Mchakato wa kufanya usafi wa hatua 5 ni mkusanyo wa mazoea ya kufanya usafi ambayo Wenyeji wote wanahitajiwa kufuata baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia, pamoja na sheria na miongozo ya eneo husika.
Maelezo kuhusu njia bora ya kufanya usafi yanaweza kupatikana katika Kitabu cha mwongozo wa kufanya usafi cha Airbnb, kinachojumuisha orodha kaguzi za kufanya usafi wa kina.
Unaweza pia kupata kitabu cha mwongozo pamoja na vidokezi, video na kadhalika kwa kutembelea Vidokezi > Kufanya usafi kutoka kwenye akaunti yako ya Kukaribisha Wageni kwenye kivinjari cha wavuti.
Matayarisho mazuri yanaweza kukusaidia wewe pamoja na timu yako kufanya usafi kwa ufanisi na usalama zaidi. Hakikisha kwamba:
Kufanya usafi ni kuondoa vumbi na uchafu kwenye sehemu mbalimbali, kama vile sakafu na sehemu za juu za kaunta. Hakikisha kwamba:
Kutakasa ni pale unapotumia kemikali kupunguza bakteria zilizo kwenye sehemu mbalimbali kama vile vitasa vya milango na rimoti za televisheni. Hakikisha kwamba:
Mara baada ya kumaliza kutakasa, ni wazo zuri kuhakikisha kwamba umetakasa kila mahali. Hakikisha kwamba:
Ili kusaidia kuzuia maambukizi ya kuenea, ni muhimu ukamilishe kufanya usafi na kutakasa chumba kabla ya kubadilisha vifaa kwa ajili ya mgeni anayefuata.
Wenyeji ambao hawatakubali mazoea yetu ya usalama ya COVID-19, ikiwemo mchakato wa kufanya usafi wa kina wa hatua 5, hawataruhusiwa kukaribisha wageni.
Mazoea haya pia yanahitaji uvaaji wa barakoa na kuepuka mikusanyiko unapotakiwa kufanya hivyo na sheria au miongozo ya eneo husika.
Wenyeji ambao wanakiuka viwango vya kufanya usafi mara kwa mara au sana wanaweza kupewa onyo, kusimamishwa na wakati mwingine, akaunti zao zinaweza kuondolewa kwenye Airbnb.