SIMULIZI ZA WENYEJI

Jinsi Tess anavyokaribisha wageni

Tessa hukaribisha wageni jijini Londoni ili apate pesa za ziada.

Ni nini kilichokupa motisha yako ya kuanza kukaribisha wageni?

Nilikuwa na lengo dogo sana nilipoanza kuwa mwenyeji wakati wa Olimpiki. Nilifikiria, "Huenda nikapata pesa za kutosha za kwenda likizo au kuweka mfumo wa kupasha nyumba yangu joto."

Ni nini kimekufanya uendelee kuwa mwenyeji kwa miaka mingi hivi?

Niligundua kwamba, mara tu nilipoanza kupata wageni, ulimwengu wangu ulianza kupanuka papo hapo. Ninaipenda. Mimi ni balozi wa London kwa kuwa nalijua jiji vizuri sana na ninaweza kuwaonyesha watu vitu ambavyo hawavingesoma katika vitabu vya mwongozo. Ninaweza kuwasaidia wengine. Ninathaminiwa na watu.

Je, una vidokezi au ushauri wowote kwa mtu anayefikiria kuwa mwenyeji?

Kuwa na utulivu juu ya nyumba yako na ufurahie.

Je, Garantii ya Mwenyeji ni jambo muhimu kwako?

Ni muhimu kabisa. Ninapenda sana kwamba ninalo hilo la kuniimarisha na kunisaidia. Kwa kweli sijawahi kuhitaji kuitumia. Nimekuwa na wageni wazuri kweli, nimewapa imani, nao wamenipa imani. Lakini hilo linakuja kwa msingi imara wa Garantii ya Mwenyeji.

Je, kuwa mwenyeji kumebadilisha mtindo wako wa maisha?

Ndiyo, bila kifani. Nimeweza kusomea taaluma ya nguo kwa miaka mitatu katika Chuo cha Sanaa cha Morley. Chochote ambacho ningeweza kukishona na kukiunda kwa mikono yangu, nilikifanya. Nimeweza kusafiri. Kuwakaribisha wageni kumenisaidia kulipa usanifu mpya jikoni na maboresho mengine.

Je, kuwa mwenyeji kumebadilishaje jinsi unavyoshughulikia nyumba yako?

Nimejifunza kutoshikamana sana na vitu vyangu.

Simulizi zingine za wenyeji

Anza kutayarisha tangazo lako