SIMULIZI ZA WENYEJI

Jinsi Dorothee anavyokaribisha wageni

Dorothee hukaribisha wageni jijini Londoni ili ashiriki nyumba yake na watu wengine

Ni nini kilichokupa motisha yako ya kuanza kukaribisha wageni?

Tangu tuliponunua nyumba yetu takriban miaka 11 iliyopita, tumekuwa na wageni wa kulala kila wakati. Hii ni sehemu ya mtindo wetu wa maisha, haswa kwa sababu tuna chumba cha ziada cha kulala ambacho huwa hatukitumii vile. Kufikia sasa hali imekuwa nzuri sana. Tunauleta ulimwengu nyumbani kwetu. Na pia ni njia nzuri ya kupata manufaa kamili ya rasilimali tuliyo nayo - nyumba yetu.

Huwa unawakaribishaje wageni nyumbani kwako?

Ikiwa bado ninafanya kazi wageni wanapofika, kawaida binti yangu hushughulikia utaratibu wa kuingia. Anaipenda sana na anahisi kama ana kazi. Ni utangulizi mzuri kwa wageni wetu, kwa sababu wanatambua kikamilifu kuwa ni nyumba ya familia.

Je, watoto wenu hutangamana na wageni pia?

Watoto huwa wanadokeza "Mnapaswa kwenda kwenye mkahawa ule. Mnaweza kupata kahawa nzuri kule. Msikose kujaribu baga kule. " Wageni wengi huwa wanathamini sana hilo. Wanahisi wamekaribishwa na kana kwamba wanapata kionjo cha maisha ya London Kusini.

Je, kuwa mwenyeji kumebadilishaje jinsi unavyoshughulikia nyumba yako?

Huwa nahakikisha jiko letu ni safi kabisa (si jambo rahisi ukiwa na watoto wawili!) na ninahakikisha bustani ya mbele ni safi na inavutia.

Je, mapato ya ziada kutokana na kukaribisha wageni yamewawezesha kufanya nini?

Huwa tunanua bidhaa katika ujirani wetu, katika masoko ya wakulima, na tunakula vyakula freshi visivyokuzwa kwa kemikali, jambo ambalo hatungeweza kulimudu kama hatungekuwa wenyeji wa Airbnb.

Je, uhuru uliopo kwenye tovuti ya Airbnb, ambapo unaweza kuweka sheria zako mwenyewe, ni jambo muhimu kwako?

Ni muhimu sana, kama inavyotarajiwa ukiwa na watoto wawili. Tuna shughuli chungu nzima na wakati mwingine tunataka nafasi hiyo sisi peke yetu. Ni jambo zuri sana kuwa na uhuru wa kuamua ni wakati upi tunataka kukaribisha wageni.

Mojawapo ya sheria zenu ni kwamba wageni wanakuwa sehemu ya familia yako wanapokaa nanyi. Unaweza kuelezea zaidi?

Wageni wengi wanathamini na kuelewa kuwa - wanapoweka nafasi kwetu, maelezo husema kuwa ni nyumba ya familia. Na ikiwa wako tayari kutangamana na watoto, inakuwa bora zaidi. Kawaida hiyo inamaanisha wakati mwingine sote tutapata kikombe cha chai pamoja jikoni. Tutaongea kuhusu jinsi siku ilivyokuwa kisha kila mtu ataendelea na kile anachokifanya. Ni fursa nzuri kweli ya kutangamana.

Simulizi zingine za wenyeji

Anza kutayarisha tangazo lako