Jinsi ya kuanzisha biashara kwenye Airbnb

Fuata hatua hizi rahisi ili uanze kujipatia pesa kwenye Airbnb.
Na Airbnb tarehe 24 Jun 2022
video ya dakika 10
Imesasishwa tarehe 21 Jul 2023

Vidokezi

Huhitaji kuwa na uzoefu wa kuendesha biashara ili uwe Mwenyeji mwenye mafanikio kwenye Airbnb. Kulingana na simulizi ya Wenyeji Bingwa Bryan na Catherine huko Columbus, Ohio, hakuna yeyote kati yao aliyekuwa na uzoefu wowote wa biashara ndogo au ukarimu kabla ya kuanza huduma ya kukaribisha wageni kwenye Airbnb kwa kutangaza chumba cha ziada cha kulala.

"Miaka minane baadaye, tunakaribisha wageni kwenye nyumba nne tofauti na tunashughulikia kitanda na kifungua kinywa," anasema Bryan.

Ikiwa unafikiria kuhusu kufungua nyumba yako au sehemu nyingine kwa wageni na unajiuliza jinsi ya kuanza biashara ya kukaribisha wageni kwenye Airbnb, uko mahali panapofaa. Hizi hapa ni hatua rahisi za kukusaidia kuanza, kuanzia kuamua ni pesa ngapi unaweza kujipatia hadi kupata maelezo kuhusu mipango ya kila siku inayohusika.

Tathmini soko lako

Kwanza, angalia maeneo mengine kwenye Airbnb na sehemu zinazotoa kitanda na kifungua kinywa katika eneo lako zinazofanana na sehemu yako. Jaribu kufahamu kile wanachotoa na kile wanachokosa ambacho unaweza kutoa.

Fikiria wageni ambao wanaweza kuweka nafasi katika sehemu yako. Je, eneo lako huwapata wasafiri wengi wa kikazi au familia wakati wa likizo? Je, kuna vivutio katika eneo lako, kama vile hifadhi za taifa au maeneo ya kihistoria? Taarifa hii inaweza kukusaidia kufanya maamuzi kuhusu ubunifu, vistawishi na muda wa kukaa ambao ungependa kutoa.

Ni muhimu kujua sheria na kodi zinazotumika kwa upangishaji wa muda mfupi katika eneo lako kabla ya kuanza kukaribisha wageni. Airbnb haiwezi kukupa mwongozo wa kisheria au ushauri wa kodi, lakini tunaweza kukusaidia kupata taarifa kuhusu kanuni za kukaribisha wageni.

Kadiria uwezo wako wa kujipatia mapato

Baada ya kufanya utafiti wa soko, tunaweza kukusaidia kukadiria mapato unayoweza kupata. Unapoweka malengo yako ya mapato, unaweza pia kutaka kufikiria kuhusu matumizi yako na mkakati wako wa bei:

Orodhesha gharama zako
Ili ufahamu faida unayoweza kupata, kadiria gharama zako za mapema—kwa gharama kama vile mapambo, Wi-Fi na mambo mengine ya msingi ili kufanya sehemu yako iwe tayari kwa ajili ya kuwekewa nafasi—na vilevile gharama zinazoendelea au zinazorudiwarudiwa, kama vile mashuka, vifaa vya usafi wa mwili, huduma za kufanya usafi au malipo ya rehani. Hakikisha kwamba unatambua gharama za matengenezo, pia, kama vile ukarabati unaohitajika au ukaguzi wa kila mwaka wa dohani.

"Tunaweka lahajedwali ya gharama na mapato yetu yote, hivyo tunajua kinachoingia na kutoka."
Superhost Bryan,
Columbus, Ohio

Weka mkakati wako wa kupanga bei
Unapoweka mkakati wako wa kupanga bei, fahamu kile ambacho nyumba nyingine za karibu zinazopangisha zinatoza mwaka mzima na jinsi bei yako ya awali ilivyo kwa kulinganishwa na hizo. Unaweza kurekebisha kulingana na uhitaji kwa kusasisha bei yako kimsimu, wakati wa wikendi na hafla kubwa.

Kumbuka kwamba kando na bei yako ya kila usiku, wageni hulipa ada ya huduma na ada zozote za ziada unazojumuisha. Utakuwa na uwezo wa kuongeza bei yako unapoendelea kukusanya tathmini zenye ukadiriaji wa nyota tano, kwa hivyo usiogope kuanzia upande wa chini.

Fikiria upangaji bei kiotomatiki
Ili kufanya bei yako iwe ya kiotomatiki, unaweza kuwasha kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki. Nyenzo ya Upangaji Bei Kiotomatiki huzingatia mambo zaidi ya 70, ikiwemo msimu na uhitaji—na unaweza kuweka bei ya chini ya kila usiku, ili bei yako isiwahi kuenda chini ya kiasi hicho.

Amua jinsi utakavyokaribisha wageni

Kuna njia nyingi tofauti za kukaribisha wageni kwenye Airbnb na baadhi ya Wenyeji wanaweza kutumia muda mwingi kukaribisha wageni kuliko wengine. Fahamu jinsi ambavyo upatikanaji wako unaweza kuwa na uchunguze nyenzo na huduma zinazoweza kuwa na manufaa kwako.

Bryan na Catherine walipoanza kukaribisha wageni, walifanya kila kitu, kuanzia kazi ya kufua hadi matengenezo, Bryan anasema. Hatimaye, waliamua kulipia baadhi ya huduma hizo.

Unaweza pia kufanya baadhi ya vipengele vya biashara yako viwe vya kiotomatiki kupitia nyenzo kama vile ujumbe ulioratibiwa, majibu ya haraka na Kuweka Nafasi Papo Hapo.

Unaamua ni lini na mara ngapi unakaribisha wageni kwenye Airbnb. Ukitumia mipangilio ya kalenda na ya kuweka nafasi, unaweza kuweka upatikanaji wako, kuweka muda wa chini na wa juu wa kukaa na kadhalika.

Wape wageni huduma ya kipekee

Mafanikio yako kama Mwenyeji yanategemea uwezo wako wa kuwapa wageni wako huduma ya kukumbukwa.

Amua ni wageni gani ambao ungependa kuwakaribisha kwenye sehemu yako—kama vile watu walio na wanyama vipenzi, wanandoa, familia au watu wanaofanya kazi wakiwa mbali na utoe vistawishi vinavyokidhi mahitaji yao. Fikiria maelezo ambayo yatafanya tangazo lako lionekane na wageni wako wahisi kuwa wa kipekee, kama vile ujumbe makinifu wa makaribisho au vitu vya ukumbusho vya eneo lako.

"Tulishirikiana na msanii wa eneo letu ili kuchora sehemu za nje za nyumba zetu na kuzigeuza kuwa kadi ndogo za posta ambazo wageni wetu wanaweza kutumia au kutuma nyumbani," anasema Catherine.

Tangaza sehemu yako

Kutangaza sehemu yako kwenye Airbnb hufanywa bila malipo yoyote na unalipa ada ya huduma wakati nafasi iliyowekwa imethibitishwa pekee. Tunalenga kufanya mchakato huu uwe rahisi na wa moja kwa moja: Fuata tu hatua hizi rahisi.

Picha nzuri na kichwa cha tangazo kinachovutia ni baadhi ya mambo ya kwanza ambayo watu hugundua wakati wanavinjari sehemu za kukaa kwenye Airbnb, kulingana na Catherine. Baadhi ya Wenyeji hupiga picha zenye ubora wa juu kwa kutumia simu mahiri au unaweza pia kufikiria kuajiri mtaalamu.
"Tuligundua tofauti kubwa katika nafasi tulizowekewa wakati tuliwekeza katika picha za kitaalamu."
Superhost Catherine,
Columbus, Ohio

Kumbuka kwamba sehemu yoyote inaweza kumfaa mtu. Hakikisha kwamba maelezo na picha za tangazo lako zinaweka matarajio sahihi.

Pata usaidizi kutoka Airbnb

Airbnb inajitahidi kuwasaidia Wenyeji kwa kila hatua, ili uweze kukaribisha wageni ukiwa na uhakika.

Vidokezi

Airbnb
24 Jun 2022
Ilikuwa na manufaa?