Kwa nini utangaze eneo lako kwenye Airbnb?

Unaweza kugeuza sehemu yako ya ziada iwe mapato ya ziada, popote ulipo.
Na Airbnb tarehe 3 Jan 2020
video ya dakika 5
Imesasishwa tarehe 16 Nov 2022

Vidokezi

  • Jipatie pesa za ziada kwa masharti yako

      • Ungana na wageni na usherehekee jumuiya ya eneo lako

          • Pata usaidizi na ulinzi kwenye kila hatua

          Haijalishi malengo yako ni yapi, kukaribisha wageni kwenye Airbnb kunatoa njia ya kufurahisha na inayoweza kubadilika ya kuyatimiza. Unaweza kuwakaribisha wageni katika aina yoyote ya sehemu, popote ulimwenguni, mara chache au mara nyingi kadiri unavyopenda.

          Pesa unayojipatia inaweza kukusaidia kufanya mambo kama vile kulipa bili za nyumba, kuweka akiba kwa ajili ya tukio kubwa maishani au kulipia gharama za likizo yako ijayo. Mbali na kuleta pesa za ziada, kukaribisha wageni kunakupa fursa za kuungana na wasafiri kutoka kote ulimwenguni na kuisaidia jumuiya ya eneo lako.

          Iweke kwenye Airbnb kwa masharti yako

          Unapokaribisha wageni kwenye Airbnb, unachagua jinsi na wakati wa kuwakaribisha wageni. Unaweza kutoa sehemu ya pamoja au ya kujitegemea, iwe uko nyumbani au mbali.

          Ingawa baadhi ya Wenyeji hugeuza ukarimu wao kuwa biashara, wengine huuchukulia kama jambo la kawaida. Unaweza kujaribu kukaribisha wageni ili kwenda sambamba na tukio maalumu katika eneo lako au kuhakikisha kwamba eneo lako linakaliwa unapokuwa likizoni.

          "Ninapenda kujifanyia kazi mwenyewe," anasema Magaly, Mwenyeji Bingwa huko East Wenatchee, Washington. "Ni njia ya maisha inayoweza kubadilika, usawa kamili wa kuwa na uwezo wa kukazia umakini kwa watoto wangu na bado nijitolee kabisa kwenye kazi zinazonipa mapato ya ziada."

          Jipatie pesa za ziada

          Katika utafiti wa hivi karibuni, Wenyeji wengi walisema kwamba wanatangaza sehemu yao kwenye Airbnb ili wajipatie pesa. Wanatumia pesa za ziada ili kusaidia kugharimia kupanda kwa gharama za maisha, iwe ni kwa ajili ya kulipa bili au kuwa na pesa za matumizi ya ziada.

          "Nilianza kukaribisha wageni nilipohamia kwenye nyumba yangu mwenyewe," anasema Yuan, Mwenyeji Bingwa huko Singapore. “Mapato thabiti kutokana na kutangaza chumba changu cha ziada kwenye Airbnb husaidia kufadhili gharama zangu za kila siku, kwa kuwa nilirudi shuleni na sina tena kazi ya wakati wote.”

          Mwaka 2021, Wenyeji wapya ulimwenguni kote walijipatia jumla ya zaidi ya USD bilioni 1.8, ambayo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 30 inapolinganishwa na mwaka 2019. Mapato ya wastani kwa Wenyeji nchini Marekani mwaka 2021 yalikuwa USD13,800, ongezeko la asilimia 85 ikilinganishwa na mwaka 2019. Na fursa za kukaribisha wageni, kuanzia wikendi za mara chache hadi mwaka mzima, zimeendelea kukua mwaka 2022.

          "Tangu tulipotangaza kwenye Airbnb, hatujaangalia nyuma," anasema Robin, Mwenyeji Bingwa huko Mount Barker, Australia. "Tunawekewa nafasi kikamilifu, mwezi mmoja baada ya mwingine na mapato yetu kama Wenyeji, pamoja na pensheni yetu na uwekezaji mwingine, hutupa mtindo mzuri wa maisha."

          Sherehekea jumuiya yako

          Zawadi za kupangisha sehemu yako zinazidi akaunti yako ya benki. Wenyeji wanatuambia kwamba kusherehekea jumuiya zao na kuungana na watu wanaovutia ambao labda wasingekutana nao vinginevyo ni marupurupu mengine maarufu.

          James na Roxanne, Wenyeji Bingwa huko Holetown, Barbados, huwapa wageni wao vitu vilivyotengenezwa katika eneo hilo, kama vile biskuti zilizookwa hivi karibuni kwenye meza iliyo kando ya kitanda, ambazo pia wanauza katika duka dogo kwenye nyumba hiyo. "Wageni mara nyingi hununua idadi kubwa ya Cane Dog Coffee ya eneo hili baada ya kuionja kwenye chumba chao," James anasema.

          Brian, Mwenyeji Bingwa mwenye Hello House Hostel huko Las Palmas de Gran Canaria, Uhispania, anasema kwamba alianza kukaribisha wageni ili kupata uzoefu wa kusafiri wakati anakaa nyumbani. "Wageni ambao tumewakaribisha wamekuwa wa ajabu," anasema, "na tunafurahia sana visa vyao na wanaporudi."

          Weka mipangilio haraka

          Unaweza kubadilisha sehemu yoyote iwe Airbnb. Haijalishi sababu inayokufanya ukaribishe wageni, ni rahisi kuanza.

          • Gundua kile unachoweza kujipatia katika eneo lako au jisajili ili utoe sehemu ya kukaa kwa watu wakati wa shida
          • Pata mwongozo wa moja kwa moja kutoka kwa Mwenyeji Bingwa, chaguo la kumkaribisha mgeni mzoefu kwa nafasi ya kwanza unayowekewa na ufikiaji wa haraka kwa timu iliyopewa mafunzo maalumu ya wahudumu wa Usaidizi wa Jumuiya kupitia Usanidi wa Airbnb
          • Fahamu jinsi unavyolindwa na AirCover kwa ajili ya Wenyeji

          Kuweka eneo lako kwenye Airbnb kunaweza kukuruhusu kutimiza malengo yako ya kifedha, kuungana na watu kutoka kote ulimwenguni na kuwa mjasiriamali kulingana na masharti yako. Unapokuwa tayari kuwapa wageni sehemu ya kukaa, tutakusaidia kwa kila hatua.

          Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu wa ulimwengu wa kukaribisha wageni

          Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

          Vidokezi

          • Jipatie pesa za ziada kwa masharti yako

              • Ungana na wageni na usherehekee jumuiya ya eneo lako

                  • Pata usaidizi na ulinzi kwenye kila hatua

                  Airbnb
                  3 Jan 2020
                  Ilikuwa na manufaa?