Anza kwenye Airbnb

Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuanza kukaribisha wageni, kuanzia kuunda tangazo lako hadi kuandaa sehemu yako.
Na Airbnb tarehe 18 Des 2019
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 2 Sep 2021

Vidokezi

 • Angalia kanuni za eneo husika zinazohusu kukodisha nyumba

 • Weka bei yako ya kila usiku na uandae kalenda yako

 • Onyesha kilicho cha kipekee au cha kushangaza kuhusu tangazo lako

 • Fanya usafi, weka vitu muhimu na utoe sheria dhahiri za nyumba

Unda tangazo lako

Fikiria nyumba yako kama tangazo la sehemu yako. Lifanye liwe lenye kuvutia kadiri iwezekanavyo, huku ukiwa mkweli kuhusu vipengele vyovyote vya kipekee.

 • Anza na vitu muhimu. Weka maelezo kama vile mahali eneo lako lilipo, aina ya nyumba unayotoa na idadi ya vyumba vya kulala na mabafu ambayo wageni wako wataweza kufikia.
 • Piga picha za sehemu hiyo. Wageni wanapenda kuvinjari picha wakati wa kufanya uamuzi juu ya mahali pa kukaa. Ili kupiga picha bora, panga kwa unadhifu sehemu yako mapema. Piga picha za kila eneo, ukitumia mwangaza wa asili na katika mwelekeo wa ulalo pale inapowezekana.
 • Angazia maelezo ya kipekee. Unapoandika kichwa na maelezo ya tangazo lako, fikiria ni kipi hufanya eneo lako kuwa maalumu, kama vile mwonekano au bwawa la kuogelea. Pia, angalia mambo yoyote katika maelezo yako ambayo yanaweza kuwa muhimu kwa wageni kujua kabla ya kuweka nafasi, kama vile ngazi au maegesho.

Panga taratibu za usafiri

Hatua yako inayofuata itakuwa ni kuweka sawa taratibu mbalimbali kuhusu nyumba yako ili kufanya mchakato wa kukaribisha wageni uende vizuri.

Andaa sehemu yako

Iwe unatarajia mgeni wako wa kwanza au wa 100, hizi ni hatua utakazohitaji kuchukua ili kuhakikisha sehemu yako iko tayari.

 • Safisha. Safisha kila chumba ambacho wageni wanaweza kufikia, hasa vyumba vya kulala, mabafu na jiko. Hakikisha kuwa hakuna nywele, vumbi au kuvu kwenye sehemu mbalimbali na sakafu na utandike mashuka safi kitandani.
 • Hifadhi vitu vyako vya thamani. Ikiwa una mapambo ya vito, pasipoti au vitu vingine vya thamani, fikiria kuvihifadhi kwenye chumba kilichofungwa, kabati, kasha au kituo cha kuhifadhi. Au unaweza kuviweka kwa ndugu au marafiki.
 • Weka akiba ya vitu muhimu. Ili kuwasaidia wageni kuhisi wapo nyumbani, fikiria kuwapa vistawishi kama vile sabuni, shampuu, karatasi ya choo, mashuka na taulo. Ni bora pia kuwa na vitu vya ziada.
 • Toa maelezo ya kuingia. Kuwa tayari kuwaingiza wageni na kuwatoa, au ajiri marafiki au ndugu wakusaidie. Ikiwa hakuna mtu atakayekuwa karibu, wakati wote unaweza kutumia kisanduku cha funguo au kufuli la kielektroniki na kuwapa wageni maelekezo ya kuingia katika programu ya Airbnb.
 • Weka vitu vya kumalizia. Wageni wanapenda maelezo makinifu. Mwongozo wa nyumba ulio na maelekezo na vidokezi unaweza kusaidia kuwaelekeza wageni. Chupa ya mvinyo au zawadi ndogo pia inaweza kufanya wageni wahisi wamekaribishwa zaidi, lakini si lazima.

Ukishaandaa tangazo lako na sehemu yako, utakuwa tayari kuanza kukaribisha wageni na kupata mapato!

Vidokezi

 • Angalia kanuni za eneo husika zinazohusu kukodisha nyumba

 • Weka bei yako ya kila usiku na uandae kalenda yako

 • Onyesha kilicho cha kipekee au cha kushangaza kuhusu tangazo lako

 • Fanya usafi, weka vitu muhimu na utoe sheria dhahiri za nyumba

Airbnb
18 Des 2019
Ilikuwa na manufaa?