Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Jinsi Brenda ambaye ni mwenyeji wa Airbnb anajipatia mapato ya kustaafu

Kukaribisha wageni kumemruhusu mstaafu mmoja adumishe nyumba ya familia yake na kujikimu.
Na Airbnb tarehe 1 Nov 2018
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 7 Jan 2022

Brenda ambaye ni Mwenyeji wa Airbnb anawakaribisha wageni kwa uchangamfu kwenye nyumba yake ya pili katika kitongoji cha Gentilly huko New Orleans. Brenda alizaliwa na kulelewa huko New Orleans na anajivunia kuwatambulisha wasafiri kutoka kote ulimwenguni nyumbani kwake na jijini mwake. "Nimeishi hapa kwa miaka yangu yote 66 na nimemiliki nyumba hii kwa miaka 32," anasema. "Nilienda shule za umma hapa New Orleans na ninafurahia kuwaonyesha watu jiji langu." Alipoanza kuishi pamoja na mume wake wa pili, Brenda hakutaka kuuza nyumba ambayo alilelea familia yake. Kukaribisha wageni kumemwezesha kudumisha nyumba hiyo na kujikimu wakati wa kustaafu.

Brenda aligundua Airbnb alipokuwa akisaidia kumhamisha binti yake kwenda nchini Uhispania. “Tulikaa katika nyumba ya mwanamke fulani na alituhudumia vizuri. Hata alisaidia kumhamisha binti yangu katika makazi yake. Nilifurahishwa sana na huduma hiyo na nikafikiri 'Ninaweza kumfanyia mtu mwingine vivyo hivyo.'” Sasa anafanya hivyo. Wageni wanapomtembelea, Brenda huwapa kifurushi cha kuwakaribisha chenye asusa na mapendekezo. Pia anahakikisha kwamba wanajua pa kwenda na jinsi ya kufurahia jiji zima. "Ninawapa hotuba yangu ndogo ya 'Bi Brenda'." Mmoja wa wageni wangu alisema ni kama alikuwa anakaa kwenye nyumba ya shangazi yake anayempenda zaidi."

Brenda anapenda kushiriki maarifa yake kuhusu sehemu za burudani za eneo lake pamoja na wageni na kuwatuma kwenye maeneo ambayo si sehemu ya uzoefu wa kawaida wa New Orleans. "Kila mara ninapendekeza kwamba watu waende kwenye Uwanja wa Ndege wa Lakefront ambapo ndege binafsi hutua. Kuna mgahawa mdogo unaovutia zaidi unaoitwa Messina's—una magole bora zaidi ulimwenguni. Kuagiza mawili ni sawa na kuagiza mengi sana kwa sababu yana ukubwa wa sahani," Brenda anasema huku akicheka. "Kisha ninapendekeza Sassafras, ambapo unaweza kupata gumbo halisi zaidi hapa New Orleans. Wanatengeneza gumbo halisi kila siku kutoka mwanzo."

Brenda anaona wageni wake wakisaidia biashara za eneo lake kupitia pesa wanazohifadhi kwa kukaa katika Airbnb yake. "Watu wanaokuja kukaa nami, huenda wasiwe na USD600 za kukaa siku tatu katika hoteli kwenye eneo la biashara la mji lakini kile walichonacho, watachukua kiasi chote na kukitumia hapa New Orleans. Kwa hivyo [guests are] wanatumia pesa zao katika maduka na wanachangia uchumi wetu.

Kwa Brenda, kukaribisha wageni ni njia ya kumfanya aendelee kudumisha nyumba yake na kujikimu kimaisha. Baada ya jeraha lililobadilisha maisha yake, Brenda alilazimika kustaafu mapema kutoka kwenye kazi yake. "Nilifanyiwa upasuaji kwenye shingo yangu na sikuweza kufanya kazi tena." Baada ya Kimbunga Katrina, viwango vyake vya bima na kodi za nyumba viliongezeka zaidi ya mara mbili. “Ukiwa na bili kubwa za maji, umeme, malipo ya bima na kodi za nyumba, umebakisha nini? Marafiki na familia yako pekee.”

Kukaribisha wageni kumetoa chanzo muhimu cha mapato ili kulipia gharama hizi kubwa. "[Hosting is] chanzo changu pekee cha mapato, pamoja na Usalama wa Kijamii." Brenda ana wasiwasi kwamba jiji linaweza kuamua kumnyang'anya mapato haya. Ikiwa jiji litapiga marufuku kabisa vibali vya upangishaji wa muda mfupi kwa nyumba nzima katika maeneo ya makazi, "litakuwa jambo lenye kusikitisha sana na nitakosa kujua la kufanya. Zaidi ya hayo, ninajali zaidi jinsi jiji litatengeneza mapato hayo, mapato ambayo linayapata kutokana na upangishaji wa muda mfupi. Itaathiri mapato yangu sana. Itasababisha mfadhaiko mkubwa sana."

Hatimaye, Brenda anatumaini kwamba jiji litafanya uamuzi wa busara wa kuruhusu watu kama yeye walio na vibali vya upangishaji wa muda mfupi au nyumba za pili, kuendelea kukaribisha wageni kwenye nyumba zao nzima. "Natumaini kwamba watafanya uamuzi unaowaunga mkono wamiliki binafsi wa nyumba, watu ambao wameishi hapa kwa muda mrefu kama mimi." Kupitia kanuni za upangishaji wa muda mfupi za haki na za busara, Brenda anaweza kuendelea kujipatia mapato yenye maana ili kujikimu na kuendelea kuwa balozi bora wa jiji lake linalopendeza.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
1 Nov 2018
Ilikuwa na manufaa?