Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sheria

Matakwa ya afya na usalama kwa ajili ya sehemu za kukaa za Airbnb

Wakati wa janga la COVID-19, ni muhimu kuzingatia afya na usalama. Tumetengeneza mkusanyo wa mazoea ya usalama ya lazima ya COVID-19 kwa ajili ya Wenyeji na wageni wa matangazo ya Airbnb, kulingana na mwongozo kutoka kwenye Shirika la Afya Duniani na Vituo vya Marekani vya Kudhibiti Magonjwa. Aidha, unapaswa kufahamu mazoea ya jumla ya afya na usalama kwa ajili ya usalama wa COVID-19, uendelee kufuatilia vizuizi husika vya kusafiri na ushauri wa serikali na ufuate sheria zote za kitaifa na za eneo husika na miongozo.

Airbnb imeanzisha miongozo na mipango ya kusaidia kushughulikia wasiwasi wa kiafya na usalama, lakini hatua hizi haziwezi kuondoa hatari zote. Hasa ikiwa uko katika kundi linalokabili hatari kubwa (mfano: watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 au watu walio na matatizo ya afya kama vile kisukari au ugonjwa wa moyo), tunapendekeza upate mwongozo wa kitaalamu na uchukue tahadhari za ziada unapofanya uamuzi wa kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa au ya tukio kwenye Airbnb. Pata maelezo zaidi kuhusu miongozo ya afya na usalama kwa ajili ya Wenyeji na wageni wa Matukio ya Airbnb.

Mazoea ya usalama ya COVID-19 (inahitajika)

Vaa barakoa na uepuke mikusanyiko unapohitajiwa kufanya hivyo na sheria na miongozo ya eneo husika

Wanapohitajiwa na sheria na miongozo ya eneo husika, Wenyeji wote na wageni lazima wakubali:

 • Vaa barakoa au kifuniko cha uso unaposhirikiana na watu ana kwa ana
 • Dumisha umbali wa futi 6/mita 2 kutoka kwa watu wengine nyakati zote

Fuata mchakato wa hatua 5 wa Airbnb wa kufanya usafi wa kina baada ya mgeni kutoka na kabla ya mwingine kuingia

Wenyeji na wageni wote wanahitajiwa kufuata mazoea ya usalama ya COVID-19 yaliyoainishwa hapo juu, kama inavyofaa, ikiwemo mchakato wa kufanya usafi wa kina wa hatua 5 wa Airbnb baada ya mgeni kutoka na kabla ya mwingine kuingia. Mwenyeji au mgeni yeyote ambaye atakiuka miongozo hii kwa kurudiarudia anaweza kupata adhabu nyinginezo, ikiwemo kuzuiwa kwa akaunti au kuondolewa kwenye jumuiya.

Mwongozo wa ziada wa kusafiri na kukaribisha wageni wakati wa COVID-19

Usisafiri au kukaribisha wageni ikiwa hivi karibuni umekuwa katika hali ya kuweza kuambukizwa au ikiwa una dalili za COVID-19

Ili kulinda afya na usalama wa jumuiya yetu, Wenyeji (na watu wote ambao wanaweza kuwepo kwenye nyumba kabla au wakati wa ukaaji) hawapaswi kuingia kwenye nyumba yao (zao) au kushirikiana na wageni wao na wageni hawapaswi kuingia kwenye nyumba iwapo lolote kati ya mambo yafuatayo ni kweli:

 • Umeambukizwa au umepimwa na kupatikana kuwa na COVID-19 hivi karibuni
 • Unashuku kuwa wewe ni mgonjwa au umekuwa katika hali ya kuweza kuambukizwa na unasubiri matokeo ya kipimo ili kuthibitisha au kukataa utambuzi wa COVID-19
 • Unaonyesha dalili au una wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuambukizwa COVID-19
 • Umekaribiana kwa muda mrefu na mtu aliyethibitishwa au kushukiwa kuambukizwa COVID-19

Kwa maelezo zaidi kuhusu jinsi ya kusafiri kwa uwajibikaji wakati wa janga la ugonjwa wa COVID-19, tathmini makala yetu kuhusu sehemu za kukaa za karantini na kujitenga.

  Nawa mikono yako mara kwa mara

  Hakikisha kwamba unanawa mikono mara nyingi, hasa ikiwa unaingiliana na watu ambao hamkai nao kwenye nafasi uliyoweka na unagusa sehemu mbalimbali na vyombo vilivyo katika sehemu ya pamoja au eneo la pamoja.

  • Nawa mikono yako vizuri kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20.
  • Ikiwa sabuni na maji hazipatikani kwa urahisi, tumia kitakasa mikono kilicho na alkoholi ya angalau asilimia 60; paka kwenye mikono yako na uisugue pamoja hadi ikauke

  Fuata sheria na miongozo ya eneo lako kuhusu barakoa na kuepuka mikusanyiko katika maeneo ya pamoja na sehemu za pamoja

  Unapokuwa katika eneo au sehemu ya pamoja (kama Mwenyeji au mgeni), fuata sheria na miongozo ya eneo lako kuhusu kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko kutoka kwa mtu yeyote ambaye hakai kwenye nafasi uliyoweka. Wenyeji wanapaswa kuzingatia kutoa huduma ya kuingia bila kukutana ana kwa ana pale inapowezekana.

  Kumbuka, ikiwa una wasiwasi kuhusu kukaa kwenye chumba cha kujitegemea au sehemu ya pamoja, zingatia kuweka nafasi ya nyumba nzima badala yake. Ikiwa una wasiwasi kuhusu kukaribisha wageni kwenye chumba cha kujitegemea au sehemu ya pamoja, unaweza kutangaza nyumba nzima, au usitishe shughuli ya kukaribisha wageni ikiwa hiyo haiwezekani.

  Wenyeji wanapaswa pia kufuata miongozo ya eneo husika kuhusu kukaribisha wageni kwenye vyumba vya kujitegemea, sehemu za pamoja na jumla ya idadi ya watu wanaoruhusiwa kukusanyika kwenye nyumba hiyo.

  Kumbuka: Airbnb inadumisha marufuku ya kimataifa kwa sherehe na hafla zote kwenye matangazo ya Airbnb. Soma Sera yetu ya Sherehe na Hafla kwa taarifa zaidi.

  Miongozo ya ziada kwa ajili ya Wenyeji wa vyumba vya kujitegemea na sehemu za pamoja

  Wenyeji wa matangazo ya chumba cha kujitegemea au sehemu ya pamoja wanapaswa pia:

  • Kuweka kikomo cha idadi ya wageni kama inavyohitajiwa ili kuruhusu uepukaji wa mikusanyiko katika maeneo yote ya pamoja pale ambapo sheria au miongozo ya eneo husika inahitaji kufanya hivyo
  • Acha hewa safi iingie kwenye maeneo ya pamoja wakati wa ukaaji, pale ambapo ni salama kufanya hivyo, kama ilivyobainishwa katika mchakato wa kufanya usafi wa kina wa hatua 5
  • Kusafisha na kutakasa maeneo ya pamoja (kama vile mabafu na majiko) mara nyingi kadiri iwezekanavyo

  Baadhi ya serikali zinaweza kuweka vizuizi katika kukaribisha wageni kwenye vyumba vya kujitegemea au vya pamoja au zinaweza kuweka majukumu au matakwa ya ziada kwenye sehemu hizo. Tafadhali hakikisha kwamba unatathmini na kufuata mwongozo wowote wa ziada wa usalama na kufanya usafi kutoka serikalini na/au mamlaka za afya katika eneo lako la kisheria.

  Nini cha kufanya ikiwa utapimwa na kukutwa na COVID-19 wakati wa ukaaji wako au baada ya hapo

  Ikiwa hivi karibuni ulipimwa na kupatikana kuwa na COVID-19 au umeanza kuhisi dalili zozote za COVID-19, wasiliana na mtaalamu wa matibabu na ufikirie kumjulisha mtu yeyote ambaye huenda ameathiriwa au alikaribiana nawe, pamoja na mamlaka za eneo lako.

  Je, makala hii ilikusaidia?

  Makala yanayohusiana