Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuwa jirani mwema

  Heshima lazima ionyeshwe kwa majirani wetu, si jumuiya ya Airbnb pekee. Heshima hiyo inajumuisha kuepuka kuwakera majirani kupitia sherehe zenye mvurugo, hafla, kelele au tabia nyinginezo na matendo yanayosababisha usumbufu.

  Kile tunachoruhusu

  • Sheria zilizobuniwa na Wenyeji: Tunawahimiza Wenyeji waeleze wazi wazi matarajio yao kwa wageni wao katika sheria za nyumba zao, maelezo ya tangazo na kupitia nyuzi za ujumbe wa Airbnb. Airbnb inaweka viwango vya chini, lakini Wenyeji wanapaswa kuzingatia kujumuisha taarifa za ziada au miongozo mahususi kwa ajili ya kitongoji chao.
  • Hafla za huduma ya kitalii ya kiweledi: Ni biashara za huduma ya kitalii ya kiweledi pekee kama vile hoteli au kitanda na kifungua kinywa ndizo zinaweza kuandaa hafla kubwa, maadamu hazivurugi jumuiya jirani au vinginevyo kusababisha usumbufu kwenye jumuiya.

  Kile ambacho haturuhusu

  • Sherehe na hafla zinazosababisha mvurugo: Sherehe au mikusanyiko inayotishia usalama wa jumuiya jirani au inayosumbua jumuiya hiyo hairuhusiwi, bila kujali ukubwa. Jifunze zaidi kuhusu sheria zetu za karamu na hafla.
  • Matangazo ya "nyumba ya sherehe": Isipokuwa wawe wanakaribisha wageni kama sehemu ya huduma ya kitalii ya kiweledi, Wenyeji hawapaswi kuhimiza au vinginevyo kuruhusu sherehe au hafla katika maelezo ya tangazo lao au mahali penginepo.
  • Usumbufu kwa jumuiya: Tabia na matendo yenye kukera yanayojumuisha uvutaji sigara kupita kiasi karibu na majirani au uvutaji sigara katika maeneo ambayo uvutaji sigara ni marufuku, kutupa takataka ovyoovyo, kupiga kelele nyingi mno au kuziba njia ya jirani ya kuingia kwake, hayaruhusiwi.

  Tupo hapa kukusaidia

  Ikiwa wewe au mtu mwingine anahisi kutishiwa au hayuko salama, tafadhali kwanza wasiliana na maafisa wa utekelezaji wa sheria wa eneo husika ili kupata usaidizi. Kwa kuongezea, ukishuhudia au kupitia tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.

  Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kuhusu sera za jumuiya ya Airbnb.

  Makala yanayohusiana