Jinsi ya kupanga picha za tangazo ili ziwe ziara ya nyumba

Wavutie wageni wadadisi kupitia mwongozo wa picha wa chumba kwa chumba wa sehemu yako.
Na Airbnb tarehe 29 Sep 2021
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 29 Sep 2021

Vidokezi

  • Unaweza kugeuza galeri ya picha za tangazo lako kuwa ziara ya mtandaoni ambayo imepangwa kulingana na chumba

  • Hakikisha kwamba picha zako za sasa zinaangazia sehemu yako kwa kina, kisha iweke kila moja kwenye eneo sahihi la nyumba yako

  • Sasisha tangazo lako ili litumie kipengele hiki

Chagua, vinjari, weka nafasi. Hivyo ndivyo unavyotaka kila msafiri afanye wakati tangazo lako linajitokeza kwenye matokeo yake ya utafutaji, sivyo? Mara nyingi unaweza kushawishi uamuzi wake wa kukaa kwako—au uendelee kusogeza—kutumia picha unazotoa za sehemu yako.

Mbali na kutumia muda kupiga picha nzuri za tangazo na kuchagua zilizo bora zaidi ili kushiriki, unaweza kufanya nini kuwashawishi wageni? Jaribu kubadilisha matunzio yako ya picha kuwa ziara ya mtandaoni iliyopangwa.

Matunzio yako ya picha yana picha zote ambazo umepakia kwenye tangazo lako. Kwenye skrini ndogo, kama vile simu mahiri, wageni wanaweza kuangalia matunzio yako ya picha kwa kubofya picha ya jalada, ambayo iko peke yake kwenye upande wa juu wa ukurasa wa tangazo lako.

Kwenye skrini kubwa, kama vile kompyuta vibao na kompyuta mpakato, gridi yenye picha 5 inachukua nafasi ya picha moja ya jalada na kuwafanya wageni waelewe vyema zaidi kile kinachofanya eneo lako kupendeza. Wanaweza kuchagua picha yoyote ili kuvinjari galeri yako yote, iliyoonyeshwa kwenye gridi kubwa, yenye mkao wima.

Unaweza kupanga gridi hii kubwa kulingana na chumba au eneo la sehemu yako. Fikiria kama kuwapa wageni ziara ya mtandaoni—fursa ya kupitia kila kona ya sehemu yako kabla ya kuweka nafasi.

Kwa kweli, matunzio yako ya picha yanawaonyesha wageni kile wanachoweza kutarajia kwenye sehemu yako, kila picha ikielezea sehemu tofauti ya hadithi nzima.

Anza kwa kuhakikisha kwamba unatoa picha dhahiri, zenye mwangaza wa kutosha kwenye kila chumba na eneo la nyumba yako linalopatikana kwa ajili ya wageni. Mwenyeji Bingwa Sarah wa Sayulita, Meksiko, anapendekeza kujumuisha "angalau picha 2 za kila chumba cha kulala, kutoka pembe tofauti, ili wageni waweze kuona ikiwa kuna kabati, dawati au chochote kilichopo."

Kabla: Matunzio yako ya picha yanaonyesha picha za tangazo lako kama mkusanyo wa picha ambao wageni wanaweza kusogeza.

Kisha, ikiwa bado hujafanya hivyo, weka picha chache za vistawishi maalumu au maelezo mengine. Hizi zinaweza kujumuisha jiko lenye vifaa vya kutosha, ofisi iliyo na mlango au chumba cha kuchezea cha watoto kilicho na vifaa kamili.

Picha za vipengele vya ufikiaji, kama vile mlango wa kuingia usiokuwa na ngazi au milango mipana, zinaweza kutoa taarifa muhimu pia. Wageni kwa kawaida wanataka kuona kile kinachofanya sehemu yako kuwa ya kipekee—na sehemu nzuri ya kukaa.

Unapofurahia galeri yako ya picha, unaweza kuipanga iwe ziara ya mtandaoni. Sasisha tangazo lako kupitia hatua hizi mbili rahisi:

  1. Chini ya maelezo ya tangazo, chagua Nyumba na vyumba, kisha sogeza chini ili kuhariri Vyumba na sehemu za wazi.
  2. Orodha ya maeneo au vyumba ambavyo wageni wako wanaweza kutumia itaonekana. (Ili kuweka au kuondoa vyumba, nenda kwenye Hariri vyumba na sehemu za wazi.) Chagua chumba kutoka kwenye orodha, chagua kitufe cha Weka picha kisha uchague picha za chumba hiki ambazo ziko kwenye galeri yako ya picha. Rudia utaratibu huo kwa kila chumba.
Baadaye: Matunzio yako ya picha yamepangwa ili wageni waweze kuchunguza picha za tangazo lako chumba kwa chumba.

Kupanga kila picha kwenye matunzio yako ya picha kulingana na chumba mahususi au eneo husaidia kuunda ziara ya kuvutia ambayo ni rahisi kwa wageni kuelewa. Ni SAWA ikiwa una vitu vichache ambavyo ni tofauti na vingine, vinavyowekwa kiotomatiki kwenye sehemu ya Picha za Ziada mwishoni mwa ziara—hakikisha kwamba picha hizi hazijumuishwi na nyingine ili kuepusha mkanganyiko.

Baada ya kusasisha tangazo lako, galeri yako hupangwa kulingana na chumba au eneo. Wageni hupata muhtasari wa nyumba ambayo huwaruhusu kuchunguza kila eneo au wanaweza kusogeza ili kuona ziara nzima. Ziara kwa kawaida huanza sebuleni, kisha huhamia jikoni, vyumba vya kulala, mabafu, maeneo ya nje na sehemu zozote za ziada ulizo nazo katika tangazo lako.

Ni muhimu kukumbuka kwamba kupanga matunzio yako ya picha kulingana na chumba au eneo hakuathiri picha ya jalada au gridi yenye picha 5 upande wa juu wa tangazo lako. Kufanya hivyo ni njia nyingine tu unayoweza kusaidia kuwapa wageni wadadisi taarifa na uhakika wanaohitaji ili kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa kwako.

Vidokezi

  • Unaweza kugeuza galeri ya picha za tangazo lako kuwa ziara ya mtandaoni ambayo imepangwa kulingana na chumba

  • Hakikisha kwamba picha zako za sasa zinaangazia sehemu yako kwa kina, kisha iweke kila moja kwenye eneo sahihi la nyumba yako

  • Sasisha tangazo lako ili litumie kipengele hiki

Airbnb
29 Sep 2021
Ilikuwa na manufaa?