Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Mabadiliko ya hivi karibuni kwenye tathmini ya Mwenyeji Bingwa

Tumerejea kwenye vigezo vyetu 4 vya kawaida vya kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa.
Na Airbnb tarehe 20 Ago 2020
Inachukua dakika 2 kusoma
Imesasishwa tarehe 27 Jun 2022

Vidokezi

 • Tumefanya mabadiliko ya muda kwenye tathmini zetu za Mwenyeji Bingwa ili kuisaidia jumuiya ya Wenyeji wakati wa janga la ugonjwa wa COVID-19

 • Kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022, utahitaji kukidhi tena vigezo vyote 4 vya kawaida ili kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa

Janga la ugonjwa wa COVID-19 limevuruga tasnia ya usafiri na taratibu za Wenyeji kote ulimwenguni. Ili kutambua wakati huu tata na mgumu, tumefanya mabadiliko ya muda kwenye vigezo vyetu vya tathmini ya Mwenyeji Bingwa.

Kuanzia mwezi Aprili mwaka 2020, Wenyeji Bingwa waliweza kudumisha hadhi yao bila kukidhivigezo vyetu vyote 4 vya kawaida. Sasa, wakati usafiri unaendelea kurejelea hali ya kawaida, tunarudi kwenye mchakato wetu wa awali wa tathmini.

Kuanzia na tathmini ya tarehe 1 Aprili, 2022 na katika tathmini za siku zijazo, Wenyeji wanahitaji kukidhi vigezo vyote 4 ili kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa.

Vigezo hivyo 4 ni:

 • Kudumisha ukadiriaji wa jumla wa 4.8
 • Kudumisha kiwango cha kutoa majibu cha asilimia 90 au zaidi
 • Kukaribisha wageni kwa ukaaji 10 katika mwaka uliopita (au usiku 100 kwa angalau nafasi 3 zilizowekwa)
 • Kudumisha kiwango cha kughairi cha chini ya asilimia 1
Unapokuwa Mwenyeji Bingwa, unazawadiwa beji maalumu kwenye wasifu na tangazo lako. Tathmini za Mwenyeji Bingwa hufanyika mara 4 kwa mwaka, mwezi Januari, Aprili, Julai na Oktoba na kila tathmini huchanganua utendaji wako katika siku 365 zilizopita.

  Tulianza kuongeza muda wa hadhi ya Mwenyeji Bingwa mwezi Aprili mwaka 2020, tathmini ya kwanza ya Mwenyeji Bingwa wakati wa COVID-19. Hata hivyo, kadiri usafiri unavyoendelea kuimarika, Wenyeji wote watahitaji kutimiza vigezo vyote katika tathmini ya tarehe 1 Aprili, 2022 ili kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa.

  Hivyo vigezo 4 ni kama ifuatavyo:

  • Kudumisha ukadiriaji wa jumla wa 4.8
  • Kudumisha kiwango cha kutoa majibu cha asilimia 90 au zaidi
  • Ukaaji 10 katika mwaka uliopita (au usiku 100 kwa angalau ukaaji tatu kwa Wenyeji walio na nafasi zilizowekwa za muda mrefu)
  • Kudumisha kiwango cha kughairi cha asilimia 1 au chini
  Tathmini ya Mwenyeji Bingwa ya mwezi Aprili itaangalia utendaji wako katika siku 365 zilizopita—kwa hivyo sasa ni wakati wa kufanya marekebisho yoyote ambayo yatasaidia kuhakikisha kwamba umejitayarisha kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa mwezi Aprili.

  Kwa sababu ya vigezo vya tathmini vya Mwenyeji Bingwa katika mwaka uliotangulia wa utendaji ikiwa, kwa mfano, una kiwango cha juu cha kughairi sasa ambacho hakihusiani na COVID-19, hali hiyo inaweza kuathiri hadhi yako ya Mwenyeji Bingwa katika siku zijazo. Fuatilia hadhi yako ya Mwenyeji Bingwa hapa

  Tafadhali kumbuka pia kwamba robo yoyote ya mwaka ambapo Mwenyeji Bingwa anakosa kutimiza chochote kati ya hivyo vigezo 4—ikiwemo sehemu za kukaa na kiwango cha kughairi—haitajumuishwa kwenye zile robo 4 mfululizo za mwaka zinazohitajika ili kupata kuponi ya USD100 ya usafiri au ya Matukio ya Airbnb. Wenyeji Bingwa ambao wanatimiza vigezo vyetu vyote 4 vya kawaida bado watajumuisha robo hizi kwenye kuponi yao.

  Tafadhali kumbuka pia: Ingawa tuliongeza muda wa hadhi kwa Wenyeji Bingwa ambao walikidhi angalau vigezo 2 kati ya vigezo vyetu 4Wenyeji Bingwa bado lazima wakidhi vigezo vyote 4 kwa robo 4 mfululizo ili kupata kuponi ya Airbnb ya USD100. Kwa mfano, ikiwa hadhi yako ya Mwenyeji Bingwa iliongezwa muda mwezi Januari mwaka 2022 lakini hukukidhi vigezo vyote 4 hadi mwezi Aprili mwaka 2022, utastahiki kupata kuponi mwezi Aprili mwaka 2023, ikiwa utadumisha hadhi yako mwezi Julai mwaka 2022, mwezi Oktoba mwaka 2022 na mwezi Januari mwaka 2023.

  Vidokezi

  • Tumefanya mabadiliko ya muda kwenye tathmini zetu za Mwenyeji Bingwa ili kuisaidia jumuiya ya Wenyeji wakati wa janga la ugonjwa wa COVID-19

  • Kuanzia tarehe 1 Aprili, 2022, utahitaji kukidhi tena vigezo vyote 4 vya kawaida ili kupata hadhi ya Mwenyeji Bingwa

  Airbnb
  20 Ago 2020
  Ilikuwa na manufaa?