu yako kwa manufaa
Jiunge na jumuiya ya wenyeji wenye ukarimu. Toa nafasi yako ya ziadabila malipo kwa watu walio na hitaji la makazi ya muda mfupi.
Shiriki sehemu yako kwa manufaa
Jiunge na jumuiya ya wenyeji wenye ukarimu. Toa nafasi yako ya ziadabila malipo kwa watu walio na hitaji la makazi ya muda mfupi.

Zaidi ya watu 50,000 wamepata makao ya muda mfupi kwa ufadhili wa wenyeji katika Open Homes.

Wawe ni wapenzi wa ndoa mpya waliopoteza nyumba yao katika moto, mgonjwa wa saratani anayehitaji kuwa karibu na utunzaji maalumu, au familia inayotoroka mgogoro katika mkoa wao wa nyumbani- Open Homes huwaruhusu wenyeji wake kutoa sehemu zao bila malipo kwa watu wanaopitia wakati mgumu.

Jinsi kukaribisha wageni hufanyika

1
Tengeneza wasifu
Tuambie kuhusu sehemu yako na kwa nini unataka kukaribisha wageni
2
Subiri ombi
Utapata ujumbe kutoka kwa mashirika yasiyo ya faida au watu wanaonusuriwa
3
Jiandae kukaribisha wageni
Mtakubaliana kuhusu tarehe na kupanga matarajio mapema

Jinsi unavyoweza kuwakaribisha wageni

Ukaaji wa kimatibabu

Shiriki nyumba yako na watu katika safari ya kupona

Wageni hawa wanahitaji sehemu ya kukaa wakati wanapokea matibabu au wanaposafiri kwa ajili ya kujiliwaza. Ukaaji huo uratibiwa na mashirika yasiyolenga faida ambayo huwasaidia wagonjwa kupata utunzaji wanaohitaji.
Makao kwa wakimbizi

Karibisha wageni wanapoanza awamu mpya katika maisha yao

Mara nyingi wageni hawa huwa wamehamia mji mpya na wanatarajia kushirikishwa kwenye jumuiya. Ukaaji huu huratibiwa na mashirika ya misaada ya wakimbizi kwa niaba ya wateja wao.
Msaada wakati wa janga

Kuwa sehemu ya mpango wa mwitiko dhidi ya majanga

Ukaaji kama huu hufanyika wakati wa matukio, kama vile moto wa misitu au kimbunga kinapoathiri jumuiya. Wageni huwa watu ambao wamehamishwa au wafanyakazi wa uokoaji wanaokuja kusaidia.

Jinsi tunavyokusaidia

Tunajua hili linaweza kuwa kama jukumu kubwa. Ndiyo sababu tunajitahidi tuwezavyo ili kutoa rasilimali na ulinzi kabla na wakati wa ukaaji.
Uchunguzi na ukaguzi wa hali ya juu
Ingawa hakuna mfumo wa uchunguzi ulio kamili, kote duniani tuna wawakilishi wa mashirika na wageni ambao huweka nafasi moja kwa moja kupitia Airbnb kwa kuzingatia kanuni, ugaidi na orodha za udhibiti.
Malipo ya kufidia uharibifu wa mali
Ijapokuwa uharibifu usiotarajiwa huwa ni nadra sana kutokea, tunaelewa kwamba unaweza kuhitaji ulinzi. Garantii ya Mwenyeji itafidia kila mwenyeji kwa uharibifu wa mali wa hadi USD 1,000,000.
Mahitaji ya wageni na uthibitishaji
Kabla ya ukaaji wowote, wafanyakazi wa shirika lisilo la faida au wanaohamishwa lazima wafungue akaunti ya Airbnb. Wataombwa kutoa maelezo kama jina lao kamili, tarehe ya kuzaliwa, picha, nambari ya simu, anwani ya barua pepe na taarifa za malipo.
Rasilimali na usaidizi wa simu saa 24
Hauko peke yako katika jambo hili. Mbali na timu ya Airbnb ya usaidizi kwa wateja ya saa 24, utaweza kufikia timu maalumu kwa maswali yoyote kuhusu uwekaji nafasi wa Open Home.

Tunaoshirikiana nao

Tumeshirikiana na mashirika yanayoaminika ili tuweze kuelewa kwa kweli jumuiya tunazozihudumia na jinsi ya kuwasaidia kwa njia bora. Mashirika hayo yasiyo ya faida hutumia Open Homes ili kupata malazi ya wateja wao na kutoa usaidizi kwa wenyeji wakati wa ukaaji.
Shirika lako lisilo la faida linataka kufanya kazi na Open Homes? Tutumie ujumbe.

Jiunge na jumuiya ambayo inataka kuchangia katika jamii kwa njia mpya, ya kibinafsi zaidi.

Una maswali?
Pata majibu kwenye Kituo chetu cha Msaada au Wasiliana nasi.
Tembelea Kituo cha Msaada