SIMULIZI ZA WENYEJI

Jinsi Uslan anavyokaribisha wageni

Uslan hukaribisha wageni jijini London ili awe sehemu ya jumuiya ya Airbnb

Ni nini kilichokupa motisha yako ya kuanza kukaribisha wageni?

Nilikuwa nimetumia Airbnb kama mgeni kwa miaka mingi, na nilifurahia kila wakati — iwe ni eneo, nyumba au mwenyeji. Nadhani hali hizo nzuri ndizo zilinipa msukumo wa kuwa mwenyeji.

Ulikuwa na wasiwasi upi kabla ya kuanza kukaribisha wageni?

Niseme ukweli? Mahali pa kuweka vitu vyangu vyote ili visiwe vizuizi! Kwa sababu nilikuwa nishawahi kuwa mgeni hapo awali, wasiwasi mwingi juu ya mtu kukaa nyumbani kwangu tayari ulikuwa ushapungua - nilijua nyumba yangu itakuwa na bima, nilijua kuna amana za usalama, na nilijua kwamba wageni wangeheshimu nyumba yangu jinsi mimi na marafiki zangu tulivyoheshimu nyumba tulizokaa.

Ni nini unachopenda zaidi kuhusu kuwa mwenyeji?

Si ustaarabu sana kusema pesa, lakini kwa kweli, ni muhimu. Kando na hilo, ninafurahia sana kukutana na wageni na kushiriki ufahamu wangu wa eneo langu. Mimi ni mzaliwa na mwenyeji wa London na ninahusika sana na eneo ninaloishi. Uwezo wa kuwajulisha wageni wanaotaka kuchunguza eneo hili kuhusu sehemu nzuri zisizojulikana ni jambo la kupendeza kweli.

Ni nini kimekuwa cha kushangaza zaidi kuhusu kukaribisha wageni?

Kufahamu jumuiya ya wenyeji wengine wa Airbnb katika eneo langu na kazi nzuri wanayoifanya. Airbnb sio tu mgeni na mwenyeji, kuna mengine mengi ambayo jumuiya ya wenyeji huyafanya.

Simulizi zingine za wenyeji

Anza kutayarisha tangazo lako