Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Kuwa jirani mwema

Heshima lazima ionyeshwe kwa majirani wetu, si jumuiya ya Airbnb pekee. Heshima hiyo inajumuisha kuepuka kuwakera majirani kupitia mikusanyiko yenye vurugu, kelele au tabia na matendo mengineyo yanayoudhi.

Kile tunachoruhusu

  • Sheria zilizobuniwa na Wenyeji: Tunawahimiza Wenyeji waeleze wazi matarajio yao kwa wageni wao katika sheria za nyumba zao, maelezo ya tangazo na kupitia nyuzi za ujumbe wa Airbnb. Airbnb inaweka viwango vya chini, lakini Wenyeji wanapaswa kuzingatia kujumuisha taarifa za ziada au miongozo mahususi kwa ajili ya kitongoji chao.
  • Hafla za huduma ya kitalii ya kiweledi: Ni biashara za huduma ya kitalii ya kiweledi pekee kama vile hoteli au sehemu zinazotoa kitanda na kifungua kinywa zinazoweza kuandaa hafla kubwa, maadamu hazivurugi jumuiya jirani au vinginevyo kusababisha usumbufu kwenye jumuiya.

Kile ambacho haturuhusu

  • Mikusanyiko yenye kuvuruga: Mikusanyiko inayotishia usalama wa jumuiya jirani au inayosumbua jumuiya hiyo hairuhusiwi, bila kujali ukubwa wake. Pata maelezo zaidi kuhusu sheria zetu za usumbufu wa jumuiya, ikiwemo sheria zetu dhidi ya sherehe na hafla zenye kuvuruga.
  • Matangazo ya "nyumba ya sherehe": Isipokuwa wawe wanakaribisha wageni kama sehemu ya huduma ya kitalii ya kiweledi, Wenyeji hawapaswi kuhimiza au vinginevyo kuruhusu mikusanyiko yenye kuvuruga, sherehe au hafla katika maelezo ya matangazo yao au kwingineko.
  • Usumbufu kwa jumuiya: Tabia na matendo yenye kuvuruga ikiwemo uvutaji sigara kupita kiasi karibu na majirani au kuvuta sigara katika maeneo ambayo uvutaji sigara ni marufuku, kutupa taka ovyo, kupiga kelele nyingi mno au kuziba njia ya jirani ya kuingia kwake, hayaruhusiwi.

Tuko hapa ili kukusaidia

Ikiwa wewe au mtu mwingine anahisi kutishiwa au anahofia usalama wake, tafadhali wasiliana kwanza na mamlaka za utekelezaji wa sheria za mahali husika ili kupata usaidizi. Aidha, ukishuhudia au kukumbana na tabia ambayo inakiuka sera zetu, tafadhali tujulishe.


Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa kutoa mwongozo wa jumla kwa sera za jumuiya ya Airbnb.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili