Je, sehemu yangu inafaa kwenye Airbnb?
Vidokezi
Unaweza kutoa chumba cha kujitegemea au cha pamoja, nyumba nzima, au sehemu ya kipekee
Matarajio ya chini kabisa: sehemu ya kulala yenye starehe na upatikanaji wa bafu
Weka matarajio kwa kuwa mkweli kuhusu mazuri na mabaya ya eneo lako
Huenda usifikirie kuwa chumba cha ziada cha kulala au mashua ya kustarehesha inaweza kuwa maarufu kwenye Airbnb, lakini kila aina ya sehemu, kuanzia ndogo zaidi hadi za kipekee zaidi, inaweza kuwavutia wageni.
Haijalishi ni aina gani ya eneo ulilonalo, jambo muhimu ni kuunda eneo zuri la kulala ambalo wewe mwenyewe ungefurahia kulitumia, maelezo ya kina ya tangazo yanayoonyesha kile kinachofanya sehemu yako ivutie.
Anza na mambo ya msingi
Kimsingi, wageni wanatarajia sehemu safi, nzuri ya kulala na ufikiaji wa choo. Si kila eneo lililotangazwa kwenye Airbnb lina jiko, lakini ikiwa wageni wako wanaweza kulifikia, bainisha ikiwa ni jiko kamili au chumba kidogo cha kupikia.
Shiriki sehemu yoyote
Mtu yeyote aliye na sehemu ya ziada anaweza kufanikiwa akiwa Mwenyeji wa Airbnb. Hakuna kitu kama eneo “bora," unahitaji tu kuwa mwaminifu na kuweka maelezo ya kina kwenye tangazo lako na picha ili kuwasaidia wageni waelewa nini hasa cha kutarajia. Kuanzia vyumba vya ziada hadi mitaa ya kifahari, kuna sehemu nzuri kwa kila mtu kwenye Airbnb.
Fafanua aina ya nyumba yako
Karibu kila aina ya nyumba inaweza kuwavutia wageni kwenye Airbnb. Je, ni nyumba? Fleti? Chumba katika kondo yako? Baadhi ya maeneo yametengwa kuwa ya kipekee, kama vile nyumba za kwenye miti, mahema, vijumba, nyumba za shambani, na magari ya malazi na RV.
Chagua ni wapi wageni wanaweza kwenda
Unaweza kuwafahamisha wageni kwamba watakuwa na ufikiaji wa pekee wa nyumba yako nzima, au chumba cha kujitegemea au kwamba watatumia kwa pamoja sehemu kama vile eneo la kulala, jiko au choo pamoja na watu wengine kama vile familia yako, washiriki wa chumba au wageni wengine. Iwe utatenga sehemu yako kwa ajili ya wageni au kuweka vitu vyako hapo ni juu yako kuamua. Mambo muhimu ni sehemu yako kuwa safi na kuwasiliana na wageni kuhusu kipi hasa cha kutarajia.
Kuwa mkweli kuhusu mazuri na mabaya
Daniel, Mwenyeji jijini San Francisco, anasema kuwa kila wakati anakuwa mwazi kuhusu eneo lake. "Kile unachowaambia wageni wako kwamba watakipata na kile wanachokipata wanapowasili kwenye nyumba yako vinapaswa kulingana,” anasema. “Ni bora kuweka matarajio ya chini kwenye tangazo lako kisha wageni wafike na kukuta eneo zuri zaidi kuliko walivyotarajia badala ya kuwaahidi mambo mazuri mno ambayo hayapo kwenye eneo lako."
Onyesha na useme
Ikiwa wageni wanaweza kukutana na wanyama vipenzi katika sehemu ya pamoja, kutaja hili katika maelezo ya tangazo lako ni mwanzo mzuri. Lakini muhimu zaidi ni kupakia picha za mbwa wako mwenye rangi nzuri au paka wako mzuri kwenye Airbnb, ukijumuisha maelezo mafupi kuwafahamisha wageni kwamba kuna uwezekano kwamba watakutana na mnyama.
Picha zinazungumza zaidi kuliko maneno, hasa kwa kuwa baadhi ya wageni wanaweza kuweka nafasi bila kusoma kila kitu vizuri. Ikiwa sehemu yako inajumuisha vipengele vyovyote vya kipekee, pia ni wazo zuri kuthibitisha wakati wa mchakato wa kuweka nafasi kwamba wageni wamesoma tangazo lako kutoka juu hadi chini.
Weka bei ya eneo lako kihalisia
Unaona sehemu yako si kasri, usiwe na shaka! Wageni wengi huthamini makazi ya kawaida ilimradi wanaona yanalingana na pesa waliyotoa. Unapoanza, unaweza kuzingati bei ya utangulizi ambayo ipo chini kidogo ya kile unacholenga. Kufanya hivyo kutakusaidia kuvutia wageni, na mara tu ukipata tathmini nzuri, unaweza kukagua tena na kuongeza bei yako ili kuendana na malengo yako.
Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu wa kuweka tangazo lenye mafanikio
Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.
Vidokezi
Unaweza kutoa chumba cha kujitegemea au cha pamoja, nyumba nzima, au sehemu ya kipekee
Matarajio ya chini kabisa: sehemu ya kulala yenye starehe na upatikanaji wa bafu
Weka matarajio kwa kuwa mkweli kuhusu mazuri na mabaya ya eneo lako